Mwenyekiti
wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Kamati kuu ya
CCM ikulu jijini Dar es Salaam leo(picha na Freddy Maro)
EXCLUSIVE INTERVIEW: BRAZIL TO HOST WORLD CUP AGAIN AFTER 64 YEARS!
MOblog
Tanzania’s Chief Editor, Damas Makangale in an exclusive interview with
the Brazilian Ambassador to Tanzania, Hon Francisco Carlos Soares Luz
at his office.
By Damas Makangale, MOblog Tanzania
MOblog: What was your initial reaction when you heard that Brazil will host the 2014 World Cup?
Ambassador
Luz: I think like every Brazilian who is crazy about football, I was
very excited with the news. At a time we knew that there was no
competition since Columbia had retired its candidate so Brazil was
standing alone. We knew [the World Cup] was supposed to happen in South
America, so we are very happy and excited with the opportunity of
hosting the world cup again after 64 years.
MOblog:
Brazilians are going to the world cup with a squad of younger and very
promising players compared to Spain, Germany and Argentina. To what
extent do you think it will help the team to win the trophy?
Ambassador
Luz: I think Scolari has done the right thing. He has mixed the team
with young, talented players who are ready to present themselves to the
world and become national heroes like Neymar da Silva Santos but he has
included veterans; mature and experienced players.
MOblog: Do you think Brazil will benefit from a home advantage and go on to win their first World Cup since 2002?
Ambassador
Luz: We have won the confederation cups and a home advantage will be a
factor during the world cup finals. We believe that the home ground will
make a difference to us.
NAPE: CCM BADO NI KIPENZI CHA WATANZANIA WENGI
NAPE NNAUYE |
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimewashukuru Watanzania kwa kukiamini na kukipatia ushindi wa kishindo katika uchaguzi mdogo wa udiwani uliofanyika jana katika kata 27 na CCM kushinda kata 23.
Akitoa shukrani hizo, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema leo kwamba siri ya CCM kuimwaga CHADEMA ni uadilifu katika kuwatumikia wananchi na kwamba, kushindwa kwa chama hicho ni ushahidi kwamba hakikubaliki na Watanzania wamewathibitishia kwamba hawajazoea vurugu.
Nape alisema CCM inaahidi kuendelea kuwatumikia Watanzania kwa amani na utulivu kwa kuwa ina uzoefu wa kufanya siasa kistaarabu na ndio siri ya kukubalika kwa wananchi.
Akizungumzia kushindwa kwa CHADEMA alisema wamehukumiwa kutokana na vurugu na kupiga watu kwenye kampeni za uchaguzi na ndio maana wametumia gharama kubwa na helkopta tatu na kuambulia kata tatu.
“CHADEMA wamevuna walichopanda Watanzania hawapenda vurugu, wamezoea amani na utulivu sasa wamewaadhibu kwa kuwanyima kura na huo ni ushahidi kwamba Watanzania hawakiamini,” alisema.
Katika uchaguzi huo CCM ilishinda katika kata CCM ilishinda katika kata 23 za Kibindu na Magomeni (Pwani), Kiwalala na Namikage (Lindi), Ubwage (Shinyanga), Ibumu na Nduli (Iringa), Kiomoni na Mtae (Tanga), Nyasura(Mara), Malindo, Santillya (Mbeya), Partimbo(Arusha, Mkwiti (Mtwara), Tungi na Ludewa (Morogoro) na Mrijo (Dodoma).
KONGAMANO LA 9 LA CTO KUHUSU MABADILIKO YA MFUMO WA UTANGAZAJI WA ANALOJIA KWENDA DIJITALI (DBSF) KUANZA KESHO ARUSHA
Mkurugenzi wa Utangazaji
kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Habbib Gunze (kushoto)
akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha leo Februari 10, 2014 juu ya
Kongamano la 9 la CTO la mabadiliko ya mfumo wa utangazaji wa analojia kwenda Dijitali (DBSF) ambao
utafanyika kuanzia 11 – 14 Februari, 2014 Naura Springs Hotel, Arusha Tanzania.
Katikati ni Katibu Mtendaji wa CTO, Prof. Tim Unwin, akifuatiwa na Katibu
Mtendaji wa Shirika la Mawasiliano Afrika Mahsriki (EACO) Hodge Semakula.
kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Habbib Gunze (kushoto)
akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha leo Februari 10, 2014 juu ya
Kongamano la 9 la CTO la mabadiliko ya mfumo wa utangazaji wa analojia kwenda Dijitali (DBSF) ambao
utafanyika kuanzia 11 – 14 Februari, 2014 Naura Springs Hotel, Arusha Tanzania.
Katikati ni Katibu Mtendaji wa CTO, Prof. Tim Unwin, akifuatiwa na Katibu
Mtendaji wa Shirika la Mawasiliano Afrika Mahsriki (EACO) Hodge Semakula.
Mkurugenzi wa Utangazaji
kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Habbib Gunze (kushoto)
akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha leo Februari 10, 2014 juu ya kukamilika kwa maandalizi ya Kongamano la 9 la CTO la mabadiliko ya mfumo wa utangazaji wa analojia kwenda Dijitali (DBSF) ambao
utafanyika kuanzia 11 – 14 Februari, 2014 Naura Springs Hotel, Arusha Tanzania.
Kulia ni Katibu Mtendaji wa CTO, Prof. Tim Unwin.
kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Habbib Gunze (kushoto)
akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha leo Februari 10, 2014 juu ya kukamilika kwa maandalizi ya Kongamano la 9 la CTO la mabadiliko ya mfumo wa utangazaji wa analojia kwenda Dijitali (DBSF) ambao
utafanyika kuanzia 11 – 14 Februari, 2014 Naura Springs Hotel, Arusha Tanzania.
Kulia ni Katibu Mtendaji wa CTO, Prof. Tim Unwin.
Mkurugenzi wa Utangazaji
kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Habbib Gunze akifafanua zaidi juu ya Kongamano hilo 9 la CTO la mabadiliko ya mfumo wa utangazaji wa analojia kwenda Dijitali (DBSF)
kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Habbib Gunze akifafanua zaidi juu ya Kongamano hilo 9 la CTO la mabadiliko ya mfumo wa utangazaji wa analojia kwenda Dijitali (DBSF)
Katibu Mtendaji wa Commonwealth Telecommunications Organisation (CTO)
Prof. Tim Unwin, akizungumza na wanahabari wa jijini Arusha juu ya
kukamilika kwa maandalizi ya mkutano huo unaoanza Februari 11-14, 2014 katika hoteli ya Naura Spring Arusha.Kushoto ni Habbib Gunze, Mkurugenzi wa Utangazaji kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Kulia ni Katibu Mtendaji wa Shirika la Mawasiliano Afrika Mashariki (EACO), Hodge Semakula.
Prof. Tim Unwin, akizungumza na wanahabari wa jijini Arusha juu ya
kukamilika kwa maandalizi ya mkutano huo unaoanza Februari 11-14, 2014 katika hoteli ya Naura Spring Arusha.Kushoto ni Habbib Gunze, Mkurugenzi wa Utangazaji kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Kulia ni Katibu Mtendaji wa Shirika la Mawasiliano Afrika Mashariki (EACO), Hodge Semakula.
Katibu
Mtendaji wa Commonwealth Telecommunications Organisation (CTO) Prof.
Tim Unwin, akizungumza na wanahabari wa jijini Arusha juu ya kukamilika
kwa maandalizi ya mkutano huo unaoanza Februari 11-14, 2014 katika
hoteli ya Naura Spring Arusha.
Viongozi TCRA, CTO na EACO wakizungumza na wanahabari
Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo.
Wanahabari na maofisa wa TCRA wakiwa katika mkutano huo.
Katibu
Mtendaji wa Shirika la Mawasiliano Afrika Mashariki (EACO), Hodge
Semakula akielezea zoezi la uhamaji kutoka mfumo wa Analojia kwenda
Dijitali kwa nchi za Afrika Mashariki hasa Tanzania ulivyofanikiwa.
Wanahabari wakifuatilia mkutano huo.
RAIS KIKWETE AIFARIJI FAMILIA YA MAREHEMU MZEE PATRICK QORRO
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombelezo ya msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Karatu Waziri wa Kilimo na Ushirika Serikali ya awamu ya kwanza, Mhe. Patrick Qorro (72) aliyefariki dunia usiku wa kuamkia Jumamosi baada ya kuugua kwa muda mfupi na kulazwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha Mifupa ( MOI) jijini Dar es Salaam.
