Mwenyekiti
wa Mkesha Mkuu wa Kuliombea Taifa (Dua maalumu), Askofu Godfrey
Mallassy (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari
Dar es Salaam leo, kuhusu mkesha huo utakaofanyika Uwanja wa Taifa,
Desemba 31 mwaka huu. Kulia ni Askofu William Mwamalanga wa Kanisa la
Kiinjili la Kipentecoste Tanzania.
Mwenyekiti
wa Mkesha Mkuu wa Kuliombea Taifa (Dua Maalumu), Askofu Godfrey
Mallassy. Kutoka kulia ni Askofu Nickson Kallinga, Mchungaji Derrick
Luhende, Askofu William Mwamalanga, Makamu Mwenyekiti wa mkesha huo,
Askofu Keneth Dismas, Mchungaji Debora Mallasy (Mjumbe), Mama Mchungaji
Olivia Mallongo (Mjumbe) na Debora Elisha (Mjumbe)
Mchungaji Debora Mallasy (kushoto), akiwauliza swali wanahabari. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa mkesha huo,Askofu Keneth Dismas
Dotto Mwaibale
ASKOFU
Godfrey Mallassy wa Kanisa la Tanzania Fellowship of Churches (TFC),
amesema wasingependa kuona machafuko ambayo yatasababisha kutoweka kwa
amani iliyopo nchini hasa katika kipindi hiki cha kuelekea katika
uchaguzi wa kuwachagua viongozi wa Serikali za Mitaa.
Wanahabari wakiwachukua taarifa hiyo.
|
Pia
alisema kipindi cha kuelekea kuchagua katiba mpya na uchaguzi mkuu pia
kuna kila sababu ya kila mwananchi kuhakikisha anailinda amani ya nchi
iliyodumu kwa muda mrefu.
Akizungumza
Dar es Salaam leo wakati akitoa taarifa kuhusu kufanyika kwa mkesha
mkubwa wa kitaifa, katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam alisema
maandalizi yote yamekamilika hivyo aliwaomba watanzania kufika kwa wingi
kwa ajili ya dua hilo ambalo hufanyika kila mwishoni mwa mwaka.
Maombi yakifanyika baada ya mkutano huo. |
Alisema
hakuna taifa lolote duniani ambalo linapenda kupoteza amani yake kwani
amani ni mfano wa yai ambalo kama likianguka na kupasuka haliwezi kurudi
tena.
Pia
alitumia fursa hiyo hiyo kuwaasa waandishi wa habari kuandika habari za
usawa na kuacha kuandika habari za kupotosha jamii kwani kufanya hivyo
kunaweza kuhatarisha nchi.
“Tunaenda
kuelekea uchaguzi mkuu mwaka 2015 na kuchagaua katiba mpya hivyo basi
ni vyema kuandika habari za ukweli na si za uchochezi kwani kwenda
kinyume na maadili ya kazi zenu mnaweza kuupotosha umma ukizingatia kuwa
ninyi ni muhimili wa nne wa nchi usio rasmi. “alisema.
Maombi yakifanyika ndani ya Ukumbi wa Habari Maelezo baada ya kumalizika kwa mkutano huo. |
Akizungumzia
mkesha huo alisema mkesha huo utafanyika katika mikoa mingine 16,ambayo
ni Dodoma, Kilimanjaro, Lindi, Mtwara, Iringa, Kagera, Ruvuma, Mbeya na
Singida.
Alitaja
mikoa mingine kuwa ni Morogoro na Simiyu na lengo la mkesha huo ni
kumshukuru mungu kwa awamu ya nne ya uongozi wa taifa na kuliombea taifa
letu na mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya na uchaguzi mkuu 2015.
“Taifa
lolote linatakiwa kuombewa kutokana na kupata maendeleo yaliyo kamili
hivyo basi sisi wanadamu pekee hatuwezi kupata amani kwa siasa na Jeshi
ila mwenyezi mungu pekee,” alisema.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)
No comments:
Post a Comment