Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi
Nape Nnauye akisalimiana na baadhi ya viongozi wa CCM baada ya kuwasili
katika mkutano wa kufunga kampeni za Uchaguzi wa serikali za Mitaa za
Jimbo la Ilala, Dar es Salaam, leo jioni.
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM)
kimejigamba kuwa kinaingia kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa kesho,
kikiwa kimeshajizolea maelfu ya nafasi ambazo wagombea wake wamepita
bila kupingwa.
Akizungumza juzi wakati wa mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi huo, jijini Dar es Salaam Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye alisema, kulingana na takwimu CCM imepita bila kupingwa katika vijiji 2708, mitaa 644, na vitongoji zaidi ya 26,300.
Akizungumza juzi wakati wa mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi huo, jijini Dar es Salaam Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye alisema, kulingana na takwimu CCM imepita bila kupingwa katika vijiji 2708, mitaa 644, na vitongoji zaidi ya 26,300.
Wana CCM wakimshangilia Nape alipowasili kwenye mkutano huo
Wananchi wakimshangilia Nape alipowasili kwenye mkutano huo
Nape akiwa Jukwaa Kuu pamoja na viongozi wa CCM baada ya kuwasili kwenye mkutano huo
Lwiza Mbutu akiongoza bendi ya Twanga Pepeta kutumbuiza baada ya kuwasili Nape kwe ye mkutano huo
Twanga akionyesha uhodari wa kuchezambele ya meza kuu
Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es
Salaam, Abilahi Mihewa akisalimia wananchi wa Jimbo la Ilala
waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano huo wa kufunga kampeni za
serikali za mitaa
Kada wa CCM Haji Manara
akiwasalimu wakazi wa Jimbo la Ilala wakati wa mkutano huo. wa kufunga
kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika kwenye makutano ya
mtaa wa Kongo na Faru ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa jimbo la
Ilala ni sehemu salama sana kwa CCM kwa kuwa jimbo hilo lina historia ya
CCM
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es
Salaam Ramadhani Madabida akisalimia wananchi wa Jimbo la Ilala wakati
wa mkutano huo wa kufunga kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa
jimbo la ilala uliofanyika kwenye makutano ya mtaa wa Kongo na Faru.
Mbunge wa Jimbo la Ilala Azani
Zungu akilonga jukwaani, ambapo aliwataka watendaji wa serikali kuacha
kuwabunghudhi mamalishe wa jimbo hilo kwa kuwa ni eneo la biashara tu,
hivyo watendaji hao watengeneze mazingira mazuri badala ya timua timua
ya mara kwa mara
Nape akihutubia kwenye mkutano huo
Nape akihutubia wananchi kwenye mkutano huo na ifuatayo ni habari kamili ya alichosema
Nape akimkaribisha jukwaani Gungu
Mohamed Tambaza, mgombea wa Uenyekiti mtaa wa Mtambani B ili kuomba kura
kwa niaba ya wagombea wenzake wa jimbo la Ilala wakati wa mkutano huo
wa kufunga kampeni za serikali za mitaa uliofanyika leo kwenye makutano
ya mtaa wa Kongo na Faru.
Nape akimsikiliza Gungu Mohamed Tambaza akiomba kura
Kada wa CCM Khamis Mkotya akimpongeza Nape wakati wa mkutano huo
Nape akimpongeza Haji Manara
Mkotya na Zungu
Mkotya na makada wengine wa CCM wakifuatilia
Shamrashamra uwanjani baada ya mkutano. Picha zote na Bashir Nkoromo-theNkoromo Blog
No comments:
Post a Comment