Marehemu
Qorro ambaye wakati wa Serikali ya awamu ya kwanza aliwahi kushika
nyadhifa mbalimbali, ikiwamo Waziri mdogo wa Kilimo na Ushirika na
baadaye kuwa waziri kamili wakati wa awamu ya pili, alikuwa akisumbuliwa
na tatizo la kuvuja damu kwenye mzunguko wa kichwa kulikosababishwa na
hitilafu ya figo.Kwa
mujibu wa msemaji wa familia, Bw. James Bwana, Marehemu anatarajiwa
kuagwa rasmi leo kabla ya kusafirishwa Jumatano hadi Kijiji cha
Mbulumbulu, wilayani Karatu, mkoani Arusha kwa ajili ya mazishi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mjane wa marehemu Dkt Martha Qorro na wanafamilia wengine nyumbani kwa aliyekuwa Mbunge wa Karatu Waziri wa Kilimo na Ushirika Serikali ya awamu ya kwanza, Mhe. Patrick Qorro (72) aliyefariki dunia usiku wa kuamkia Jumamosi baada ya kuugua kwa muda mfupi na kulazwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha Mifupa ( MOI) jijini Dar es Salaam.
PICHA NA IKULU
KAMISHNA WA SENSA YA WATU NA MAKAZI ASISITIZA MATUMIZI YA TAKWIMU SAHIHI
Kamishna wa Sensa ya Watu na Makazi Bi. Hajjat Amina Mrisho Said (katikati) akizungumza na Wadadisi wa Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi wa mwaka 2014 kwa Kanda ya kasikazini inayojumuisha mikoa ya Tanga, Arusha, Kilimanjaro na Manyara. Kulia kwake ni Opio Mamu Msimamizi wa mafunzo katika kanda hiyo na kushoto kwake ni Juma Shaban Meneja Takwimu, Ofisi ya Taifa ya Takwimu mkoa wa Manyara.
Wadadisi wa Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi wa mwaka 2014 kwa Kanda ya kasikazini inayojumuisha mikoa ya Tanga, Arusha, Kilimanjaro na Manyara wakimsikiliza kwa makini Kamishna wa Sensa ya Watu na Makazi Bi. Hajjat Amina Mrisho Said (hayupo pichani) katika mafunzo ya utafiti huo yanayotarajia kumalizika kesho jijini Tanga.
Kamishna wa Sensa ya Watu na Makazi Bi. Hajjat Amina Mrisho Said (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wadadisi wa Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi wa mwaka 2014 kwa Kanda ya kasikazini inayojumuisha mikoa ya Tanga, Arusha, Kilimanjaro na Manyara. Mafunzo ya utafiti huo yanayotarajia kumalizika kesho jijini Tanga.
(Picha zote na Veronica Kazimoto – Tanga)
………………………………………………………………………………
Na.Veronica Kazimoto na Aron Msigwa – Tanga.
Ofisi
ya Taifa ya Takwimu imewataka wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa
Serikali, siasa na waandishi wa habari kutumia takwimu sahihi
zinazotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu pindi wanapotekeleza majukumu
yao.
Akizungumza
na waaandishi wa habari pamoja na wadadisi wa Madodoso ya utafiti wa
Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi mwaka 2014 kutoka kanda ya kaskazini
leo jijini Tanga Kamishna wa Sensa ya Watu na Makazi kutoka Ofisi ya
Taifa ya Takwimu Bi. Hajjat Amina Mrisho Said amesema kuwa ni jukumu la
kila mtendaji katika eneo lake kuhakikisha kuwa anatumia takwimu
sahihi zinazotolewa na Ofisi hiyo.
Amesema
Ofisi ya Taifa ya Takwimu ndiyo yenye mamlaka na dhamana ya utoaji wa
takwimu za masuala mbalimbali nchini na kuongeza kuwa matumizi ya
takwimu zisizo sahihi yana athari kwa jamii hasa wakati wa kupanga
mipango ya maendeleo kuanzia ngazi ya vijiji mpaka taifa.
Amesema
kuwa takwimu sahihi huwezesha utekelezaji wa mipango ya maendeleo na
kuongeza kuwa zipo changamoto mbalimbali ambazo ufumbuzi wake unaweza
kupatikana kwa kufanya rejea ya takwimu sahihi kutoka Ofisi ya Taifa ya
Takwimu.
“Takwimu
ni muhimu sana katika kupanga namna ya kukabiliana na matatizo na
majanga mbalimbali yanayotokea katika jamii kama mafuriko, njaa, masuala
ya ardhi na elimu ambayo kimsingi yanahitaji matumizi ya takwimu sahihi
ili kujua kiwango halisi cha ukubwa wa tatizo na namna ya kupata
suluhisho la kudumu kwa wananchi husika.
Amesema
ni vema wadau wanaotumia takwimu kwenye majukwaa mbalimbali na
waandishi wa habari kujenga tabia ya kuwasiliana na Ofisi ya Taifa ya
Takwimu kabla ya kutoa takwimu walizonazo ili kupata ukweli wa hali
halisi.
“Natoa
wito kwa wadau mbalimbali na waandishi wa habari kuhakikisha kuwa
mnapata takwimu sahihi hata kama mmezipata kutoka kwa viongozi,
tafadhali hakikisheni mnapitia mamlaka husika kupata ukweli wa takwimu
hizo ili kuepuka kutoa takwimu zisizo sahihi”, Amesisitiza Kamishna wa
Sensa.
Ametoa
wito kwa wadau mbalimbali kutembelea tovuti ya Ofisi ya Taifa ya
Takwimu ikiwa ni moja ya chanzo sahihi cha habari katika masuala yote
yahusuyo takwimu na rejea sahihi na kuongeza kuwa takwimu zote
zinazotumika kutengeneza sera za taifa za mipango ya maendeleo zinatoka
katika chanzo kimoja tu ambacho ni Ofisi ya Taifa ya Takwimu.
Katika
hatua nyingine Kamishna wa Sensa ya Watu na Makazi wa Ofisi ya Taifa ya
Takwimu Bi. Hajjat Amina Mrisho Said ametoa wito kwa Maofisa wa Takwimu
walio katika mikoa na wilaya mbalimbali nchini kutumia vikao mbalimbali
vinavyofanyika katika Halmashauri na mikoa kutoa elimu ya matumizi ya
takwimu zilizopo ili waweze kupanga mipango mbalimbali ya maendeleo na
kutatua kero mbalimbali za wananchi.
Amesema
takwimu zilizopo lazima zitafsiriwe na jukumu hilo lazima lifanywe na
wawakilishi hao wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu walio katika mikoa
mbalimbali nchini na kuongeza kuwa wataalam hao kwa kushirikiana na
viongozi wengine wa halmashauri wana jukumu la kutoa elimu kwa makundi
mbalimbali ya jamii hasa vijana ili waweze kujiajiri na kutumia fursa
zilizopo katika maeneo yao ili kupunguza utegemezi.
“Naomba
mtumie vikao hivyo vya hamashauri kutoa elimu kwa sababu tayari ninyi
mnazo takwimu, vikao vya halmashauri huwa vinahusisha viongozi
mbalimbali wa Serikali na jamii hivyo mnaweza kabisa kushauri na
kushawishi kwa viongozi hao kutumia takwimu sahihi ili kuondoa matatizo
mbalimbali likiwemo tatizo la ajira kwa vijana na kuondoa utegemezi kwa
kuwajengengea uwezo vijana wasio na ajira kujiajiri wenyewe”, amesema
Kamishna.
Aidha
ametoa wito kwa watafiti na wadadisi wa Madodoso ya Watu Wenye Uwezo wa
Kufanya Kazi 2014 watakaoendesha zoezi la utafiti wa idadi ya watu
wenye uwezo wa kufanya kazi kutoa elimu kwa vijana ambao hawana kazi
katika maeneo yote watakayopita ili kuwajengea uwezo wa kufanya kazi pia
kuwashauri kujiunga na vyuo vya ufundi Stadi (VETA) vilivyopo katika
maeneo mbalimbali nchini ili waweze kujiajiri na kuondoa wimbi la
utegemezi.
Mafunzo ya ISPS Code ya Maofisa waandamizi wa Ulinzi na Usalama yafunguliwa Bandari
Picha ya pamoja Maofisa waandamizi wa vyombo vya Ulinzi na usalama wa Bandari wakiwa na Mgeni rasmi Balozi wa Israel Mhe. Gil Haskel watatu kutoka kushoto waliokaa , akiwa na Mhe. Dr. Shaban Mwinjaka Katibu Mkuu Uchukuzi na Ndg. Phares Magesa aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa TPA kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo.
Ndg. Magesa akiwakaribisha wageni walipowasilia TPA
Mafunzo haya ya ISPS code yanafadhiliwa na Benki ya Dunia (WB) chini ya mradi wa EATTF miradi mwingine iliyopo kwenye EATTF ni Integrated Security System na Electronic Single Window System inayotarajiwa kuanza kutekelezwa na TPA kwa niaba ya Tanzania hivi karibuni.
Ndani ya chumba cha mafunzo wakati wa ufunguzi
TAARIFA ZA KIMICHEZO KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA TFF
WATANO KANEMBWA JKT WAFUNGIWA MECHI TATU
Kamati
ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imewafungia
mechi tatu wachezaji watano kati ya tisa wa timu ya Kanembwa JKT
waliolalamikiwa na Sekretarieti kwa kumpiga mwamuzi kwenye mechi ya Ligi
Daraja la Kwanza (FDL) iliyochezwa Novemba 2 mwaka jana.
