TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, June 29, 2016

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AKUTANA NA RAIS WA COMORO PAMOJA NA BALOZI WA JAPAN NCHINI JIJINI DAR ES SALAAM



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akizungumza na Rais wa Comoro Mhe.Azali Assouman walipokutana kwenye uwanja wa ndege wa Dar es Salaam ambapo Rais huyo wa Comoro alikuwa kwenye mapumziko mafupi kabla ya kuendelea na safari ya kwenda Macca kwenye ibada ya Umrah nchini Saudi Arabia.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (wa tatu kutoka kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa Comoro Mhe.Azali Assouman na ujumbe wake walipokutana kwenye uwanja wa ndege wa Dar es Salaam ambapo Rais huyo wa Comoro alikuwa kwenye mapumziko mafupi kabla ya kuendelea na safari ya kwenda Macca kwenye ibada ya Umrah nchini Saudi Arabia.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Japan nchini Mhe. Yoshida Masaharu Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo Balozi wa Japan Nchini alisema nchi yake imeridhishwa na kasi ya Serikali ya Rais Mhe. Magufuli na kuahidi kuendelea kuisaidia Tanzania

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Japan nchini Mhe. Yoshida Masaharu mara baada ya mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Comoro AzaliI Assouman amesema serikali yake itaendelea kudumisha uhusiano na ushirikiano wa kihistoria kati ya Tanzania na Comoro katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu,afya na biashara.

Rais huyo wa Comoro ametoa kauli hiyo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya Rais John Pombe Magufuli akiwa kwenye mapumziko mafupi kabla ya kuendelea na safari yake ya Mecca – Saudi Arabia kwa ajili ya ibada ya UMRAH.

Rais Azali Assouman pia amepongeza jitihada zinazofanywa na serikali ya awamu ya Tano zinazolenga kuhakikisha wananchi wa Tanzania wanapata huduma bora za kijamii na kusisitiza kuwa serikali yake itaendelea kujifunza kutoka Tanzania ili kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wa Komoro.

Akitoa ujumbe wa Rais JOHN MAGUFULI kwa Rais wa Comoro Azali assouman, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amemhakikishia Rais wa Comoro kuwa Tanzania itadumisha uhusiano uliopo kati ya nchi hizo MBILI hasa kwenye sekta za elimu, afya na biashara kwa ajili ya manufaa ya nchi hizo MBILI.

Makamu wa Rais pia amemtakia Rais wa Comoro kheri katika safari yake ya Mecca– Saudi Arabia kwa ajili ya Ibada ya Umrah.

Wakati huo huo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa JAPAN hapa nchini Masaharu Yoshida na kumweleza kuwa serikali itaendelea kuweka na kuboresha mazingira bora kwa ajili ya wawekezaji kutoka mataifa mbalimbali Duniani ikiwemo wawekezaji kutoka nchini JAPAN.

Makamu wa Rais amesema serikali ya JAPAN imekuwa mshirika mkubwa wa maendeleo kwa Tanzania katika kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo Tanzania Bara na Visiwa hasa kwenye sekta ya elimu, afya na maji na kusema jambo hilo ni zuri na lakuigwa na washirika wengine wa maendeleo.

Kwa upande wake Balozi wa Japan hapa nchini MASAHARU YOSHINDA amemhakikishia Makamu wa Rais SAMIA SULUHU HASSAN kuwa nchi yake itaendelea kufadhili ipasavyo miradi ya maendeleo hapa nchini ili kuhakikisha wananchi wa Tanzania wanapata huduma bora za kijamii.
=================================================

BALOZI SEIF AFUNGUA SEMINA YA UTAFUTAJI NA UCHIMBAJI WA MAFUTA NA GESI ASILIA ZANZIBAR


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akifungua Semina juu ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi iliyofanyika katika ukumbi wa juu wa Baraza la Wawakilishi uliopo Mbweni.Kulia ya Balozi Seif ni Waziri wa wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Mh. Salama Aboud Talib na wa Pili kutoka Kulia ni Mwakilishi wa Kampuni ya Utafiti wa Mafuta na Gesi asilia ya Rakgas kutoka Nchini Ras Al – Khaimah Bwana Kamal Ataya.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakifuatilia mada mbali mbali zilizotolewa kwenye Semina juu ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia.

