Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga akifungua Mkutano huo. Mratibu wa Afya ya mama na Mtoto mkoani Mwanza Secilia Mrema akitoa ufafanuzi mbele ya waandishi wa habari. Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Drt. James Kengia akitoa ufafanuzi wa maswali ya wadau waliokutana. Bw. Stanley Matowo, mataalam wa maji kutoka sekretarieti ya mkoa wa mwanza akichangia katika kikao hicho.Shekhe
wa Mkoa wa Mwanza Hassan Fereji akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kwimba
Seleman Mzee wakifatilia kwa karibu mtoa mada katika kikao hicho
…………………………………………………………………
Na: Atley Kuni-(Afisa habari Mwanza).
Mkoa
wa Mwanza umejiwekea malengo makubwa ili kukabiliana na afya ya uzazi
na malezi bora kwa mtoto ili kuweza kufikia malengo ya milennia ifikiapo
Desemba 2015.
Hayo yamesemwa na bibi Secilia
Mrema wakati akiwasilisha mada kwenye kikao cha pamoja kilichokutana
katika ofisi ya mkuu wa mkoa na wadau wa masuala ya afya mkoani hapa kwa
ajili yakupitia mipango waliojiwekea lakini pia kupeana majukumu ili
kuweza kufikia azma yao hiyo.
Mrema amesena, kutokana na hali ya
uzazi salama kuwa chini ukilinganisha na mikoa jirani kama vile Kagera
ndio maana wameamua kukaa pamoja ili waone kwa namna gani wanaweza
kutoka mahali walipo na kufikia malengo waliojiwekea ifikiapo mwishoni
mwa 2015.
Amesema kutokana na Uelewa mdogo
juu ya njia za uzazi salama kwa watoa huduma na kwa jamii, Mila na
desturi zinazofanya utumiaji mdogo wa huduma za afya ya uzazi na uzazi
wa mpango, ushiriki mdogo wanaume ni baadhi sababu kubwa iliyo wasukuma
kuja na mikakati hiyo, lakini pia kutokana na mpango wa Tekeleza sasa
kwa matokeo makubwa (BRN) ni njia moja wapo ya visababishi vilivyo
wafanya kuja na mikakati hiyo “ Tunajua suala la afya ya uzazi ni jukumu
la jamii nzima ndio maana tumeona ni vema tuka kaa wadau wote tunao
husika ili tuweze kuangalia kiunaga ubaga mikakati hii tuliojiwekea.
Kutokana na changamoto hizi mkoa kwa kupitia halmashauri za wilaya umejiwekea malengo yafuatayo
Kupiga vita mila na desturi
zinazofanya utumiaji mdogo wa huduma za afya ya uzazi kama vile,
uzazi wa mpango, ushirikishwaji wa wanaume, Kuongeza kiwango cha
wajawazito kujifungulia kwenye vituo vya kutolea huduma za afya kutoka
68%-80% ifikapo desemba 2015, kuongeza kiwango cha huduma baada ya
kujifungua ndani ya siku 7 kutoka 21% mpaka 62% ifikapo Decemba 2015,
kuongeza kiwango cha watoto wanaozaliwa na kina mama wenye maambukizi ya
VVU kutumia ARV (prophylaxis) kutoka 45% to 65% ifikapo Decemba 2015
kuongeza namba ya vituo vinavyotoaa huduma ya IMCI kutoka 69%-80%
ifikapo Desemba 2015, mbali ya mikakati hiyo vilevile mkoa umedhamiria
Kuboresha utoaji wa taarifa kwa wakati kutoka 66%-100% ifikapo Decemba
2015.
Mrema amekwenda mbali zaidi
nakusema ili waweze kufikia malengo waliojiwekea watatoa mafunzo kwa
watoa huduma kuhusu (njia za kisasa za uzazi wa mpango, huduma za
dharura wakati wa uchungu na kujifungua, huduma ya kumsaidia mtoto
mchanga kupumua baada ya kuzaliwa, IMCI, mtuha). Aidha kupitia vyombo
vya habari watatumia mwanya wakutoa elimu kwa umma ili wajue umuhimu wa
afya ya uzazi lakini pia kufanya mikutano mingi ya uraghabishaji kwa
umma ili ufahamu umuhimu wa masuala ya afya ya uzazi kwa mama na mtoto.
Mkoa wa Mwanza ni mojawapo ya
mikoa 6 inayo unda kanda ya Ziwa ambao una wilaya ziapatazo saba zenye
visiwa 68. Huku mkoa huo kwa mujibu wa sensa ya watu na makaazi ya
mwaka 2012 ikiwa jumla ya watu wapatao 2,772,509, idadi ya watoto chini
ya mwaka mmoja ikiwa ni 104,507, na watoto watoto chini ya miaka 5
ikiwa ni 516,998 huku wanawake wenye umri wa kuzaa kwa maana ya umri
kati ya miaka (14-49yrs) ni 677,100.
Mrema amesema, wastani wa watoto
katika familia ni 5.4 (Fertility rate), na ukuaji wa wakazi kwa maana
ongezeko la watu kimkoa ikiwa ni 3.2% kwa mujibu wa sense ya 2012, aidha
mkoa pia una jumla ya vituo vya kutolea huduma za afya 360 kati ya
hivyo vituo 263 (73) % vinatoa huduma za afya ya uzazi na mtoto.
Awali akifungua kikao hicho Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo katika hotuba yake iliyosomwa na Mkuu
wa Wilya ya Nyamagana alisema ni jukumu la kila mmoja wetu “kujihoji ni
kwa vipi mama apoteze maisha ili hali kila mmoja wetu anajua kuwa mama
ndiye anaye tengeneza maisha”? aidha amesema kuwa kutokana na lengo la
nne la millennia kugusa suala nyeti kama hili ndio maana kama taifa
tayari tathimini ilifanyika ambapo Wakuu wa Mikoa yote Tanzania Bara,
Makatibu Tawala na Waganga Wakuu wa Mikoa Tanzania walikutana na
Mheshimiwa Rais tarehe 15 Mei, 2014 na kupewa taarifa ya tathimini hiyo
na kujadili mkakati mpya ulioboreshwa wa kitaifa katika kufikia lengo la
4 na la 5. Ifikapo mwishini mwa mwaka 2015, “Pamoja na mengine
tuliyokubaliana mbele ya Mheshimiwa Rais, suala la uwajibikaji lilipewa
kipaumbele ambapo kila mmoja wetu aliweza kupata uzoefu wa mikoa
mingine, mfano Singida na Mara jinsi walivyofaulu katika suala la afya
ya uzazi.
Kikao hicho cha siku moja
kimewakutanisha Viongozi wa dini, wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa
halmashauri, wenyeviti wa halmashauri, waganga wakuu wa wilaya na
waratibu wa afya ya uzazi wa wilaya pamoja na wataalam kutoka
sekretarieti ya mkoa wa Mwanza.
Imeandaliwa na Afisa habari- Mwanza- ofisi ya Mkuu wa mkoa. soma zaidi na picha kupitia: www.mwanzareview.blogspot.com
No comments:
Post a Comment