Wachezaji
hao ni Bariki Abdul, Mrisho Musa, Nkuba Clement, Nteze Raymond na Philo
Ndonde. Wachezaji ambao hawakutiwa hatiani kutokana na ushahidi dhidi
yao kutojitosheleza ni Abdallah Mgonja, Mbeke Mbeke, Ntilakigwa Hussein
na Uhuru Mwambungu.
Mechi
hiyo dhidi ya Stand United iliyochezwa Uwanja wa Kambarage mjini
Shinyanga ilivunjwa na refa Peter Mujaya dakika ya 87 kutokana na
kupigwa na wachezaji hao baada ya kuamuru ipigwe penalti dhidi ya timu
yao.
Adhabu
hiyo imetolewa kwa kuzingatia Ibara ya 49 (1)(b) ya Kanuni za Nidhamu
za TFF baada ya kupitia vielelezo vilivyowasilishwa na Sekretarieti ya
TFF ambavyo ni ripoti ya refa, ripoti ya kamishna wa mechi hiyo na video
iliyoonesha tukio hilo.
Pia
kabla ya kutoa adhabu baada ya kusikiliza utetezi kutoka kwa
walalamikiwa ambao ni wachezaji hao na timu yenyewe ya Kanembwa JKT.
Nayo Kanembwa JKT imetiwa hatiani na kupigwa faini ya sh. milioni ambayo
inatakiwa kuilipa kabla ya kucheza mechi inayofuata.
Kamati
hiyo iliyokutana jana (Februari 9 mwaka huu) chini ya Mwenyekiti wake
Tarimba Abbas, kwanza imelaani kitendo cha wachezaji wa timu hiyo
kumzonga refa, kwani vitendo vya aina hiyo ndiyo vichocheo vya vurugu
viwanjani.
Lakini
pia imempongeza nahodha wa Kanembwa JKT, Mbeke Mbeke kwa kuwa mstari wa
mbele kuwazuia wachezaji wenzake waliokuwa wakimpiga refa wa mchezo
huo.
Vilevile
Kamati hiyo imesema aliyesababisha matatizo hayo ni refa Mujaya, na
ingawa ilikuwa na uwezo wa kumchukulia hatua lakini haikufanya hivyo kwa
vile hakukuwa na mlalamikaji na tayari Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB)
ilishamwadhibu.
MAJINA YA MABINGWA WA MIKOA MACHI 30
Vyama
vya Mpira wa Miguu vya mikoa vimetakiwa kuwasilisha majina ya mabingwa
wao kufikia Machi 30 mwaka huu kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa
(RCL).
Timu
zote zitakazofuzu kucheza RCL zinaruhusiwa kusajili wachezaji wapya
wasiozidi watano kutoka ndani ya mkoa kwa kufanya taratibu za uhamisho.
Kamati imesisitiza kuwa usajili wa RCL ni uleule uliotumika kwenye Ligi
ya Mkoa.
Kamati
ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
iliyokutana Februari 6 mwaka huu imekataa ombi la Chama cha Mpira wa
Miguu Mkoa wa Mwanza (MZFA) kuongeza timu za Ligi ya Mkoa kutoka 20 hadi
24.
Ikiwa
chini ya Mwenyekiti wake Geofrey Nyange, Kamati hiyo imesema kwa mujibu
wa Kanuni ya Ligi ya Mkoa, ligi hiyo inatakiwa kuwa na timu kati ya 16
na 20, hivyo vyama vya mpira wa miguu vya mikoa vinatakiwa kuendesha
ligi kwa kufuata kanuni.
Kamati
hiyo imeongeza kuwa hata kama ingekubalia ombi la MZFA kiutaratibu
lisingewezekana kwa vile kanuni hufanyiwa marekebisho baada ya msimu
kumalizika, wakati ombi hilo limewasilishwa katikati ya msimu.
KOCHA MARSH ASUBIRI VIPIMO VYA MWISHO
Kocha
Msaidizi wa Taifa Stars, Sylvester Marsh ambaye amelazwa Hospitali ya
Taifa Muhimbili (MNH) anasubiri vipimo vya mwisho ili aweze kuanza
matibabu.
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemtoa kocha huyo nyumbani kwake
jijini Mwanza na kumleta Dar es Salaam kwa lengo la kuhakikisha anapata
matibabu zaidi na kwa uangalizi wa karibu.
Tayari
majibu ya kipimo cha kwanza yameshapatikana, hivyo yanasubiriwa majibu
ya kipimo kingine ili aweze kuanza rasmi matibabu, lengo likiwa ni
kubaini kitaalamu ugonjwa unaomsumbua.
KIKOSI CHA TWIGA STARS KUAGWA FEB 12
Timu
ya Twiga Stars itaagwa rasmi Jumatano (Februari 12 mwaka huu) tayari
kwa safari ya Lusaka, Zambia kwa ajili ya mechi ya kwanza ya raundi ya
pili ya michuano ya Afrika kwa Wanawake (AWC) ambayo fainali zake
zitafanyika Oktoba mwaka huu nchini Namibia.
Msafara
wa timu hiyo itakayoondoka kwa ndege ya Fastjet utaongozwa na mjumbe wa
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
Ahmed Idd Mgoyi.
Hafla
ya kuwaaga wachezaji wa timu hiyo itafanyika saa 5 asubuhi kwenye ofisi
za TFF. Timu hiyo itaondoka Februari 13 mwaka huu alfajiri tayari kwa
mechi hiyo itakayochezeshwa na waamuzi kutoka Rwanda.
RAIS KIKWETE AKUTANA NA MJUMBE WA EU, NA SHIRIKA LA GLOBAL VOLUNTEERS LA MAREKANI IKULU
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea ujumbe toka Umoja wa Ulaya (EU) kutoka kwa Mkurugenzi wa EU pembe ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika ambaye pia ni mjumbe maalumu wa EU kwenye nchi za ukanda wa Maziwa Makuu, Ikulu jijini Dar es salaam leo Februari 10, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mkurugenzi wa EU pembe ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika ambaye pia ni mjumbe maalumu wa EU kwenye nchi za ukanda wa Maziwa Makuu, Bw. Koen Vervaeke (kushoto) na Mwakilishi Mkazi wa EU nchini Tanzania Balozi Filiberto Ceriani Sebregondi, bada ya kukutana nao Ikulu jijini Dar es salaam leo Februari 10, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea ujumbe toka Umoja wa Ulaya (EU) ukiongozwa na Mkurugenzi wa EU pembe ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika ambaye pia ni mjumbe maalumu wa EU kwenye nchi za ukanda wa Maziwa Makuu Bw. Koen Vervaeke, Ikulu jijini Dar es salaam leo Februari 10, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Bw. Burham Philbrook wa Shirika la Global Volunteers la Minnestota, Marekani, akishuhudiwa na Askofu Dkt. Owdenburg M. Mdegella wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Iringa walipomtembelea na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Februari 10, 2014
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea jarida toka kwa Bw. Burham Philbrook wa Shirika la Global Volunteers la Minnestota, Marekani, akishuhudiwa na Askofu Dkt. Owdenburg M. Mdegella wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Iringa walipomtembelea na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Februari 10, 2014.
PICHA NA IKULU
MAGARI ZAIDI YA 3000 YAKWAMA ENEO LA HEDARU BAADA YA MVUA KUBWA KUNYESHA NA KUZUIA BARABARA
Baadhi ya wasafiri waliokwama wakiangalia greda inayojaribu kutengeneza njia ili waweze kupita.
Wasafiri wakiwa wamekwama eneo la Hedaru
Maroli na mabasi yakiwa kwenye foleni baada ya njia kuzibwa na mafuriko ya maji
Wakandarasi wakijadiliana jambo ili kuweza kupata ufumbuzi
Umati wa wasafiri wakiwa wanashangaa jinsi barabara ilivyozuiwa na maji
Hii ndio hali halisi inavyoonekana malori yakiwa yamekwama katikati ya barabara
…………………………………………………………………..Magari zaidi ya 3000 yamekwama mda huu eneo la hedaru baada ya barabara kufungwa na kuzibwa na maji mengi yaliyosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha eneo hilo.Wasafiri wamekwama eneo hili kwani magari na mabasi pia magari ya mizigo yanashindwa kupita kwa kuwa njia haionekani.
Kampuni ya ujenzi inayojenga barabara hiyo wanajitaidi kuchimba maeneo ya pembeni ili kuweza kuhamisha maji ili angalau njia iweze kuonekana.Hali ni mbaya eneo hili hivyo serikali inatakiwa kuwahi kwenda kutoa msaada wa kuweza kupunguza maji na hatimaye magari yaweze kupita.