Mtaalamu wa utafiti na uchimbaji mafuta na gesi kutoka Kampuni ya Rakgas ya Nchini Ras Al – Khaimah Bwana Osama Abdel akityoa mada kwenye semina ya mafuta na gesi ilitotolewa kwa wawakilishi wa Zanzibar.
Mrakibu Msaidizi wa Mafunzo { ASP } Juma Makame wa Pili kutoka kulia mwenye shati la drafti akimpatia maelezo Balozi Seif aliyepo kati kati juu ya harakati za kukamilika kwa matengenezo makubwa ya Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi hapo Kikwajuni Mjini Zanzibar.Wa kwanza kutoka Kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Joseph Abdulla Meza, wa kwanza kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Nd. Omar Hassan na nyuma ya ASP Juma Makame ni Msimamizi wa ujenzi kutoka KMKM LCDR Hamad Masoud Khamis.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais w Zanzibar Nd. Joseph Abdulla Meza akimueleza Balozi Seif hatua zinazofanywa za kuimarisha eneo la nje ya Ukumbi huo.Picha na – OMPR – ZNZ.
==============================================

Wafanyabiashara wahimizwa kuchukua mashine za EFD.

Na: Lilian Lundo - MAELEZO - Dodoma

Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeanza kugawa Mashine za Kutunza Hesabu za Kodi za Kielektroniki (EFD) bila malipo kwa wafanyabiashara wa kati na wadogo.

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt Ashatu Kachwamba alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Neema William Mgaya juu ya mpango wa serikali kugawa mashine hizo Nchi nzima.

“Nia ya Serikali ni kusambaza mashine za EFD Nchi nzima lakini tumeanza na Mkoa wa Dar es Salaam ambapo jumla ya mashine 5,703 zinaendelea kugawiwa kwa wafanyabiashara wa kati na wale wadogo ambao mauzo ghafi yao ni kati ya shilingi milioni 14 mpaka milioni 20 kwa mwaka,” alifanunua Mhe. Ashatu.

Aliendelea kwa kusema kuwa, japo mashine hizo zimekuwa zikitolewa bure lakini wafanyabiashara hawafiki katika ofisi za TRA kuzichukua. Hivyo amewataka kundi hilo la wafanyabiashara kufika katika ofisi za TRA wanazolipia kodi katika Mikoa ya Ilala, Kinondoni au Temeke kuchukua mashine hizo, kwani ni wajibu wa kila mfanyabiashara kutumia mashine hizo katika mauzo ya kila siku.

Aidha Mhe. Ashatu amesema kuwa utaratibu wa matumizi ya mashine hizo ulianzishwa kwa lengo la kurahisisha na kuboresha utunzaji wa kumbukumbu za biashara za walipa kodi. Aliongeza kuwa mfumo huo ulianzishwa ili kupata ufumbuzi wa matatizo ya utunzaji kumbukumbu za mauzo na utoaji wa risiti za mauzo zinazoandikwa kwa mkono.

Vile vile mfumo huo umerahisisha usimamizi na ukadiriaji wa kodi kwa kuwa kumbukumbu zote za mauzo na manunuzi huhifadhiwa na kutunzwa kirahisi kwenye mashine za EFD na taarifa za mauzo ya mlipa kodi hutumwa kwenye seva ya TRA kwa njia ya mtandao kupitia mashine hizo. 
===========================================

Waziri Nape Nnauye akutana na Wanachama wa Shirikisho la kazi za Sanaa za Ufundi Tanzania.


