JINA la Rose Muhando ni mojawapo
ya majina yanayofanya vizuri katika muziki wa Injili barani Afrika
hasa kutokana na uwezo wake jukwaani pindi anapofikisha uinjilishaji kwa
waamini na mashabiki mbalimbali.
Muhando ni mzaliwa wa kijiji cha
Dumila, wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro, Tanzania, Afrika Mashariki
na ni mwimbaji wa nyimbo za injili kwa lugha ya Kiswahili ambaye umahiri
wake awapo jukwaani umefanikisha kutambulika barani Afrika.
Rose atakayepanda jukwaani
kuanzia Desemba 25, Agosti 3 mwaka huu alizindua albamu yake Kamata
Pindo la Yesu yenye nyimbo za ‘Facebook’, ‘Bwana Niongoze’, ‘Wewe
Waweza’, ‘Usiniache’, ‘Nibariki na Mimi’, ‘Usivunjike Moyo’ na ‘Kwema’.
Awali Rose kabla hajawa Mkristo
alikuwa Muislam na ni mama wa watoto watatu. Alimpokea Yesu Kristo pale
alipokuwa anaumwa na yuko kitandani akiwa na umri wa miaka 9, aliugua
kwa muda wa miaka mitatu na baadae alipona na kubadili dini na kuwa
Mkristo.
Rose alizama kwenye muziki
katika kwaya iliyoko Dodoma na alikuwa mwalimu wa Kwaya katika kwaya ya
Dodoma St. Mary’s katika kanisa la Kianglikana la Chimuli.
Januari 31 mwaka 2005, Rose
Muhando alizawadiwa tuzo ya Mtunzi bora wa nyimbo za Injili, Mwimbaji
Bora na albamu Bora ya Mwaka. Tuzo hizo zilitolewa katika Tamasha
Tanzania Gospel Music Awards, 2004
Desemba mwaka 2005 alihudhuria
katika tamasha la Nyimbo za Injili katika kusaidia kuchangia kwa watoto
na wajane Dar es Salaam ambapo alitekeleza ipasavyo uchangiaji huo.
Februari 2011, Rose Muhando
alisaini mkataba na Mult Album Recording Deal na Kampuni ya Sony Music
ya Afrika Kusini. Kusaini huko kulitangazwa katika mkutano wa waandishi
wa habari Dar es Salaam, Tanzania na hiyo ni mara ya kwanza kufanyika
Afrika Mashariki.
Baadhi ya albamu za Rose Muhando ni:
1. Mteule uwe macho, 2004
2. Kitimutimu, 2005
3. Jipange sawasawa, 2008
4.Utamu wa Yesu 2012
4.Kamata Pindo la Yesu 2014
Tuzo alizopata
2005 -Tanzania Music Awards: Mwimbaji Bora wa Kike Nyimbo za Dini (“Mteule uwe macho”)
2009 – Mwimbaji Bora wa Nyimbo za Injili
2008- Alitunukiwa tuzo nchini Kenya ya Mwimbaji Bora wa Injili Afrika
Amewahi kuzawadiwa kitita cha Sh200,000 na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC).
No comments:
Post a Comment