PINDA AKUTANA NA BALOZI WA ISRAEL
Waziri Mkuu , Mizengo Pinda akisalimiana na Balozi wa Israel nchini, Mhe. Gil Haskel kabla ya mazungumzo yao, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Februari 10, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Balozi wa Israel nchini, Mhe. Gil Haskel, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Februari 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
MTU MMOJA ANAYESADIKIWA KUWA JAMBAZI SUGU AMEUAWA NA WANANCHI WILAYANI MOMBA.
MNAMO TAREHE 09.02.2014 MAJIRA YA SAA 18:20
HRS JIONI MTU MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA HEZRON MWAISANILA (22) MKAZI WA ILOMBA JIJINI MBEYA ALIFARIKI DUNIA WAKATI ANAPATIWA MATIBABU HUKO KATIKA KITUO CHA AFYA TUNDUMA WILAYA YA MOMBA BAADA YA KUSHAMBULIWA NA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI WAKITUMIA SILAHA ZA JADI FIMBO NA MAWE. CHANZO CHA MAUAJI HAYO NI TUHUMA ZA WIZI BAADA YA MAREHEMU HUYO AKIWA NA WENZAKE WAWILI WALIOKIMBIA WALIPORA FEDHA TASLIMU TSHS. MILIONI 1,200,000/=, ZAMBIA KWACHA MILIONI 1,200,000/=, DOLA ZA KIMAREKANI 60 NA SIMU YA KIGANJANI MALI YA DENIS ODAS (22) MFANYABIASHARA NA MKAZI WA MAPOROMOKO – TUNDUMA MAJIRA YA SAA 16:45HRS JIONI AKIWA ANATOKA DUKANI. MAREHEMU ALIKUWA NI JAMBAZI SUGU NA ALIKUWA ANATAFUTWA NA POLISI KUHUSIANA NA MATUKIO MBALIMBALI YA UHALIFU LIKIWEMO TUKIO LA UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA BAADA YA KUPORA PESA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.675 CLX AINA YA TOYOTA KLUGER MNAMO TAREHE 25.01.2014 MAJIRA YA SAA 20:00HRS USIKU HUKO ENEO LA ISYESYE JIJINI MBEYA AKITUMIA SILAHA AINA YA SMG NA KUMJERUHI MFANYABIASHARA MMOJA AITWAYE OBADIA JANAS (41) MKAZI WA ISYESYE KWA KUMPIGA RISASI MGUU WA KULIA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE WAWAFIKISHE WATUHUMIWA WA UHALIFU WANAOWAKAMA KWA TUHUMA MBALIMBALI KATIKA MAMLAKA HUSIKA KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.
WATU 07 WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA KWA TUHUMA ZA KUMJERUHI MBUNGE.
MBUNGE WA JIMBO LA MBEYA VIJIJINI – CCM MHE. JACKSON MWANJALI (55)
ALIJERUHIWA KWA KUPIGWA RUNGU NA FIMBO KICHWANI NA KUNDI LA VIJANA
WANAODAIWA KUWA NI WAFUASI WA CHADEMA. TUKIO HILO LILITOKEA MNAMO TAREHE
09.02.2014 MAJIRA YA SAA 10:00HRS ASUBUHI HUKO KATIKA KITONGOJI CHA SHIPONGO WILAYA YA MBEYA VIJIJINI WAKATI MBUNGE HUYO AKIWA NA SHADRACK MWATUNGUJA -
KATIBU WA UCHUMI NA MIPANGO WILAYA YA MBEYA VIJIJINI NA BAADHI YA
VIONGOZI WA CCM WA WILAYA YA MBEYA VIJIJINI WAKIWA WANATEMBELEA VITUO
VYA KUPIGIA KURA KATIKA KATA YA SANTILYA AMBAVYO VIPO KATIKA JIMBO LAKE.
MTUHUMIWA PAUL WUMBULA (32) MKAZI WA MBALIZI NA WENZAKE SITA
WALIKAMATWA KUHUSIANA NA TUKIO HILO. WAHANGA WALIPATIWA MATIBABU NA
KURUHUSIWA, HALI ZAO ZINAENDELEA VIZURI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA
WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJIHUSISHA NA VURUGU KWANI NI KINYUME
CHA SHERIA NA KAMWE JESHI LA POLISI HALITASITA KUMCHUKULIA HATUA ZA
KISHERIA MTU YEYOTE YULE ATAKAYEJIHUSISHA NA KITENDO CHOCHOTE CHA
UVUNJIFU WA AMANI.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Sekretarieti ya Bunge la Katiba kukabidhiwa Ukumbi Jumatano
Spika wa Bunge Mhe. Anna Makinda akijaribu mojawapo ya viti vipya vilivyofungwa katika ukumbi wa Bunge tayari kwa ajiri ya Matumizi wakati wa Bunge la Katiba. Mhe. Makinda aliongoza ujumbe wa Tume ya Utumishi wa Bnge kufanya ukaguzi wa mwisho kabla ukumbi huo haujakabidhiwa kwa Sekretariat ya Bunge la Katiba Jumatano wiki hii.
Spika wa Bunge Mhe. Anna Makinda akiwa na wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Bunge kukagua ukumbi huo
Spika wa Bunge Mhe. Anna Makinda, (katikati) Naibu Spika Mhe. Job Ndugai (kushoto), Katibu wa Bunge (Wa pili Kulia) na Mhe. Hamadi Rashid Mohamed Kulia wakiangalia baadhi ya maboresho yaliyofanywa katika Ukumbi wa Bunge kwa ajili ya Bunge la Katiba. .Muonekano wa Ndani ya ukumbi huo baada ya kazi ya uwekaji viti kukamilika .Muonekano wa Ndani ya ukumbi huo baada ya kazi ya uwekaji viti kukamilika .Muonekano wa Ndani ya ukumbi huo baada ya kazi ya uwekaji viti kukamilika
Spika wa Bunge Mhe. Anna Makinda pamoja na wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Bunge wakiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi walioshiriki kuukarabati ukumbi wa Bunge kwa ajiri ya matumizi ya Bunge la Katiba.
Msama akabidhi misaada kwa vituo vitatu vya jijini Dar es salaam
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akikabidhi vyakula
mbalimbali kwa HalimaMpeta Mkurugenzi wa kituo cha kulelea watoto yatima
cha Mwandaliwa kilichopo Boko jijini Dar es salaam jana katika makao
makuu ya ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es salaam.
……………………………………………………………………………
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Msama Promotions waandaaji wa Matamasha ya Kirimasi na Pasaka jana ilikabidhi misaada mbalimbali kwa vituo vitatu vya jijini Dar es Salaam, ikitimiza ahadi ya kuisaidia jamii kabla ya Tamasha la mwaka huu linalotarajia kuanza Aprili 20 hapa nchini.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama misaada hiyo iliyogharimu shilingi milioni 7 imekabidhiwa katika vituo vya TUVUCHIDO cha Temeke Maganga, Malaika Kids cha Mwananyamala na kituo cha Yatima cha Mwandaliwa.
Msama alisema katika sehemu ya msaada huo pesa taslim shilingi milioni 2.9 ni ada kwa wanafunzi na nyingine ni kwa vifaa mbalimbali yakiwemo madaftari, sabuni za mche, unga, mafuta ya kupaka na sukari.
Aidha Msama alisema misaada hiyo imetokana na mfuko wa Tamasha la Pasaka kama ilivyokuwa kwenye Tamasha la Krismasi ambalo walikabidhi misaada ya shilingi milioni 4.
Mkurugenzi wa TUVICHIDO, Honarata Michael alimpongeza Msama kwa kuwajali watoto na jamii kwa ujumla.
Naye Mkurugenzi wa kituo cha Mwandaliwa, Halima Mpeta alisema anamshukuru Msama kwa kujali jamii kwani katika kituo chake si mara ya kwanza kukisaidia na amezidi kumuomba aendelee na moyo wa kukisaidia kituo chake na vingene vyenye mahitaji.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akikabidhi masanduku ya miche ya sabuni kwa Halima Mpeta Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akikabidhi mafuta ya kupaka na vyakula mbalimbali kwa mtoto Heidin Din wa kito cha watoto yatima cha TUVUCHIDO cha Temeke Maganga.Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akikabidhi vyakula mbalimbali kwa Honorata Michael wa kutoa cha watoto yatima cha TUVUCHIDO cha Temeke Maganga Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akikabidhi vyakula mbalimbali kwa watoto yatima wa kituo cha Malaika cha Mwananyamala Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akikabidhi fedha taslimu shilingi 700.000 kwa Honorata Michael wa TUVUCHIDO cha Temeke Maganga kwa ajili ya kulipia karo za watoto wanaosoma katika shule mbalimbali kutoka kituoni hapo. Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akikabidhi hundi ya shilingi 700.000 kwa watoto wa kituo cha Mwandaliwa. Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akikabidhi madaftari na vifaa vingine vya shule kwa ajili ya watoto yatima wa vituo vya Malaika, Mwandaliwa na TUVUCHIDO cha Temeke Maganga vya jijini Dar es salaam.
Bi. Honorata Michael wa TUVUCHIDO cha Temeke Maganga akishukuru kwa niaba ya wenzake mara baada ya kupokea msaada huo jana.
