Wananchi wa kijiji cha Kitelewe wakishiriki kubeba bomba za maji zilizotolewa msaada na mbunge wao Filikunjombe |
Wannchi wa Kitewele wakimpokea mbunge Filikunjombe kushoto |
Baadhi ya wananchi wa kitewele wakiwakatika mkutano huo |
Wananchi wakimsikiliza mbunge wao kwa makini |
Mbunge Filikunjombe kulia akijibu swali la mkazi wa kijiji cha Kitelewe kushoto huku wakifurahi wote baada ya majibu mazuri ya kutaka wazee na vijana kuungana kushiriki katika maendeleo |
WANANCHI wa Kijiji cha KITEWELE kata
ya MAWENGI wilaya ya LUDEWA mkoani Njombe , wanatarajia kuanza kunufaika
na huduma ya maji safi na salama ya bomba baada ya kukamilika kwa
ununuzi wa vifaa ikiwemo mabomba ya kutandika ardhini ambayo yamegharimu
kiasi shilingi zaidi ya Milioni 26 msaada uliotolewa na mbunge wa
jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe .
Akizungumza leo na wananchi hao
mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo mbunge Filikunjombe alisema
kuwa kukabidhi kwa vifaa hivyo na mradi huo wa maji ni utekelezaji wa
ahadi yake ya maji kwa wananchi hao aliyoitoa mwaka 2012 kufiatia ombi
la wananchi hao zaidi ya 800 waliokuwa wakikabiliwa na adha ya maji .
Mbunge Filikunjombe alisema
kuwa toka nchi itape uhuru mwaka 1961 wananchi hao hawajapata kuwa
na maji safi na salama na kuwa miaka yote wamekuwa wakitumia maji
ya mito ambayo si safi na salama kabla ya kufika na kuombwa
kuwasaidia kupata huduma hiyo ya maji safi .
“Ndugu zangu nikiwa kama
mbunge wenu nimekuwa nikiumia zaidi kuona wananchi wangu
mnapata shida ya maji na ndio sababu ya kuahidi kuungana nanyi
katika kuwafikishia huduma ya maji….ombi langu kwenu tuzidi
kushirikiana ili kutatua kero zetu bila kusubiri wahisani “
Miaka miwili iliyopita, Mbunge
wa Jimbo la Ludewa, DEO FILIKUNJOMBE alishuhudia kadhia hiyo akiwa
katika Zahanati ya kijiji hicho na akawaahidi wananchi kuwafikishia
maji, ahadi ambayo ameitekeleza mwaka huu na kukabidhi mabomba kwa
wananchi yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 20 tayari kwa kuanza
kazi ya kuchimba mitaro na kutandika mabomba hayo.
Hata hivyo alisema kuwa
maendeleo ya wananchi wa KItelewe na jimbo la Ludewa yataletwa
na wananchi wenyewe kwa kuunganisha nguvu zao pasipo kusubiri
wahisani na kuwa baadhi ya maeneo ya wilaya hiyo wananchi siku
zote wamekuwa wakijitolea kushiriki katika maendeleo mbali mbali.
Akielezea kuhusu adha ya maji
katika jimbo lake na jinsi alivyoshiriki kutatua alisema kuwa yapo
maeneo ambayo wananchi wamekuwa na adha kubwa ya maji na tayari
ameanza kumaliza kero hiyo.
Kwa upande wake diwani wa viti
maalum tarafa ya Mawengi Bilgeter Haule aliema kuwa moja ya vitu
ambavyo wana Ludewa wanajivunia ni kumpata mbunge ambaye
anawajibika kwa wananchi kama ilivyo kwa mbunge huyo.
“ Tanzania mtu ambae hatakuj
kusaulik ni pamoja na baba wa Taifa mwalimu Julius Nyerere ambae
alitanagazwa kuwa mwana heri ila kwetu Ludewa kutokana na kero
tulizozipata toka uhuru hadi leo ambapo zinapatiwa ufumbuzi kwa
pamoja tutamkumbuka mheshimiwa mbunge wetu Deo Filikunjombe kama
mwanaheri baada ya kutatua kero zetu na kuondoka katika kundi la
watanzania wasiofurahia uhuru wao”
No comments:
Post a Comment