theNkoromo Blog, Kinondoni
Manispaa ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, imedhihirisha jitihada zake za kwenda na wakati katika huduma zake, baada ya kuamua kutoa huduma ya bure ya mtandao wa intrenet wa WiFi kwenye Kituo kipya cha Mabasi cha Sinza, jijini Dar es Salaam.
Manispaa ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, imedhihirisha jitihada zake za kwenda na wakati katika huduma zake, baada ya kuamua kutoa huduma ya bure ya mtandao wa intrenet wa WiFi kwenye Kituo kipya cha Mabasi cha Sinza, jijini Dar es Salaam.
Akizindua huduma hiyo, jana, Meya
wa Manispaa ya Kinondoni, Yussuf Mwenda alisema, mtandao wa WiFi
umeunganishwa kwenye kituo hicho kupitia mkongo wa mawasiliano kupitia
Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL).
Mwenda alisema, mtandao huo
utakuwepo usiku na mchana na kila mwenye kompyuta au simu zenye uwezo wa
kunasa Wi-Fi ataona katika simu au kompyuta yake akitaarifiwa kuwepo
mtandao wa bure wa KMC_FREE WiFi.
Alisema, mdau atakachofanya ni
kujinga bure na kuendelea kupata taarifa mbalimbali zikiwemo za tovuti
ya serikali na ya Manispaa hiyo ya Kinondoni na nyingine zote
atakazotaka.
Mwenda alisema, baada ya kuweka
mtandao kwenye Kituo hicho, mwakani Manispaa hiyo itaweka mtandao huo wa
WiFi kwenye Kata zote 34 za Manispaa hiyo.
Alisema, mradi huo wa WiFi
umegharimu sh. milioni 21, na Manispaa hiyo itakuwa ikiendelea kulipia
huduma hiyo sh. milioni 2 kila mwezi ambazo itakuwa inalipa kwa mkupuo
kwa mwaka.
Kuzinduliwa kwa huduma hiyo,
kumeifanya Manispaa ya Kinondoni kuwa ya kwanza nchini kote, na pengine
hata Afrika Mashiriki, kutoa huduma hiyo bure tena bila kutumia namba ya
siri.
Mwandishi wa habari hii
alishuhudia huduma ya aina hii kwa mara ya kwanza alipotembelea nchini
China, ambapo WiFi inapatikana bure kwenye simu hata ukiwa barabarani.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni,
Yussuf Mwenda akibofya kompyuta kuzindua huduma ya WiFi ya bure kwenye
Kituo cha Mabasi cha Sinza, wilayani humo, Ijumaa, Desemba 12, 2014
Mwenda akizungumza baada ya kuzindua huduma hiyo
Mwenda akikata utepe kwenye
chumba ilimo mitambo ya kuendesha mtandao huo wa huduma ya WiFi kwenye
Ofisi za Kituo hicho cha mabasi
Baadhi ya wafanyakazi katika ofisi hiyo yenye kugawa WiFi
Kweli: “WiFi ya Manispaa ya
Kinondoni inapatikana bure! vijana wakisema baada ya kuipata WiFi
iliyozinduliwa kwenye Kituo hicho cha Mabasi
Vibao vinavyoonyesha Mabasi yaendeko kutoka kwenye Kituo hicho
No comments:
Post a Comment