……………………………………………………………………………
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Msama Promotions waandaaji wa Matamasha ya Kirimasi na Pasaka jana ilikabidhi misaada mbalimbali kwa vituo vitatu vya jijini Dar es Salaam, ikitimiza ahadi ya kuisaidia jamii kabla ya Tamasha la mwaka huu linalotarajia kuanza Aprili 20 hapa nchini.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama misaada hiyo iliyogharimu shilingi milioni 7 imekabidhiwa katika vituo vya TUVUCHIDO cha Temeke Maganga, Malaika Kids cha Mwananyamala na kituo cha Yatima cha Mwandaliwa.
Msama alisema katika sehemu ya msaada huo pesa taslim shilingi milioni 2.9 ni ada kwa wanafunzi na nyingine ni kwa vifaa mbalimbali yakiwemo madaftari, sabuni za mche, unga, mafuta ya kupaka na sukari.
Aidha Msama alisema misaada hiyo imetokana na mfuko wa Tamasha la Pasaka kama ilivyokuwa kwenye Tamasha la Krismasi ambalo walikabidhi misaada ya shilingi milioni 4.
Mkurugenzi wa TUVICHIDO, Honarata Michael alimpongeza Msama kwa kuwajali watoto na jamii kwa ujumla.
Naye Mkurugenzi wa kituo cha Mwandaliwa, Halima Mpeta alisema anamshukuru Msama kwa kujali jamii kwani katika kituo chake si mara ya kwanza kukisaidia na amezidi kumuomba aendelee na moyo wa kukisaidia kituo chake na vingene vyenye mahitaji.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akikabidhi masanduku ya miche ya sabuni kwa Halima Mpeta Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akikabidhi mafuta ya kupaka na vyakula mbalimbali kwa mtoto Heidin Din wa kito cha watoto yatima cha TUVUCHIDO cha Temeke Maganga.Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akikabidhi vyakula mbalimbali kwa Honorata Michael wa kutoa cha watoto yatima cha TUVUCHIDO cha Temeke Maganga Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akikabidhi vyakula mbalimbali kwa watoto yatima wa kituo cha Malaika cha Mwananyamala Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akikabidhi fedha taslimu shilingi 700.000 kwa Honorata Michael wa TUVUCHIDO cha Temeke Maganga kwa ajili ya kulipia karo za watoto wanaosoma katika shule mbalimbali kutoka kituoni hapo. Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akikabidhi hundi ya shilingi 700.000 kwa watoto wa kituo cha Mwandaliwa. Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akikabidhi madaftari na vifaa vingine vya shule kwa ajili ya watoto yatima wa vituo vya Malaika, Mwandaliwa na TUVUCHIDO cha Temeke Maganga vya jijini Dar es salaam.
Bi. Honorata Michael wa TUVUCHIDO cha Temeke Maganga akishukuru kwa niaba ya wenzake mara baada ya kupokea msaada huo jana.
Mashabiki wa Tamasha la Pasaka kuchagua mikoa
Na Mwandishi Wetu
WAKATI Tamasha la Pasaka kinatarajia kufanyika mwaka huu kwenye mikoa mbalimbali hapa nchini, mashabiki wa tamasha hilo ndio watachagua mikoa itakayofanyika.
Mfumo huo utasaidia mashabiki wa mikoani kuteua mikoa yao ifikiwe na tamasha hilo la kumuimbia na Kumtukuza Mungu kupitia nyimbo na mapambio kupitia nyimbo mbalimbali.
Wakati taratibu za maandalizi zikiendelea, Kampuni ya Msama Promotions ambao ndio waandaaji wa tamasha hilo hivi sasa wanasubiri kibali kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama bado tunasubiri Basata watakabidhi kibali cha kufanikisha tamasha hilo ambalo mikoa sita imeonesha.
Msama alisema tamasha la mwaka huu wamejipanga kusikiliza mikoa mingi zaidi kwa sababu inaonekana mikoa mingi ina kiu ya kupata neno la Mungu kupitia waimbaji mbalimba wa Tanzania na nje.
Aidha Msama alisema wako kwenye mchakato wa kuandaa mfum ambao utafanikisha mikoa kujipigia kura.
NMB YAFUNGUA RASMI TAWI LA HIMO
Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mhe.Dkt. Ibrahimu Msengi (kati) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa tawi la NMB Himo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro. Wa kwanza kushoto ni Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini, Vicky Bishubo akifuatiwa na Meneja Mawasiliano wa NMB, Josephine Kulwa na wa kwanza kulia ni Mbunge wa Jimbo la Vunjo,Mhe.Augustino Mrema wakishuhudia uzinduzi huo. Hafla ya uzinduzi wa tawi hilo la NMB Himo ulifanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya tawi hilo mkoani Kilimanjaro.
Sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla ya uzinduzi huo wakifuatilia kwa makini sherehe za uzinduzi wa tawi jipya la NMB Himo
MORO VETERAN WAICHAPA GOLANI VETERAN YA KIMARA BAO 4
Kikosi cha Timu ya Golani Veteran ya Kimara Jijini Dar es salaam Kilichofanya Ziara Mkoa wa Morogoro.
Kikosi cha Timu ya Moro Veteran Kilichoanza .
Moja ya Hekaheka katika Lango la Golani Veterani katika Mchezo wa Kirafiki Uliopigwa Katika Uwanja Wa Jamuhuri Mkoani Morogoro.
Beki wa Golani Veteran Akiondosha Moja ya Hatari Katia Lango lake.
Mshambuliaji wa Zamani wa Timu ya Polisi Morogoro Ambaye kwa sasa anaichezea Timu ya Moro Veteran Mokil Rambo Akitafuta Mbinu za Kuwatoka Mabeki wa Golani Veteran Katika Mchezowa Kirafiki Uliochezwa Katika Uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro .
Mchezaji wa Zamani wa Timu za Morogoro Adam Seleman wa Moro Veteran akiwa
katika Hekaheka za Kutafuta Mbinu za Kuwatoka Mabeki wa Timu ya Golani
Veterani ya Kimara Dar es Salaam katika Mchezo wa KirafikiUliopigwa
Katika Dimba la Jamuhuri Mkoani Morogoro.
Wachezaji wakongwe wa Golani Veteran Ambao walikuwa Kivutio Katika Mchezo
Timu ya Soka ya Moro Veteran ya Mkoani Morogoro Leo Wameichapa Timu ya Golani Veteran ya
Kimara Dar es Salaam jumla ya Magoli 4 kwa Moja.Mchezo huo
uliopigwa katika uwanja wa Jamuhuri Mkoani Morogoro Ulikuwa wa Kasi na
Upinzani wa hali ya Juu.
Hadi Mapumziko Matokeo Yalikuwa Sare ya Bila Kufungana.
Kipindi
cha Pili Moro Vetrani Walifungua Karamu ya Mgoli Katika Dk 50 Goli
lilofungwa Na Seif baada ya Kupewa Pasi na Kufumua Shuti lilomshinda
Golikipa.
Moro
Veterani Waliendela Kulishambulia Goli la wapinzani Wao Na Kufanikiwa
Kupata Mabao Mawili Katika Dakika za 67 na 70 Kupitia kwa Mshambulizi
wao Khamis .
Magoli
hayo yaliwachanganya Benchi la Ufundi la Gorani Veterani hali
Iliyowafanya Kufanya Mabadiliko Haraka na Kuwasaidia Kupata Bao La
kufuta Machozi Katika Dk 79 ya Mchezo.Wakiwa Bado wanaimani wanaweza
Kuzudisha Magoli mawili yaliosalia walijisahau Na kukuta wakipigwa Goli
na 4 katika Dk 87 Ya Mchezo Goli Lililofungwa na Khamisi Madole.
Hadi Mwisho Moro Veteran 4 Golani Veteran 1
RAYS OF LIGHT EXHIBITION IMPRINTS ITS FOOT ON THE LAND OF THE KILIMANJARO
Rt.
Hon. Mizengo Peter Pinda, the Prime Minister of the United Republic of
Tanzania (left) and Mr. Jehangir Bhaloo, President of the Aga Khan
Council for Tanzania, officially cutting the ribbon at the opening
ceremonies of the Rays of Light Exhibition at the Diamond Jubilee Hall
in Dar es Salaam, Tanzania. (Photo: RAYSOFLIGHT/Aly Z. Ramji).
Rt.
Hon. Mizengo Peter Pinda, the Prime Minister of the United Republic of
Tanzania and Mr. Jehangir Bhaloo, President of the Aga Khan Council for
Tanzania, receiving a tour from Karim Kanji(tour guide) for the Rays of
Light Exhibition. (Photo: RAYSOFLIGHT/Aly Z. Ramji).
After visiting France, Portugal, United States, United Kingdom, UAE, Uganda, and Canada, the Rays of Light: Glimpses into the Ismaili Imamat, finally
makes its hallmark debut on Tanzanian soil. The much-anticipated
Exhibition marks a significant milestone for Tanzania as it coincides
with the upcoming 50th Anniversary of the Union of Tanganika and Zanzibar.
