Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo akishangaa uchafu ulio kithiri eneo la makoroboi .Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo akiwa katika Eneo la Soko kuu. .Eneo la Pembeni ya iliyokuwa standi kuu ya Mwanza, ambapo Mulongo ametoa siku ishirini na moja pawe pameendelezwa. Mkuu
wa Mkoa akimsikiliza Bibi Asia Rashidi mfanyabiashara wa soko kuu
wakati wa ziara hiyo (Picha zote na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza
………………………………………………………………………………..
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa
Mulongo amekerwa na hali ya uchafu iliyopo katika mitaa ya Jiji la
Mwanza na kuwaagiza watendaji wa halmashauri hiyo kuacha kukaa
ofisini na badala yake watoke na kwenda kuwasikiliza watu katika maeneo
yao ya kibiashara.
Mulongo ametoa kauli hiyo jijini
Mwanza, mara baada yakufanya ziara yakutembelea maeneo yaliyotengwa
maalumu kwa ajili ya wafanyabiashara ndogondogo Jijini humo na kukuta
hali ya mazingira kiafya ikiwa hairidhishi.
Mkuu huyo wa mkoa akiwa
ameambatana na kamati ya Ulinzi na usalama ya Mkoa alitembelea maeneo ya
Makoroboi, Soko kuu, Sahara na Standi ya Nyegezi.
Aidha katika hatua nyingine
ameuagiza uongozi wa jiji hilo kuhakikisha wana viainisha vikundi vidogo
vidogo vinavyo undwa na vijana pamoja na kina mama ili viweze
kukabidhiwa jukumu la kutunza mazingira badala ya kazi hiyo kuachiwa
mawakala wa usafi ambao kwa namna moja au nyingine wameonekana kulemewa
na jukumu hilo .
” Tunacho taka kuona ni hawa
samaki wadogo wadogo na wao wanakuwa na kuvuka hatua hii waliyo nayo na
kukuza mitaji yao, alisema Mulongo na kuongeza kuwa, wenye kutaabika na
hali mbaya ya usafi sehemu zote ni hawa wanao kaa katika maeneo hayo.
Alitoa agizo hilo kwa uongozi wa
Jiji la Mwanza kufuatia majibu yaliyo tolewa na Afisa afya wa jiji bw.
Kamenya kwamba wao kama jiji huwalipa mawakala kiasi cha Tsh. 1000 kwa
kila mita miatatu za usafi wanazo zifanyia usafi, suala ambalo lilizua
mjadala na kumlazimisha mkuu wa mkoa kuugaiza uongozi wa jiji kuachana
na mpango huo na badala yake wawatambue kwanza watu wanao kaa katika
maeneo husika ndio wapewe jukumu lakutunza usafi ” Pale Moshi, wenzenu
walichofanya ni kuwaweka vijana na akina mama katika vikundi na kisha
kuwaelekeza nini cha kufanya.
Amesema endapo vikundi hivyo
vikiwezeshwa ndivyo vinaweza kufanya suala la usafi kupata suluhisho la
kudumu la usafi, kwakuwa watakuwa na uchungu wakimuona mtu yeyote
anathubu kuchafua mazingira wao watakuwa wakwanza kumkemea na kumfikisha
kwenye mamlaka husika kwa ajili ya hatua stahiki.
Mkuu huyo wa mkoa tangu
aliporipoti na kujitambulisha amefatilia kwa karibu suala la ujenzi
Maabara pamoja na hali ya usafi katika Jiji la Mwanza, ambapo siku zote
amekuwa akinukuliwa akisema anataka kila mmoja atomize majukumu ya kazi
aliyo ajiriwa nayo kwa ufanisi bila kutegea.
(Picha na habari na Afisa habari Mwanza zaidi soma Mwanzareview.blogspot.com)
No comments:
Post a Comment