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (kushoto) akipokea maelezo kuhusu sanamu iliyochongwa toka kwa Mwandamizi na Msemaji wa Chama cha Wasanii na Wachongaji Tanzania (CHAWASAWATA) Bw. Nyunga Joseph Nyunga wakati alipotembela katika eneo lao lililoko Mwenge, jijini Dar es Salaam, 28 Juni, 2016.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (wa tatu kushoto) akiangalia kazi za sanaa ya uchongaji ndani ya moja ya mabadanda ya Wachongaji hao wakati alipotembela katika eneo lao lililoko Mwenge, jijini Dar es Salaam, 28 Juni, 2016.Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (katikati) akiwa ameongozana na baadhi ya Viongozi wa Chama cha Wasanii na Wachongaji Tanzania (CHAWASAWATA) wakati alipowasili katika eneo lao lililoko Mwenge, jijini Dar es Salaam, 28 Juni, 2016.PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM.


Na Benedict Liwenga-WHUSM.

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye ameahidi kuzitataua baadhi ya changamoto mbalimbali zinazoikabili Chama cha Wasanii na Wachongaji Tanzania (CHAWASAWATA) ikiwemo upatikanaji wa Hati Miliki ya Kiwanja kwa ajili ya kazi zao, Ushuru unaotozwa kupitia Idara ya Maliasili nchini pamoja na Sheria ya Tozo katika Viwanja vya Ndege.

Mhe, Nnuaye ametoa ahadi hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati alipokutana na Wanachama wa Shirikisho hilo ambapo amesema kuwa, suala la upatikanaji wa Hati Miliki ya eneo kwa ajili ya kazi za Wachongaji hao alishaanza kuifanyia kazi kwa kufanya mawasiliano na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi na amewahakikishia kwamba Hati ya eneo hilo itapatikana ili Wachongaji hao waweze kuwa na eneo lao maalum la kazi zao.

‘’Suala la upatikanaji wa Hati Miliki katika eneo lenu ambalo limekuwa likileta minong’ono niachieni mimi kwani najua katika hili kuna baadhi ya watu wenye fedha wanataka kuwakandamiza watu wasio na uwezo kwa kudai kuwa eneo ni la kwao, hapo awali nilishafanya mazungumzo na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na nawahahakikishieni kuwa haki itatendeka, kwani hakuna mtu mwenye mfuko mkubwa wa kuweza kuiingiza Serikali nzima katika suala hili’’, alisema, Mhe. Nnauye.

Kuhusu suala la Ushuru unaotozwa na Maliasili nchini, Mhe. Nnauye amesema kuwa yuko tayari kukaa na watu wa Maliasili na kuona namna gani ushuru huo unavyotozwa hususani kwa Wachonagji hao pasipo kuonewa mtu ambapo pia ameshauri kuwa baadhi ya kodi ambazo zinazoweza kuua biashara za watu wenye vipato vya chini ni vema zikaondolewa ili zisiendelee kuwaumiza.

Aidha, Mhe, Nnauye ameahidi kutembelea maeneo ya Viwanja vya ndege ili kuweza kujua baadhi ya bidhaa za kazi za Uchongaji ambazo zimekuwa zikikamatwa na Watendaji viwanjani hapo zimekuwa zikiishia wapi ili kuondoa malalamiko yanayoelekezwa katika viwanja hivyo.

SHAMO WORLD FOUNDATION YATOA MSAADA KATIKA KITUO CHA WATOTO YATIMA CHA MAUNGA JIJINI DAR LEO.



WAZIRI MKUU wa Lesotho, Dk. Pakalitha Mosisili amekubali kutekeleza masharti yaliyowekwa na Wakuu wa Nchi na Serikali na Kamati ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Uchumi na Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC Double Troika Summit), na kuridhia timu ya uchunguzi kwenda nchini humo kufanya uchunguzi wa hali ya kiusalama na kisiasa.

Dk. Mosisili ametoa uamuzi huo leo (Jumanne, 28 Juni, 2016) wakati wa kikao maalum cha Wakuu wa Nchi na Serikali (SADC Summit) na wakuu wa nchi wanaounda Kamati ya Siasa, Ulinzi na Usalama (SADC Organ on Politics, Defense and Security Cooperation) kilichofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (GICC), jijini Gaborone, Botswana.

Pia amekubali viongozi waupinzani na baadhi ya maofisa wa kijeshi wanaoishi uhamishoni ambao walikimbia machafuko yaliyotokea nchini humo warejee nchini mwao na kuahidi kwamba atahakikisha wanapatiwa ulinziwa kutosha. 