Opened
officially today at the Diamond Jubilee Hall in Dar es Salaam, by the
Rt. Honourable Mizengo Peter Pinda, the Prime Minister of the United
Republic of Tanzania, the Ismaili Jamat and the peoples of Tanzania will
have an exclusive peek into the world of the Shia Ismaili Imamat and
the role of the Aga Khan development(AKDN) globally.
The
vision of both the late Sir Sultan Mohamed Shah(Aga Khan III) and a
glimpse of the work of H H the Aga Khan over the past 50 years, are
demonstrated through the varied projects that are in existence today.
During
the opening ceremony, amid the joy and fanfare at the Diamond Jubilee
Hall, Honorable Mizengo Pinda, thanked the Aga Khan Shia Imami Ismaili
Council for Tanzania for organizing the event, and stated “We are
here to celebrate this historic event worldwide, which indeed reflects
the life and work of His Highness Prince Aga Khan, a true pioneer and
one of Tanzania’s most committed and trusted friends. A person whose
family and community have been the pride of the great things we are
proud of as a Country.”
For
Tanzanians, this marks a truly exclusive occasion; many of the featured
projects demonstrate AKDN’s rich history in the country. The Imamat
initiatives, specifically in socio-economic and cultural programs date
back over a century in Tanzania, with the establishment of the first Aga
Khan Girls School in Zanzibar in 1905. By the 1960’s there were nearly
65 Aga Khan Schools across the nation. The Aga Khan Education Services
is currently planning the construction of a $30 million Aga Khan
Academy, which will be affiliated with all other Aga Khan Academies
globally.
Another integral program in the country is the current establishment of
the Aga Khan University in Arusha. The AKU plays an integral role in
educating skilled professionals with an ethic of social responsibility
and commitment to serving their community. The AKU Arusha Campus will
boast professional graduate schools in management, law, government and
public policy, journalism and tourism to name a few.
The
Aga Khan Health Services Tanzania has had a major impact in the
country, with the first dispensary being established in 1929. Since
then, numerous other health initiatives through AKHST have been
established; these include the Aga Khan Hospital, as well as numerous
Outreach Health Centers in Mwanza, Morogoro, Mbeya, Iringa, Arusha,
Dodoma and Mbezi Beach, and of course the newly inaugurated Oncology
wing, which was opened in January 2014.
The
historical association between Tanzania and the Ismaili Imamat span
over a century exemplified by H H the Aga Khan’s presence at the
Independence of Tanganyika in 1961, it was in 1991, that the Aga Khan
signed an Accord of Cooperation for Development with the then President,
H.E. Ali Hassan Mwinyi. Just a decade later, in 2001, former President
H.E. Benjamin William Mkapa signed an official protocol with H H the Aga
Khan enhancing the collaboration between the AKDN and Tanzania, by
formalizing the establishment of a mission and enabling it to facilitate
the optimal utilization of resources for the AKDN’s objectives.
President of the Aga Khan Council for Tanzania, Mr. Jehangir Bhaloo during his opening remarks stated, “The
Rays of Light’ is a celebration of a life. Not just any life. It is a
celebration of the life and work of the Imam of the time. In our
Shia ethical tradition, the Imam leads not only in the interpretation of
the faith but also in the effort to improve the quality of life of his
community and of wider societies within which the community lives. A
guiding principle of the Imamate’s institutions, according to His
Highness Aga Khan is to “replace walls that divide with bridges that
unite.”
With
far too many development programs to list, it is known that the
cooperation between Tanzania and the AKDN has significantly impacted the
lives of many Tanzanians. Given this unique history with Tanzania, the Rays of Light
Exhibition will also be visited by H.E. Dr. Mohamed Gharib Bilal, the
Vice President of the United Republic of Tanzania, as well as former
Tanzanian Presidents H.E. Al-Haj Ali Hassan Mwinyi and H.E. Benjamin
William Mkapa.
TAI YATOA MAFUNZO KWA VITENDO JUU YA KUNAWA MIKONO NA KUSAFISHA KINYWA KWA WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI KILIMANI JIJINI DAR ES SALAAM
Katibu
Mkuu wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Tanzania Aspiration Initiatives –
TAI Bw. Gwamaka Mwabuka akitoa maelekezo kwa mwanafunzi wa darasa la
pili shule ya Msingi Kilimani Juma Abdul jinsi ya kunawa mikono kwa
usahihi ili kuipeka magonjwa. Wanaoshuhudia ni baadhi ya wanafunzi toka
Denmark waliopata mualiko na TAI kupitia taasisi ya Global Platform.
1.Wanafunzi
wa darasa la pili shule ya msingi Kilimani wakijifunza kwa vitendo
jinsi ya kusafishwa kinywa na kuepukana na magonjwa yanayotokana na
kutosafisha kinywa.
………………………………………………………………………………………….
Taasisi
isiyo ya kiserikali ya TAI – Tanzania Aspiration Initiatives imefanya
mafunzo ya kulinda afya kwa vitendo kwa wanafunzi Zaidi ya 200 wa Darasa
la Kwanza, la pili na darasa la awali katika shule ya msingi Kilimani
iliyopa Sinza Uzuri wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam ikiwa ni
muendelezo wa miradi miwili inayojulikana kama Mikono Ming’avu (MiMi) na
Kinywa Kisafi (KiKi).
Miradi
yote ina lengo kuu la kupambana na magonjwa yanayoweza kuzuilika kama
Magonjwa ya tumbo na yale ya meno na kinywa yanayoathiri zaidi watoto.
Mafunzo hayo pia yalishirikisha Vijana wengine kutoka nchini Denmark
walio nchini katika ziara ya kimasomo chini ya Jukwaa la kimataifa la
Global Platform.
Mikono
Ming’avu (MiMi) ni mradi uliyojikita katika kutoa mafunzo kwa vitendo
kwa watoto wa shule za msingi kutatua tatizo la magonjwa
yanayosababishwa na mikono michafu kama vile Pneumonia na homa ya
Matumbo (Diarrhea). Mradi huu tayari umeshawafikia Zaidi ya watoto 1000
katika baadhi za shule za msingi jijini Dar es salaam huku malengo ni
kufikia shule zote za msingi Tanzania nzima.
“Hatua
hizi za TAI ni baada ya kuona Watanzaia wengi hawana tabia ya kunawa
mikono na sabuni kwa ufasaha ambapo ni moja ya sababu inayochangia
magonjwa yanayoweza kuzuilika, lakini pia yanaathiri ukuaji wa mtoto.
Kila mwaka watoto Zaidi ya milioni 3.2 duniani walio chini ya miaka 5
wanakufa kwa sababu ya homa ya matumbo na pneumonia yakiwa ni magonjwa
yanayoongoza kusababisha vifo kwa watoto baada ya malaria hasa katika
nchi za kusini mwa jangwa la sahara, Tanzania ikiwepo” alisema Bw.
Gwamaka Mwaibuka, Katibu Mkuu wa TAI.
Kinywa
Kisafi (KiKi) ni ni moja kati ya mradi ya TAI ukiwa na lengo la
kupunguza tatizo la magonjwa ya Kinywa na meno kwa watoto ambapo taasisi
hiyo hufanya mafunzo kwa vitendo kwa kushirikiana na wataalam
kuwafundisha watoto njia sahihi za kufanya usafi wa meno na kinywa na
kuhimiza tabia ya kusafisha kinywa kuanza tangu utotoni. TAI ni taasisi iliyoanzishwa kwa lengo la kuimarisha maisha ya kila mmoja katika jamii hasa watu wanaoushi katika mazingira magumu na umasikini kupitia sekta tano za Elimu, Afya, Ujasiriamali, Teknolojia ya Habari na Mazingira. Kwa taarifa Zaidi ingia www.tai.or.tz au Tufuate katika ukurasa wetu wa Facebook www.facebook.com/tai2012.
UMOJA WA MATAIFA WASISITIZA UMUHIMU WA KUWA NA UTAMADUNI MZURI WA KUENZI WANAWAKE WANAOLETA MABADILIKO KWENYE JAMII
Picha
juu na chini ni Mwandishi wa habari na mpiga picha kutoka Ufaransa,
Pierre-Yves Ginet akizungumza na wanafunzi wa shule za sekondari
mbalimbali za jijini Dar es Salaam na kuwaonyesha picha na kuwapa
ufafanuzi wa mambo mbalimbali ambayo wakinamama wamekuwa wakifanya kwa
mustakabali kwa kuleta usawa na haki za wanawake duniani.
Shirika
la Ufaransa la Alliance Francaise de Dar es Salaam liliandaa safari ya
maonyesho iliyopewa jina “women in Resistance by the talented French
photo-journalist Pierre-Yves Ginet.
Mwandishi
wa habari huyo mpiga picha Pierre-Yves Ginet ambaye alifanya kazi ya
kutafuta wanawake wanaojituma katika maisha yao ya kila siku na kazi
zake zimeweza kuwapa ari na moyo wakinamama wengi Afrika.
Kati
ya 2001 na 2006, alisafiri zaidi ya nchi 17 akipiga picha za wakinamama
ambayo katika shughuli zao waliweza kufungua ukurasa mpya na
kubadilisha historia katika kizazi cha leo.
Katika
shughuli na katika njia tofauti walizotumia katika kubadilisha maisha
wa wakinamama wengi duniani, wanawake kupitia kazi za picha Ginet
wameweza kuwa na dhamira moja kubwa nayo ni kubadilisha maisha ili
kuweza kuwa matumaini ya kuwa na maisha bora zaidi kwa sasa na baadaye.
Maonyesho
hayo ya lengo la kuwapa usawa wakinamama wote kupitia mabara yote hapa
duniani na hasa nchi zinazoendelea, sehemu za vita.
Na
sehemu kubwa ya picha hizo zinaonyesha jinsi wakinamama wanavyopambana
ili kujikwamua katika unyonge na ukandamizaji wa aina yoyote hapa
duniani.
Mmoja
wa wananfunzi akibadilishana mawazo na Mwandishi wa habari na mpiga
picha kutoka Ufaransa, Pierre-Yves Ginet anayetumia maonyesho ya picha
mbalimbali kuelimisha jamii kupitia picha hizo.
Afisa
Habari kutoka Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Usia
Nkhoma Ledama akifafanua jambo kwa wanafunzi wa shule za sekondari
mbalimbali za jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya siku ya
kimataifa ya kupinga ukeketaji duniani.
Ujumbe
wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Katika kuadhimisha siku ya kimataifa
ya kupinga ukeketaji duniani inayoambatana na siku ya Wanawake Duniani
ni kufikisha sifuri katika kuondoa swala ukeketaji duniani.
Ujumbe
unasema kwamba ukeketaji umepungua katika sehemu kubwa ya dunia na
takwimu zinasema kwamba zaidi ya wanawake na wasichana 125 milioni ambao
wanaishi katika dunia ya leo katika nchi 29 za Afrika na Mashariki ya
kati walifanyiwa vitendo vya ukeketaji, na kama swala hii likiendelea
zaidi ya wasichana 86 milioni duniani watafanyiwa vitendo vya ukeketaji
kufikia mwaka 2030.
Salome
Anyoti kutoka shirika la umoja wa mataifa la wanawake akisisitiza jambo
kwa wanafunzi wa sekondari wa kutoka shule mbalimbali hapa Dar es
Salaam katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani kwa kuangali picha za
wakinamama walioleta mabadiliko katika maisha yao na wengine kwa
ujumla.
CHUO CHA MAENDELEO YA UTALII ZANZIBAR CHAFANYA SHEREHE ZA MAHAFALI YA TANO.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk akizunguza na wahitimu mbalimbali (hawapo pichani) mara baada ya kuwatunuku vyeti na stashahada katika Mahafali ya tano Chuoni hapo, (kulia yake) Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Khamis Mussa Omar na (kushoto) Kaimu Mwenyekiti Bi. Naila Jidawi.
Mkurugenzi wa Chuo cha Maendeleo ya Utalii Zanzibar Bi. Zulekha Khamis Omar akitoa maelezo juu maendeleo ya Chuo katika Mahafali ya tano Chuoni hapo. Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha Maendeleo ya Utalii Zanzibar Khamis Mussa Omar akieleza machache kuhusu muelekeo wa Chuo hicho na kumkaribisha Mgeni rasmin kutunuku vyeti kwa wahitimu.
Baadhi ya wahitimu wa Mapishi ya vyakula na Uokaji wakiwa wamesimama mara baada ya kutunukiwa vyeti na Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk katika sherehe zilizofanyika Chuoni hapo
Baadhi ya wageni waalikwa waliofika katika sherehe ya Mahafali ya tano ya Chuo cha Maendeleo ya Utalii Maruhubi Zanzibar.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk akimpa zawadi ya mlango kwa niaba ya wanafunzi wa ICT & ACCOUNT, Maalim. Hassan Mrisho Haji katika sherehe ya Mahafali iliyofanyika Chuoni hapo.
Wapiga Picha nao wakiuza picha zao mara baada ya kumaliza kwa Mahafali chuoni hapo. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).Baadhi ya wahitimu wakimsikiliza Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk (hayupo pichani) ambae ni mgeni rasmin wa Mahafali ya tano ya Chuo cha Maendeleo ya Utalii Maruhubi Zanzibar.
MTEMVU ANOGESHA MASHINDANO YA SERIKALI ZA MITAA TEMEKE
Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (kulia) akimkabidhi Nahodha wa
Timu ya Jamaica ya Mtaa wa Keko Molemo, Paulo Peter zawadi ya sh.
300,000 baada ya kuifunga timu ya DotmondMtaa wa Jamaica ya Mtaa
wa Keko Magurumbasi katika mechi ya kuchagua wachezaji wa kuunda timu
ya kombaini ya Kata ya Keko jana kwenye Uwanja wa Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam Kitivo cha Elimu (DUCE), Chang,ombe Dar es Salaam . Jamaica
lishinda mabao 3-1. Pia timu ya Dotmond ilizawadiwa sh. 200,000.
Abbas Mtemvu akimkabidhi Nahodha wa timu ya Dotmond ya Maa wa
Keko Magurumbasi zawadi ya sh. 200,000 baada ya kuwa washndi wa pili katika mchezo huo.
Bakari Hemed wa timu ya Dotmond akka mca Mbegu
Wapenzi wa soka wakiangalia mechi hiyo.
HATIMAYE MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KWA AJILI YA MAISHA PLUS/MAMA SHUJAA WA CHAKULA YATANGAZWA RASMI.
Kutoka
kushoto ni Afisa Mtendaji wa Kampuni ya DMB ambao ni wamiliki wa Maisha
Plus Masoud Ally (Kipanya) , Sharon Mariwa Meneja wa Mahusiano OXFAM,
Francis Bonda(Kaka Bonda) Mkurugenzi wa Usanifu katika Kampuni ya DMB
pamoja na Mkamiti Mgawe Afisa utetezi wa haki za kiuchumi OXFAM, wakati
wa kutangaza rasmi majina ya waliochaguliwa katika Maisha Plus/ Mama
Shujaa wa Chakula
Afisa
Mtendaji wa Kampuni ya DMB ambao ni wamiliki wa Maisha Plus Masoud Ally
(Kipanya) akielezea Mchakato mzima wa kazi ilivyokuwa kabla , wakati wa
kuwatafuta washiriki wa Maisha Plus/Mama Shujaa wa Chakula na kutaja
rasmi majina ya waliochaguliwa katika usahili huo.
Francis
Bonda(Kaka Bonda) Mkurugenzi wa Usanifu katika Kampuni ya DMB akitilia
mkazo baadhi ya mambo wakati wa kutangaza rasmi majina ya waliochaguliwa
kuingia Maisha Plus/ Mama Shujaa wa Chakula.
Baadhi
ya Waandishi wa Habari na wadau Mbalimbali wakiwa wanasikiliza
kutangazwa kwa majina ya waliochaguliwa katika Shindano la Maisha Plus/
Mama Shujaa wa Chakula.
*************
Majina ya waliochaguliwa kwa ajili ya usaili wa
Mama Shujaa wa Chakula / Maisha Plus 2014.
Mama Shujaa wa Chakula / Maisha Plus 2014.
Usaili:
Mama Shujaa watapigiwa kura mtandaoni ili kupata washiriki
20 ambao wataingia kijijini Maisha Plus. Zoezi la kuwapigia kura litafanyika
baada ya uhakiki ‘verification’ pamoja na upigaji picha kuthibitisha taarifa
walizojaza kwenye fomu.
20 ambao wataingia kijijini Maisha Plus. Zoezi la kuwapigia kura litafanyika
baada ya uhakiki ‘verification’ pamoja na upigaji picha kuthibitisha taarifa
walizojaza kwenye fomu.
Kauli mbiu
ya Mwaka huu ni Wekeza kwa wakulima
wadogo wanawake. INALIPA.
ya Mwaka huu ni Wekeza kwa wakulima
wadogo wanawake. INALIPA.
Vijana wa Maisha Plus watagawanywa katika makundi
mawili ya watu 20 na kupelekwa katika vijiji vilivyochaguliwa Iringa na
Zanzibar, huko wataishi pamoja na familia zilizochaguliwa na kutakiwa kuishi
maisha sawa na familia hizo. Zoezi kuu litakuwa kusaidia kutatua changamoto
zinazowakabili wakazi wa vijiji hivyo kama changamoto za maji, n.k.
mawili ya watu 20 na kupelekwa katika vijiji vilivyochaguliwa Iringa na
Zanzibar, huko wataishi pamoja na familia zilizochaguliwa na kutakiwa kuishi
maisha sawa na familia hizo. Zoezi kuu litakuwa kusaidia kutatua changamoto
zinazowakabili wakazi wa vijiji hivyo kama changamoto za maji, n.k.
