MASAUNI AKABIDHI MSAADA WA PAMPU NA KUKAGUA MIRADI JIMBONI KIKWAJUNI
Mbunge
wa Jimbo la Kikwajuni, Zanzibar ambae pia ni Naibu Waziri Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kushoto),
akimkabidhi Mkurugenzi wa Operesheni za Kiufundi wa Mamlaka ya Maji
Zanzibar, Maulidi Hassan Khamisi(kulia), bomba za pampu ya maji
itakayotumika kuunganisha mtandao wa maji .Mradi huo una umbali wa
kilomita 3.5. ukiwa na lengo la kutatua kero ya maji jimboni hapo.
Mbunge
wa Jimbo la Kikwajuni, Zanzibar ambae pia ni Naibu Waziri Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wanne kulia), akiangalia
mafundi wakiweka tuta barabarani wakati alipotembelea mradi wa ujenzi
wa barabara katika jimbo hilo ikiwa na lengo la kutimiza ahadi za ujenzi
wa barabara kwa wananchi wa jimbo hilo.
Mhandisi
wa Mradi wa Uwekaji wa Taa za Barabarani katika Jimbo la Kikwajuni,
Zanzibar, Ephantus Mathi (kushoto)kutoka Kampuni ya Central Electrical,
akitoa maelezo juu ya mradi huo kwa Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambae
pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad
Masauni (wapili kulia). Wa kwanza kulia ni Mwakilishi wa Jimbo hilo,
Nassor Salum Jazeera.
Mbunge
wa Jimbo la Kikwajuni, Zanzibar ambae pia ni Naibu Waziri Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na wataalamu
wa Mradi wa Uwekaji Taa za Barabarani katika Jimbo la Kikwajuni.
Mafundi kutoka Kampuni ya Central Electrical wakiendelea na uwekaji wa
nyaya za umeme katika moja ya nguzo ya taa katika mitaa ya Jimbo la
Kikwajuni ikiwa ni ukamilishaji wa ahadi za Mbunge wa Jimbo hilo,
Mhandisi Hamad Masauni.
No comments:
Post a Comment