Januari mwaka huu, mkutano wa SADC Double Troika uliagizakwambaifikapo Februari Mosi, mwaka huuSerikali ya Lesotho iwe imetangaza matokeo ya Tume iliyoundwa kuchunguza matatizo ya kisiasa na kiusalama nchini humo hususan mazingira yaliyopelekea kifo cha marehemu Luteni Jenerali Maaparankoe Mahao ambaye alikuwa Mkuuwa Majeshi.

Kwaupande wake, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye alikuwa akimwakilisha Rais Dk. John Pombe Magufuli katika kikao hicho amesema wamepitia ripoti iliyoundwa na timu ya SADC iliyochunguza kuhusu matatizo ya Lethoto ambayo iliwahoji Viongozi wa Serikali, Jeshi, Bunge na familia ya marehemu Luteni Jenerali Mahao.

“Lengo la hatuahiiza SADC ni kuhakikisha inarejesha hali ya amani na utulivu kwenye maeneo ya siasa, ulinzi na usalama katika nchi wanachama wa Jumuiya hiyo ili wananchi wake waweze kuishi vizuri,” amesema.

Pia Waziri Mkuu amesema Tanzania inatarajiwa kukabidhiwa uenyekiti wa Wakuu wa Nchina Serikali na Kamati ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Uchumi na Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC Double Troika Summit), Agosti mwaka huu ambapo kitafanyika kikao kingine nchini Tanzania.

Mkutano huo wa ulifunguliwa na Rais wa Botswana, Mhe. Lt. Jen. Seretse Khama Ian Khama na ulihudhuriwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye alikuwa akimwakilisha Rais Dk. John Pombe Magufuli; Rais wa Afrika Kusini, Bw. Jacob Zuma; Rais wa Msumbiji, Bw. Filipe Jacinto Nyusi; Rais wa Zimbabwe, Bw. Robert Mugabe, Mfalme Muswati wa III wa Swazland.

SADC Double Troika ni kikao maalum kinachojumuisha Wakuu wa Nchi na Serikali (SADC Summit) na wakuu wa nchi wanaounda Kamati ya Siasa, Ulinzi na Usalama (SADC Organ on Politics, Defense and Security Cooperation).

SADC Double Troika ni mkutano unaohusisha viongozi wakuu watatu wanaoongoza chombo cha ushirikiano wa siasa, ulinzi na usalama na wengine watatu kutoka kwenye Mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa SADC. Hawa wanawakilisha mwenyekiti aliyepo madarakani, mwenyekiti aliyemaliza muda wake na mwenyekiti ajaye ambaye huwa ni makamu mwenyekiti.

Chini ya muundo wa SADC, kuna mambo makuu mawili; la kwanza likiwa ni utangamano wa kikanda ambao unasimamiwa na mkutano wa wakuu wa nchi (SADC Summit) na la pili ni la siasa, ulinzi na usalama ambalo linasimamiwa na chombo maalum (SADC Organ).

Wajumbe wa mkutano wa SADC Organ ni Msumbiji (Mwenyekiti); Afrika Kusini (Mwenyekiti aliyemaliza muda wake) na Tanzania inayotarajia kuchukua uenyekiti wa chombo hiki ifikapo Agosti, 2016. Botswana, Zimbabwe na Swaziland ndizo zinaunda SADC Summit.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, JUNI 28, 2016.
==============================================

WATEJA WA SIMBA CEMENT KUNUNUA KUNUNUA SARUJI KWA M PESA


KIWANDA Cha Saruji cha Simba Cement (TCCL) cha Tanga, kimeinmgia makubaliano na Kampuni ya simu ya mkononi ya Vodacom Tanzania Limited, kwa mteja kununua saruji kwa kutumia M PESA bila tozo yoyote.

Makubaliano hayo yaliyofanyika leo viwanja vya Hotel ya Tanga Beach na kushuhudiwa na viongozi wa pande zote mbili na kutajwa kuwa yatakuwa mkombozi kwa mwananchi wa kipato cha chini kwa kununua Saruji kwa simu badala ya kutumia Taasisi za pesa na kupanga foleni.

