Mshindi
wa Big Brother 2014,Idris Sultan akizungumza na waandishi wa habari
(hawapo pichani) katika hoteli ya Hyatt Regency,Jijini Dar es salaam
leo,wakati akizungumzia ushindi wake na uzoefu alioupata katika Jumba
hilo la Big Brother huko nchini Afrika Kusini.Kulia ni Meneja Masoko wa
Kampuni ya MultiChoice Tanzania,Furaha Samalu na kushoto ni Meneja
Uhusiano wa Kampuni ya MultiChoice Tanzania,Barbara Kambogi.
Mshindi wa Big Brother 2014,Idris Sultan akisisitiza jambo wakati
akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika hoteli ya Hyatt
Regency,Jijini Dar es salaam leo.
Idris akizungumza.
Alikuwa Mshiriki mwenza wa Idris Sultan,Irene Laveda akizungumza machache kwenye Mkutano huo.
Meneja
Uhusiano wa Kampuni ya MultiChoice Tanzania,Barbara Kambogi akizungumza
jambo wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam
leo.
Sehemu ya Waandishi wa habari waliofika katika Hoteli ya Hyatt Regency kumsikiliza Mshindi wa Big Brother 2014,Idris Sultan.
Mshindi wa Big Brother 2014,Idris Sultan (pili kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Meneja
Masoko wa Kampuni ya MultiChoice Tanzania,Furaha Samalu (pili
kulia),Meneja Uhusiano wa Kampuni ya MultiChoice Tanzania,Barbara
Kambogi (kushoto) pamoja na Mwanalibeneke Othman Michuzi a.k.a Mzee wa Mtaa kwa Mtaa
Wadau wakipiga picha ya pamoja na Idris na Laveda.
Mpiga picha na Blogger,Salma Msangi kazini.
Na Bakari Issa,Dar es Salaam
Mshindi
wa Big Brother Africa 2014,Idris Sultan ameeleza siri ya
mafanikio yake katika shindano lililomalizika hivi karibuni nchini
Afrika ya Kusini mbele ya waandishi wa habari waliofika kumsikiliza
leo kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Idris
alifanikiwa kupata ushindi huo baada ya kupigiwa kura na nchi
tano ambazo ni Tanzania,Kenya,Uganda,Rwanda pamoja na Namibia na
kutwaa Dola za Kimarekani 300,000 sawa na shilingi Milioni 500
za Kitanzania na kufanikiwa kumbwaga mpinzani wake,Tayo kutoka nchini
Nigeria.
Idris
amesema kuwa ushindi huo ni kwa ajili ya mashabiki hususan
waliompigia kura wakati akiwa katika jumba la Big Brother
huko Afrika ya Kusini na kutoa shukrani kwa nguvu,bidii ambazo
watu walimuekea yeye na kupata ushindi huo.
“Ushindi
huu si wa kwangu peke yangu bali ni ushindi wa mashabiki ambao
waliniwekea nguvu pamoja na bidii na kufanikisha ushindi huu,”alisema
Idris.
Pia
Idris amezitaja changamoto alizokutana nazo katika jumba la Big
Brother kuwa ni kutokumjua mtu kama anakurekebisha au anakutoa
kwenye njia,hivyo basi kushindwa kujua njia sahihi ya kushindana.
“Kutokujua
Waafrika wanafikiriaje, hauwezi kujua mtu anakurekebisha au
anakupotosha au anakutoa kwenye njia,unashindwa kufahamu hiyo ndiyo
changamoto niliokutana nayo,”alieleza Idris
Aidha,
amewataka washiriki wa Tanzania watakaokuja kushirika shindano
hilo,wasifikirie watu wanafanya nini ndani ya jumba bali wafanye wao
kama wao na sio kumuiga mtu mwingine.
No comments:
Post a Comment