Baadhi
ya wafanyakazi wa TASAF wakiwa katika Mkutano wa kilele cha Maadhimisho
ya wiki ya Utumishi wa Umma uliojadili namna ya kuboresha utoaji wa
huduma kwa wananchi.
Baadhi
ya wafanyakazi wa TASAF wakifuatilia kwa umakini hotuba ya Mkurugenzi
Mtendaji wa Mfuko huo Bwana Ladislaus Mwamanga, ( hayupo pichani)
kujadili uboreshaji wa huduma za mfuko huo katika utoaji wa huduma kwa
wananchi.
Mkurugenzi
Mtendaji wa TASAF,Bwana Ladislaus Mwamanga ( aliyeshika kipaza sauti)
akitoa ufafanuzi juu ya moja ya masuala yaliyoulizwa na wafanyakazi
(hawapo pichani) katika kikao cha kufunga wiki ya utumishi wa umma
yaliyofanyika katika ofisi za makao makuu ya taasisi hiyo jijini Dar esa
salaam.
Mfuko huo wa Maendeleo ya Jamii unaotekeleza Mpango wa Kunusuru
Kaya Maskini , unatoa huduma kwa Zaidi ya Kaya Milioni Moja na Lakini
Moja nchini kote jukumu iliyopewa na serikali katika jitihada zake za
kupambana na Umaskini nchini..
Imearifiwa katika kikao hicho kuwa mafanikio makubwa yameanza
kujitokeza kwa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ambapo wengi
wao wameanza kujiwekea misingi ya kupunguza umaskini kwa kuwa na uwezo
wa kusomesha watoto,kupata huduma za afya,kuwa na uhakika wa lishe na
kuongeza uchumi wao.
Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini pia umeanza kusisimua hamasa ya
walengwa wa Mpango huo kuboresha maisha yao kwa kiwango cha kuanza
kuboresha makazi yao kwa kujinunulia mabati na kuezeka nyumba,kuanzisha
miradi midogo midogo kama ufugaji wa kuku wa kienyeji,mbuzi nahata
nguruwe.
Akizungumza katika kikao hicho Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF bwana
Ladislaus Mwamanga amesisitiza watumishi wa Mfuko huo kuendeleza
jitihada za kuwahudumia wananchi na hususani walengwa wa Mpango kwa
kuzingatia taratibu na kanuni za utumishi wa umma kama zinavyoelekeza.
Zifuatazo ni picha za watumishi wa TASAF wakiwa kwenye ukumbi wa
mikutanowa taasisi hiyo maarufu kama “Mlimani City conference hall”
ulioko makao makuu ya taasisi hiyo jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment