TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Saturday, February 15, 2014
CHADEMA YALE YALE YAMPIGA CHINI MSHINDI WA KURA ZA MAONI, WAWEKA MBEBIZ KWENYE UBUNGE
Wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi
jimbo la Kalenga walivyompongeza Sinkala Mwenda siku ya kura za
maoni baada ya kushinda wenzake 13.
KAMATI kuu ya chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) imemteua aliyekuwa mshindi wa pili wa kura za maoni katika zoezi la kura za maoni Bi Grace Tendega kupeperusha bendela ya Chadema katika uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga.
Habari za uhakika kutoka ndani ya kamati kuu ya Chadema iliyoketi jijini Dar es Salaam leo zinadai kuwa aliyekuwa mshindi wa kura za maoni mwanasheria Sinkala Mwenda hajateuliwa na kamati kuu hiyo mbali ya kuongoza kwa kura kura 132 dhidi ya kura 122 alizopata mpinzani wake wa karibu Grace Tendega
Katibu wa Chadema wilaya ya Iringa vijijini Felix Nyondo ameuthibitishia mtandao huu wa www.matukiodaima.com kuwa amepata taarifa hizo za kuteuliwa Bi Grace Tendega kuwa mgombea wa Chadema jimbo hilo la Kalenga .
Hata hivyo alisema anapongeza maamuzi ya kamati kuu na kuwataka wana Chadema Kalenga kujiandaa kwa kampeni za uchaguzi huo na kuanza kumnadi mgombea wao ili kuweza kushinda uchaguzi huo mdogo.
Kutokana na uteuzi sasa Tendega atavaana Godfrey Mgimwa wa CCM katika uchaguzi huo ili kuziba nafasi iliyoachwa waziri na aliyekuwa mbunge wa jimbo la Kalenga marehemu Dr Wiliam Mgimwa aliyefariki mwanzoni mwa mwaka huu.
Hata hivyo duru za kisiasa kutoka ndani ya Chadema zinadokeza kuwa sababu ya kuachwa kwa mgombea huyo aliyeshinda kura za maoni mwanasheria Mwenda ni kutokuwa na mtaji wa watu kwa maana ya kutokubalika ndani na nje ya chama hicho hivyo Chadema kuona kumsimamisha Mwenda ni kulipoteza jimbo hilo.
Huku kwa upande wa mteule wao Bi Tendega amekuwa na sifa ya kugombea katika jimbo hilo kupitia chama cha Jahazi Asilia na kufanya vema japo si kwa kushinda hivyo nin imani yao kupitia Chadema anaweza kufanikiwa kushinda.
KAMATI kuu ya chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) imemteua aliyekuwa mshindi wa pili wa kura za maoni katika zoezi la kura za maoni Bi Grace Tendega kupeperusha bendela ya Chadema katika uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga.
Habari za uhakika kutoka ndani ya kamati kuu ya Chadema iliyoketi jijini Dar es Salaam leo zinadai kuwa aliyekuwa mshindi wa kura za maoni mwanasheria Sinkala Mwenda hajateuliwa na kamati kuu hiyo mbali ya kuongoza kwa kura kura 132 dhidi ya kura 122 alizopata mpinzani wake wa karibu Grace Tendega
Katibu wa Chadema wilaya ya Iringa vijijini Felix Nyondo ameuthibitishia mtandao huu wa www.matukiodaima.com kuwa amepata taarifa hizo za kuteuliwa Bi Grace Tendega kuwa mgombea wa Chadema jimbo hilo la Kalenga .
Hata hivyo alisema anapongeza maamuzi ya kamati kuu na kuwataka wana Chadema Kalenga kujiandaa kwa kampeni za uchaguzi huo na kuanza kumnadi mgombea wao ili kuweza kushinda uchaguzi huo mdogo.
Kutokana na uteuzi sasa Tendega atavaana Godfrey Mgimwa wa CCM katika uchaguzi huo ili kuziba nafasi iliyoachwa waziri na aliyekuwa mbunge wa jimbo la Kalenga marehemu Dr Wiliam Mgimwa aliyefariki mwanzoni mwa mwaka huu.
Hata hivyo duru za kisiasa kutoka ndani ya Chadema zinadokeza kuwa sababu ya kuachwa kwa mgombea huyo aliyeshinda kura za maoni mwanasheria Mwenda ni kutokuwa na mtaji wa watu kwa maana ya kutokubalika ndani na nje ya chama hicho hivyo Chadema kuona kumsimamisha Mwenda ni kulipoteza jimbo hilo.
Huku kwa upande wa mteule wao Bi Tendega amekuwa na sifa ya kugombea katika jimbo hilo kupitia chama cha Jahazi Asilia na kufanya vema japo si kwa kushinda hivyo nin imani yao kupitia Chadema anaweza kufanikiwa kushinda.
Chadema kimeshindwa kwa mengi uchaguzi madiwani
Wapo wanaosema uchaguzi mdogo uliofanyika
Februari 8 mwaka huu katika kata 27 zilizopo ndani ya mikoa 15 nchini
umepeleka chereko CCM na majonzi Chadema.
Ni kicheko kwa CCM kwa sababu kimeshinda katika
kata 24, huku Chadema kikiambulia ushindi katika kata tatu na
NCCR-Mageuzi kata moja.
Wengi walidhani kuwa Chadema kingeweza kufanya
vyema, kutokana na kwamba uchaguzi ulifanyika ikiwa zimepita siku kadhaa
tangu chama hicho kikuu cha upinzani nchini kufanya Operesheni Pamoja
Daima na Vuguvugu la Mabadiliko (M4C), katika mikoa mbalimbali nchini.
Wapo waliogusia helikopta tatu zilizotumiwa na
chama hicho katika operesheni hizo, hasa ile ya Pamoja Daima, pamoja na
mpasuko uliokikumba baada ya kumvua nyadhifa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu
wake, Zitto Kabwe.
Mbali na Kabwe, pia kiliwafukuza uanachama
aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Dk Kitila Mkumbo na
aliyekuwa Mwenyekiti wake mkoani Arusha, Samson Mwigamba.
Binafsi naamini kuwa zipo sababu nyingi
zilizosababisha Chadema kishindwe kufanya vyema katika uchaguzi huu,
ikilinganishwa na uchaguzi mdogo wa madiwani wa Julai mwaka jana ambapo
kilishinda katika kata zote nne za Elerai, Kaloleni, Kimandolu na Themi
mkoani Arusha.
Kata hizo zilikuwa wazi tangu mwaka 2011 baada ya
chama hicho kuwatimua wanachama wake waliokuwa madiwani Estomih
Mallah(Kimandolu), John Bayo (Elerai), Reuben Ngowi (Themi) na Charles
Mpanda (Kaloleni).
Katika uchaguzi wa Februari 8, Chadema kimepoteza
Kata ya Nyasura iliyopo mkoani Bunda na Kata ya Mkongolo iliyopo jimbo
la Kigoma Kaskazini mkoani Kigoma ambazo wameshinda CCM.
Lakini kimeibuka na ushindi katika kata mbili za
Sombetini na Njombe Mjini ambazo awali zilikuwa za CCM. Pia kiliibuka na
ushindi katika Kata ya Kiborloni ambayo hata kabla ya uchaguzi huo,
diwani wa kata hiyo alikuwa wa Chadema.
NCCR-Mageuzi chenyewe kiliweza kutetea Kata ya
Kilelema mkoani Kigoma huku CCM kikipoteza Kata ya Njombe Mjini ambayo
ilikwenda kwa Chadema.
Chadema kimeangushwa na daftari la kudumu la wapiga kura.
Tangu Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) haijawahi kulifanyia maboresho daftari hilo jambo ambalo
naamini limeathiri uchaguzi huo na watu wengi wamepoteza haki yao ya
kikatiba ya kupiga kura. Katika kipindi hicho chote NEC imeendelea
kujificha kwenye kichaka cha Sheria iliyoianzisha (Sura ya 343). Sheria
hiyo inaeleza kwamba uboreshaji wa daftari hilo utafanyika mara mbili
kwa miaka mitano, yaani baada ya Uchaguzi Mkuu kupita na kabla ya
uchaguzi unaofuata.
EPL News: Winga wa zamani wa Preston na England Sir Tom Finney amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 91
Winga wa zamani wa Preston na timu ya taifa ya England Sir Tom Finney amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 91.
Finney
ambaye ameichezea Preston North End zaidi ya michezo 400 ya ligi kati
ya 1946 na 1960 na kuichezea michezo 76 timu ya taifa ya England,
aliifungia timu ya taifa ya England
magoli 30 na kuingia kwenye orodha ya wafungaji wa muda wote wa timu
yaifa ya England akishikilia nafasi ya sita ambapo anafungana na Alan
Shearer na Nat Lofthouse.
WASSIRA,MAKAMBA, NAO WAHOJIWA NA KAMATI NDOGO YA MAADILI CCM
Naibu Waziri wa Mawasiliano
Sayansi na Teknolojia, January Makamba akizungumza na waandishi wa
habari nje ya ukumbi wa White House mjini Dodoma mara baada ya kuhojiwa
na Kamati ya Maadili CCM jana.
January Makamba akiondoka kwenye Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi mara baada ya kuhojiwa na Kamati ya Maadili.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
(Mahusiano na Uratibu), Stephen Wassira akitoka nje ya ukumbi wa White
House baada ya kumaliza mahojiano na Kamati Ndogo ya Maadili CCM mjini
Dodoma jana.
Stephen Wassira akizungumza na
waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kuhojiwa na Kamati Ndogo ya
Maadili ya Chama Cha Mapinduzi. Wassira aliwaeleza waandishi kuwa
hakukuwa na tuhuma juu yake.
Wassira akifurahia jambo na
Kada maarufu wa CCM, Adam Soud mara baada ya kumaliza mazungumzo na
waandishi wa habari mjini Dodoma.
AJIRA HIZI HAPA: WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI IDARA YA UHAMIAJI
Kamishna Mkuu wa idara ya Uhamiaji anatangaza nafasi za kazi katika Idara ya Uhamiaji kwenye
vyeo vya Koplo na Konstebo wa uhamiaji.
A: MKAGUZI MSAIDIZI WA UHAMIAJI NAFASI 70
1. SIFAZINAZOHITAJIKA
Awe na shahada ya kwanza au Stashahada ya juu kutooka vyuo vikuu
vinavyotambuliwa na serikali katika fani zifuatazo; Sheria, Uchumi,
Biashara, Utawala, Uandishi wa habari, Ualimu, Usafirishaji, Rasilimali
watu, Sayansi ya kompyuta, Teknolojia ya mawasiliano, Takwimu, Uchapaji,
Uhandisi majengo na Uhandisi Mitambo.
Awe na umri usiozidi miaka 35
2. MAJUKUMU NA KAZI ZA KUFANYA
(i) Kusimamia doria sehemu za mipakani, Bandarini, Vituo vya Mabasi,
Treni na sehemu zenye vipenyo vya kuingia na kutoka nchini vikiwemo vya
majini.
(ii) Kusimamia shughuli za upelelezi, kuandaa hati ya mashitaka na kuendesha mashitaka.
(iii) Kutoa na kupokea fomu mbali mbali za maombi ya hati za uhamiaji
(iv) kufanya ukaguzi wa mwanzo wa maombi mbalimbali
(v) kupokea na kukagua hati za safari, fomu ya kuingia na kutoka nchini.
(vi) kuidhinisha malipo mbalimbali ya huduma za uhamiaji kwa wanaostahili
(vii) kuagiza ufunguaji wa majalada ya watumiaji
(viii) kutunza kumbukumbu za ruhusa kwa wanaongia na kutoka nchini
(ix) kukusanya, kusimamia na kutunza takwimu za uhamiaji na uraia
(x) Kuandaa majibu ya maombi yote ya huduma za uhamiaji yaliyokubaliwa au kukataliwa
B. KOPLO WA UHAMIAJI (NAFASI 100)
1. SIFA ZINAZOHITAJIKA
(i) Awe amehitimu Kidato cha Sita na kufaulu
(ii) Awe na umri usiozidi miaka 30
C. KONSTEBO WA UHAMIAJI (NAFASI 100)
1. SIFA ZINAZOHITAJIKA
(i) Awe amehitimu kidato cha nne na kufaulu
(ii) Awe na umri usiozidi miaka 25
D. SIFA ZA ZIADA: KOPLO/KONSTEBO WA UHAMIAJI
(i) Cheti cha ufundi stadi (Full Technical Certificate) kwenye fani ya umeme na mitambo.
(iii) Cheti au Stashahada ya Uhazili (Certificate or Diploma in Secretarial Studies)
katika chuo kinachotambulika na Serikalì.
(iv) Cheti au Stashahada ya Takwimu (Certificate or Diploma in Statistics) kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.
(v) Cheti au Stashahadayavyombo vya Majini (Certificate or Diploma in Marine Transportation
and Operation) kutoka katika Chuo kinachotambulika na Serikali.
(vi) Cheti au Stashada katika fani ya uchapaji (Printing)
(vii) Ujuzi na elimu ya kompyuta na uandishi mzuri utazingatiwa.
E. MAJUKUMU NA KAZI ZA KUFANYA
(i) Kufungua, kupanga na kutunza majalada yenye orodha ya majina ya watumiaji wa huduma
za Uhamiaji.
(ii) Kuandika Hati mbalÃmbaLi za Ubamiaji
(iii) Kufanya Doria schcme za Mipakani, Bandarini, Vituo vya Mabasi, treni na sehemu zenye
vipenyo vya kuingia na kutoka nchini vikiwcmo vya majini.
(iv) Kusindikiza watuhumiwa wa kesi za Uhamiaji Mahakamani pamoja na wageni
wanaofukuzwa nchini (Deporters).
Kufanya ukaguzi kwcnye mahoteli, nyumba za kulaLa wageni na sehemu za biashara.
(vi) Kuchapa au kuandika kwa kompyuta barua au nyaraka mbalimbali zinazohusu kazi za kila
siku za Uhamiaji.
(vii)Kufanya matengenezo/ukarabati wa mitambo na vitendea kazi vya Uhamiaji.
F: MAOMBI YOTE YAWE NA VIAMBATANISHO VIFUATAVYO.
(i) Vivuli vya vyeti vya kumalizia masonia kwa mujibu wa sifa zilizotajwa.
(ii) Nakala ya Cheti cha Kumaliza Elimu ya Msingi
(iii) Nakala ya cheti cha kuzaliwa
(iv) Picha mbili (passport size)
(v) Barua ya utambulisho kutoka kwa Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa.
Maombi yote yapite posta na barua za maombi ziandikwe kwa mkono.
(i) Maombi ya nafasi ya mkaguzi msaidizi wa uhamiaji yatumwe kwa;
KATIBU MKUU,
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI,
S.L.P 9223,
DAR ES SALAAM
(ii) Maombi ya nafasi ya Koplo wa uhamiaji na konstebo wa uhamiaji yatumwe kwa;
KAMISHNA MKUU WA UHAMIAJI,
S.L.P 512,
DAR ES SALAAM
Wednesday, February 12, 2014
KONGAMANO LA TAFAKURI MARIDHIANO KUELEKEA KATIBA MPYA, JIJINI DAR ES SALAAM MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AFUNGUA RASMI LEO
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisoma hotuba yake wakati akifungua rasmi Kongamano la Tafakuri na
Maridhiano kuelekea Katiba mpya, lililofanyika kwenye Hoteli ya White
Sands jijini Dar es Salaam, leo Feb 12, 2014 na kushirikisha Vyama vya
Siasa, Makundi ya dini na Asasi za kiraia.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, baada ya
kufunguliwa rasmi rasmi Kongamano la Tafakuri na Maridhiano kuelekea
Katiba mpya, lililofanyika kwenye Hoteli ya White Sands jijini Dar es
Salaam, leo Feb 12, 2014 na kushirikisha Vyama vya Siasa, Makundi ya
dini na Asasi za kiraia
Picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano hilo.
Baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo.
Baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo wakijadiliana jambo
Meza Kuuu.
Picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano hilo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Bilal na Waziri Mkuu,
Mizengo Pinda, wakiagana na wajumbe walioshiriki Kongamano hilo baada ya
ufunguzi uliofanyika kwenye Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam
leo Feb 12, 2014 na kushirikisha Vyama vya Siasa, Makundi ya dini na
Asasi za kiraia.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, baada ya
kufunguliwa rasmi rasmi Kongamano la Tafakuri na Maridhiano kuelekea
Katiba mpya, lililofanyika kwenye Hoteli ya White Sands jijini Dar es
Salaam, leo Feb 12, 2014 na kushirikisha Vyama vya Siasa, Makundi ya
dini na Asasi za kiraia. Picha na OMR
TAMASHA LA KUWAWEZESHA WANAWAKE NA VIJANA MAANDALIZI YANAENDELEA
WADAU WAOMBWA KUJITOKEZA KUDHAMINI
Pichani wa tatu kulia ni Mkurugenzi wa Habari na Matukio wa Kampuni ya Angels Moment ya
jiji Dar,akizungumza mbele ya Wanahabari (hawapo pichani) mapema leo
kwenye moja ya ukumbi wa mikutano ya Serena Hotel,kuhusiana tamasha la
kwanza na
la aina yake kufanyika nchini Tanzania, lenye lengo la kuongeza na
kuchochea uelewa wa wanawake katika kuchangamkia fursa mbalimbali za
kujiwekea akiba.
“Tamasha
hili limeandaliwa ili kuwaonesha wanawake na vijana umuhimu wa kuweka
akiba, aina tofauti za kuweka akiba na njia mbalimbali za kuweka akiba
pamoja na fursa za kuweka akiba kimkakati kupitia uwasilishaji wa mada
na maonesho,” alisema Bi Pamela. Pichani kulia ni Meneja Mawasiliano wa kampuni ya Angels Moment,Bi.Beatrice Millinga,Mratibu
wa Matangazo na Mahusiano kutoka kampuni ya
AZAM/Bakharessa,Bwa.Mohameda Ramadhani (Mdhamini wa tamasha hilo),pamoja
na mwisho kushoto ni Mratibu wa tamasha hilo kutoka kampuni ya MONTAGE
LTD,Bi,Teddy Mapunda.
Pichani ni baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Angels Moment ya jiji Dar wakiwa katika picha ya pamoja,mara baada ya mkutano kumalizika.
==========================================================
WADAU WAOMBWA KUJITOKEZA KUDHAMINI TAMASHA LA KWANZA LA KIPEKEE LA KUWAWEZESHA WANAWAKE NA VIJANA KUFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM
Na Beatrice Millinga
Kampuni
ya Angels Moment ya jijini Dar es Salaam imetoa wito kwa wadau
wanaojihusisha na shughuli mbalimbali za kimaendeleo kujitokeza na
kudhamini tamasha la kwanza la kipekee kwa ajili ya wanawake na vijana
lililopewa jina la Mwanamke na Akiba na linalotarajiwa kufanyika kuanzia
Februari 19 - 21, 2014 kwenye Ukumbi wa Dar Live - Mbagala, jijini Dar
es Salaam.
Akizungumza
na waandishi wa wahabari katika ukumbi wa Serena leo, Mkurugenzi wa
Habari na Matukio wa Kampuni ya hiyo, Bibi Pamela David amesema kuwa
makampuni na mashirika mbalimbali yatapata fursa ya kujitangaza, na
kutangaza bidhaa na huduma zao, kwa lengo la kuongeza ufahamu wa bidhaa
zao kwa wanawake na vijana wa Kitanzania.
“Kwa
kudhamini Tamasha hili wadau watapata sio tu fursa ya kutangaza
biashara na huduma zao bali kujitangaza wao wenyewe na kutoa elimu kwa
umma maana si wananchi wote wanauelewa wa huduma zitolewazo na mashirika
na makampuni mbalimbali hapa nchini,” alisema Bi Pamela.
Kwa
mujibu wa Bi Pamela, Tamasha hilo ni la kwanza na la aina yake
kufanyika nchini Tanzania lenye lengo la kuongeza na kuchochea uelewa wa
wanawake katika kuchangamkia fursa mbalimbali za kujiwekea akiba.
“Tamasha
hili limeandaliwa ili kuwaonesha wanawake na vijana umuhimu wa kuweka
akiba, aina tofauti za kuweka akiba na njia mbalimbali za kuweka akiba
pamoja na fursa za kuweka akiba kimkakati kupitia uwasilishaji wa mada
na maonesho,” alisema Bi Pamela.
Aliongeza
kuwa washiriki watapata fursa ya kupata elimu juu ya kukabiliana na
hatari katika uhifadhi wa fedha na masuala mbalimbali yahusikanayo na
usimamizi wa fedha.
Akizungumza
mfumo utakaotumika kuendesha tamasha hilo, msemaji wa kampuni, Bi
Pamela alisema “Tamasha litakuwa kwenye mfumo wa maonesho pamoja na
vipindi vinne vya uwasilishaji wa mada mbalimbali toka kwa wanawake
wafanyabiashara waliofanikiwa na wataalamu waliobobea kwenye nyanja
hizo.
Kwa
mujibu wa msemaji huyo watoa mada wanaotarajiwa kuwasilisha ni pamoja
na Naibu Gavana Mkuu wa Benki Kuu ya Tanzania, Dkt. Natu Mwamba na
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko Ya
Hifadhi ya Jamii (SSRA) Bibi Irene Isaka.
Tamasha
linatarajia kuwavutia washiriki 5,000 na waonyesha bidhaa 50 kutoka
maeneo mbalimbali katika sekta ya usimamizi wa fedha. Pia, inatarajiwa
kuvutia washiriki toka sekta nyingine ikiwemo biashara zenye mahusiano
na suala zima la uhifadhi wa fedha na uwekaji wa akiba kwa wanawake.
Mgeni rasmi wa Tamasha hili anategemewa kuwa Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal.
Mualiko
wa Mama Asha kwenye Tamasha hili unachagizwa na ujasiri na mchango
wake, pamoja na kujitoa kwake kwa hali na mali katika kusaidia wanawake,
vijana na makundi mbali mbali yenye uhitaji nchini Tanzania.
Tamasha
limedhaminiwa na Said Salim Bakhresa (SSB), Shirika la Hifadhi ya Jamii
(NSSF), Benki ya CRDB, STANBIC, FINCA, Mamlaka ya Usimamizi na
Udhibiti wa Mifuko Ya Hifadhi ya Jamii (SSRA). Wadhamini wengine ni
pamoja na Mfuko wa UTT, Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Mfuko wa
Pensheni kwa Mashirika ya Umma (PPF) na Kampuni ya Ashton Media.
Mvua yazidi kukwamisha vyombo vya Usafiri Masasi kuelekea Mtwara
Magari yakipishana kwa shida katika eneo hilo la Kijiji cha Mkalapa,Mkoani Mtwara kutokana na kuharibika kwa barabara hiyo.
Wakazi
wa kijiji hicho pamoja na Abiria wanaosafiri kwenda
Newala,Masasi,Nachingwea,Nanyumbu na Tunduru wakiwa wamesimama bila
kujua cha kufanya wakati magari yakiwa yamekwama.
*******
*******
Na:Abdulaziz Video,Masasi.
Barabara
ya Ndanda kwenda Masasi eneo la Kijiji cha Mkalapa,limekuwa ni majanga
matupu kama inavyoonekana katika picha hapo chini,kwani barabara hiyo
imeharibika vibara kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha matika maeneo
mbali mbali hapa nchini.
Abiria
wanaofanya safari katika maeneo hayo,inapaswa wajiandae kwa kupoteza
masaa kadhaa katika eneo hilo,kwani mambo hayajakaa sawa.
Hivyo
wakala wa Barabara Mkoa wa Mtwara (TANROADS),wanapaswa kulishughulikia
swala hili haraka iwezekanavyo ili kuwaepusha watumiaji wa barabara hiyo
kuondokana na hadha hii inayowaathiri wasafiri waendao
Newala,Masasi,Nachingwea,Nanyumbu na
Tunduru
mkuu wa mkoa wa Njombe akunwa na ufanisi wa shule ya makete girls
Mkuu
wa mkoa wa Njombe kapteni Mstaafu Aseri Msangi(katikati) akikagua
majengo ya shule mpya wa wasichana wilayani Makete, kushoto ni mkuu wa
wilaya ya Makete Josephine Matiro na kulia ni mwenyekiti wa halmashauri
ya wilaya ya Makete Daniel Okoka.
Ukaguzi huo ukiendelea.
Wananchi wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Njombe Kapteni Msangi(hayupo pichani) akizungumza nao
Mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro akizungumza kwenye mkutano shuleni hapo
Mkuu wa mkoa wa Njombe Kapteni Mstaafu Aseri Msangi akizungumza na wananchi shuleni hapo.
============================================================
Habari/picha na Edwin Moshi, Makete.
Kufuatia
kukamilika kwa kiasi kikubwa majengo ya shule mpya ya sekondari ya
wasichana Makete iliyojengwa katika kijiji cha Utweve kata ya Ukwama
wilayani Makete, mkuu wa mkoa wa Njombe Kapteni mstaafu Asseri Msangi
ameagiza shule hiyo iandikishwe ili ianze kutumika.
Mkuu
wa mkoa ametoa agizo hilo hii leo Februari 11, 2014 wakati wa ziara ya
kukagua miradi mbalimbali ya elimu wilayani Makete, ambapo baada ya
kufika shuleni hapo ameridhishwa na ujenzi wa shule hiyo na kuona haina
sababu ya shule hiyo kuendelea kukaa bila kuandikishwa ili ianze kupokea
wanafunzi.
Akizungumza
na wananchi wa vijiji viwili vinavyojenga shule hiyo ambavyo ni Utweve
na Masisiwe, mkuu huyo wa mkoa mbali ya kupokea na kutjibu kero za
wananchi, amekasirishwa na tabia ya wazazi wa vijiji hivyo kuwaambia
watoto wao wafeli kwa makusudi ili wasiendelee na masomo ya sekondari.
"Ndugu
zangu dunia tuliyopo sasahivi, si ile tuliyoishi zamani, mtoto
asiposoma ni matatizo kwake, na ninyi wazazi wenye tabia ya kuwaambia
watoto wenu wafeli kwa makusudi mnatupelekea taifa letu kaburini na sisi
hatutakubali, tunaomba muiache hiyo tabia, somesheni watoto wenu"
alisema Msangi.
Katika
hatua nyingine Kapteni Msangi amechangia kiasi cha shilingi milioni 1
kwa ajili ya shule hiyo maalum kwa ajili ya wasichana kama njia mojawapo
ya kusaidia ujenzi wa shule hiyo ambayo inatarajiwa kuanza hivi
karibuni.
Shule
hiyo pekee ya wasichana wilayani Makete inajengwa na serikali kwa
kushirikiana na wazawa wa Makete wanaoishi nje ya wilaya hiyo, wananchi
pamoja na wadau mbalimbali.
MWALIMU AJITOKEZA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KALENGA KUPITIA CHADEMA
Katibu
wa Chadema Wilaya ya Iringa Vijijini, Felix Nyondo (kulia) akipokea
fomu kutoka kwa Mwalimu Vitus Lawa (kushoto). Fomu hizo ni kwa ajili ya
kuwania kinyang'anyiro cha kuwa mgombea wa Chadema Jimbo la Kalenga,
Iringa. Baadhi
ya wadau waliomsindikiza Mwalimu Vitus Lawa kurejesha fomu za
kuchaguliwa kuwania Ubunge wa Jimbo la Kalenga katika ofisi za chama
hicho zilizoko kata ya Gangilonga, Iringa. Mwalimu
Vitus Lawa akizungumza na waandishi (hawapo pichani) baada ya kurudisha
fomu za kuwania kuchaguliwa Ubunge wa Jimbo la Kalenga katika ofisi za
chama hicho zilizoko Kata ya Gangilonga, Iringa.
Subscribe to:
Posts (Atom)