Akizungumza na waandishi wa habari, Afisa Mkuu Biashara wa Vodacom Tanzania, Gregory Verbond, alisema kampuni yake imechukua uamuzi huo wa makubaliano na kampuni ya Cement kwa lengo la kumsaidia mwananchi wa kipato cha chini.

Alisema mteja ataweza kununua Saruji (Simba Cement) kwa kutumia M PESA na hakutakuwa na tofati ya mnunuzi wa mifuko mingi na michache ambapo hatotozwa ada yoyote mnunuaji.Kwa upande wake, Mkurugenzi wa kiwanda cha Saruji, Simba Cement, Renhardt Swart, alisema makubaliano hayo ni moja ya sera za kiwanda kumsaidia mwananchi wa chini kuweza kukabiliana na changamoto za maisha.

Alisema Kiwanda cha Simba Cement daima kiko kwa ajili ya wananchi na faida inayopata inairejesha kwa wananchi na kuwataka kuitumia fursa hiyo ambayo iko na unafuu kwa ununuaji.

TAARIFA KWA UMMA:UTEUZI WA BODI YA WADHAMINI WA SHIRIKA LA TAIFA LA HIFADHI YA JAMII (NSSF)





 

-
-
-
-
-
-
-
-


=================================================

PROF. MAKAME MBARAWA ATOA MIEZI MITATU KWA BARABARA YA DODOMA-MAYAMAYA KUKAMILIKA


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (Katikati), akifafanua jambo wakati akizungumza na Mkandarasi SINO HYDRO COMPANY LIMITED anayejenga barabara ya Dodoma-Mayamaya KM 43.6.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa kwanza kulia), akitoa maelekezo kwa Mkandarasi SINO HYDRO COMPANY LIMITED anayejenga barabara ya Dodoma-Mayamaya KM 43.6, alipokagua maendeleo ya ujenzi huo

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, ametoa miezi mitatu kwa Kampuni ya SINO HYDRO COMPANY LIMITED inayojenga Barabara ya Dodoma-Mayamaya kwa kiwango cha Lami kuhakikisha barabara hiyo inakamilika.

Akizungumza mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo yeye urefu wa kilomita 43.6 Prof. Mbarawa amemtaka mkandarasi kuikabidhi barabara kwa Serikali ifikapo mwezi Oktoba mwaka huu.

“Hakikisheni barabara hii ambayo ni sehemu ya barabara kuu ya Great North Road inakamilika ili kuharakisha mkakati wa Serikali wa kukamilisha barabara hiyo eneo la Tanzania kwa kiwango cha lami, amesema Waziri Prof. Mbarawa.Barabara ya Dodoma-Mayamaya ni sehemu ya Barabara ya Dodoma-Kondoa-Babati yenye urefu wa Kilomita 247.8 ambayo ujenzi wake umegawanywa sehemu tatu ambazo ni Dodoma-Mayamaya KM 43.6, Mayamaya-Mela-Bonga KM 188.15.

‘Kukamilika kwa barabara hii ambayo ni sehemu ya Barabara Kuu ya Great North Road inayoanzia Capetown Afrika Kusini hadi Cairo nchini Misri kutachochea fursa za kibiashara na kiuchumi katika Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na nchi za Kaskazini mwa Afrika’, amesisitiza Prof. Mbarawa

Mpaka sasa takribani shilingi bilioni 43 zimeshalipwa kwa mkadarasi SINO HYDRO COMPANY LIMITED kukamilisha kilimilisha KM 8 zilizobaki katika sehemu ya Dodoma-Mayamaya, barabara ambayo ambayo imejengwa kwa viwango vinavyokubalika.

Barabara ya Great North Road inayopita mikoa ya Iringa, Dodoma na Arusha inaanzia Capetown Afrika Kusini hadi Cairo Misri mbapo kukamilika kwake kutaliunganisha Bara la Afrika kwa Barabara ya Lami.
===============================================

==============================================

Tatizo la mikopo kupatiwa ufumbuzi









===========================================