Baada ya
siku 7 wanakijiji watatakiwa kuwapigia kura vijana hao ili kupata jumla ya
vijana 18 watakaopelekwa katika kijiji cha Maisha Plus kuungana na wenzao 12
kutoka nchi za Burundi, Kenya, Rwanda na Uganda.
siku 7 wanakijiji watatakiwa kuwapigia kura vijana hao ili kupata jumla ya
vijana 18 watakaopelekwa katika kijiji cha Maisha Plus kuungana na wenzao 12
kutoka nchi za Burundi, Kenya, Rwanda na Uganda.
Kauli mbiu
ya Mwaka huu ni Maisha Plus REKEBISHA.
ya Mwaka huu ni Maisha Plus REKEBISHA.
Majina
Mama Shujaa wa Chakula
- Amina Kupela Chikaponya – Mtwara
- Anna James Yuda – Morogoro
- Anna Mwanilyela Chrisant –
Katavi - Bahati Muriga –Mwanza
- Clara Ancilla Ibihya – Pwani
- Cristina Kurwa Malale –
Zanzibar - Dina Rusoti – Mara
- Dionisia Rashidi Karata – Tanga
- Doricus Msafiri Shumbi –
Singida - Edina Jamas – Mbeya
- Elinuru Moses Pallangyo –
Arusha - Elizabeth Matayo – Geita
- Elizabeth Simon – Morogoro
- Ezeleda Chedego – Dodoma
- Fredina M. Said – Shinyanga
- Gladness Ebenezery Mmary –
Kilimanjaro - Grace G.D. Mahumbuka – Kagera
- Janeth Niima – Manyara
- Kuruthumu Ramadhani Mwengele –
Tanga - Leah Dominick Mnyambugwe –
Dodoma - Mary Athanaz Ndasi – Rukwa
- Mary John Mwanga – Singida
- Mary Kessy – Dar es salaam
- Neema Robert – Simiyu
- Nyachum Haji Ame – Zanzibar
- Pendo Musa – Morogoro
- Santina Mapile – Njombe
- Thereza Kitinga – Mwanza
- Zaituni Shedrack Kalenbi –
Kigoma - Zamda Daniely Mgonganga –
Iringa
Vijana wa Maisha Plus
- Adolph Anacleth – Mwanza
- Agatha Kalesu – Rukwa
- Ally Thabit – Mwanza
- Anastazia John – Mara
- Asumta Mwingira – Dar es salaam
- Ausi Abdul Moyo – Ruvuma
- Bakari Khalid – Shinyanga
- Boniphace Meng’anyi Nyankena –
Dar es salaam - Charles Daniel – Simiyu
- Douglas Said Msalu – Arusha
- Ellymathew Kika – Njombe
- Elizabeth Joachim – Tabora
- Fahamni Kaite Mwadini –
Zanzibar - Farida Ally – Pwani
- Fadhili Isanga – Kilimanjaro
- Flora John – Singida
- Frederick Joseph Ndahani –
Singida - Hyasinta T. Hokororo – Mtwara
- Jane Julio Kalinga – Iringa
- John Sylvester Malima – Geita
- Joyce Jacob Mushy – Arusha
- Marriam Mosses – Shinyanga
- Mary Nicholaus Kavishe –
Manyara - Mbonimpaye N. Nkoronko – Rukwa
- Mohammed Selemani Lipemba -
Lindi - Moureene K. Daud – Kagera
- Nelson Daniel – Dar es salaam
- Ngoma Abdallah – Kigoma
- Osama Norman – Mbeya
- Otilia Selestin Simime – Mbeya
- Said Salum – Katavi
- Salumu Saidi Johari – Mtwara
- Scholastica Deusidedith – Geita
- Seif Mohamed Salum – Tabora
- Shaaban Masoud Shaaban –
Zanzibar - Shida Keneth Mganga – Dodoma
- Shishira G. Mnzava – Morogoro
- Thomas P. Mgazwa – Dodoma
- Yassini Hamisi Suddi – Dar es
salaam - Zaharani Yusuph Hossen – Tanga
BONANZA LA JOGGING & GLOBAL BREAKING NEWS LAFANA NDANI YA DAR LIVE
Washiriki wakimalizia mbio zao kutokea Uwanja wa Taifa mpaka Ukumbi wa taifa wa Burudani wa Dar Live.
Klabu mwenyeji, Kejo Community wakiwa jukwaani wakicheza kwa furaha katika Bonanza hilo.
Msanii wa Msondo Music Band, Hassan Moshi (mwenye Mic) akikosha nyoyo za wana Jogging waliohudhuria kwenye Bonanza la Jogging & Global Breaking News
Timu ya klabu ya Jogging ya Magenge 20 wakipepetana na Spurs (jezi nyeupe) katika mchezo wa pete hatua ya nusu fainali, katika bonanza hilo.
Wacheza drafti John Gwile (kushoto) na Mohamed Abdallah wakichuana kwenye Bonanza la Jogging & Global Breaking News
Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtevu akimpatia cheti cha shukrani Mratibu wa Dar Live, Luqman Maloto kilichotolewa na klabu mwenyeji, Kejo Community.
Mratibu wa Dar Live, Luqman Maloto akionesha cheti cha Heshima kwa Dar Live, kilichotolewa na klabu ya jogging ya Kejo kutoka Temeke.
Msondo Music Band, wakifanya yao jukwaani katika Bonanza la Jogging & Global Breaking News ndani ya Dar Live.
Washiriki kutoka klabu mbalimbali wakiwa tayari kuanza mbio zao kutoka Uwanja wa Taifa kuelekea Ukumbi wa taifa wa Burudani, Dar Live, katika Bonanza la Jogging & Global Breaking News.
Gari la huduma ya kwanza (kushoto) nalo lilikuwepo katika mbio za jogging kwa ajili ya kunusuru wale watakaopata matatizo.
Mkali wa staili ya ‘Mapanga’ kutoka TMK Halisi, Rashid Ziada ‘KR Mulla’ akifuatilia kwa karibu shoo ya Msondo ndani ya Dar Live.
(PICHA ZOTE NA NICODEMUS JONAS / GPL)
LIGI DARAJA LA KWANZA : POLISI MORO WAICHAPA BUKINAFASO
Beki wa Polisi Morogoro Akiangalia Mbinu za Kuondosha hatari zilizokuwa zinaelekezwa langoni kwao.
Polisi Morogoro katika dakika ya 87 baada ya Beki wa Bukina Faso Kujifunga Mpira wa Kona Uliopigwa Vizuri na Nahoda wa Polisi Moro.
Wachezaji waPolisi Morogoro wakishangilia Ushindi wao.
Mshambuliaji wa Bukina Faso Ally Mayuki[kulia] akitafuta mbuni za kumtoka beki wa Polisi Morogoro Teru Ally
Mayuki akifumua shuti baada ya kutoka beki Teru Ally Hata hivyo shuti hilo lilidakwa na kupi wa Polisi Bakari Abdul
Ligi Daraja la Kwanza ilianza Kutimua Vumbi jana Ambapo Katika dimba la uwanja wa Jamhuri Ulipigwa Mchezo wa Kati ya Polisi Morogoro na Bukina Faso ya Morogoro.
Katika Mchezo Huo Uliokuwa na Upinzani Mkalia Ulimalizika kwa Polisi Moro kushinda mabao 3-1
Upinzani mkali ulikuwa kwa timu ya
Burkina faso ambao walianza mchezo huo kwa kasi na kufanikiwa kupa bao
dakika 51 kupitia kwa Said Manga , Dakika 10 za mwisho polisi
waliliandama lango la Burkina faso na kufanikiwa kupata pelnati dakika
81 ambapo Fanuel Simon alipiga Pelnati hiyo kuifundi na kuisawazishia
timu yake.
Hadi 90 za kawaida zilikuwa sare ya bao 1-1 ambapo dakika za nyongeze Polisi Moro Walifanikiwa Kupata Magoli 2
Msama azindua DVD ya kwaya Mtakatifu Benedicto
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Msama Promotion,Alex Msama,(katikati) akizindua Album ya
Dvd ya kwaya ya Mtakatifu Benedicto ya Kanisa la Kathoriki kigogo
Luhanga Jijini Dar es salaam,msama alikuwa mgeni rasmi kwenye tamasha la
uzinduzi wa album hiyo ambapo alichangia Shilingi milioni
1,500,000/kulia ni Mratibu wa tamasha la Pasaka,John Melele,(kushoto)ni
Paroko wa kanisa hilo Father Vitus Sedlmair.
MASHINDANO YA NGUMI YA NELSONI MANDELA OPEN CHAMPIONSHIP YAMALIZIKA KAWE
Bondia Ezira Paul wa Kigoma akipambana na Hafidhi Kassimu wa Ngome wakati wa mashindano ya Nelson Mandela Open CHampion Ship yaliyomalizika kawe Dar es salaam Paur alishinda kwa pointi |
Baadhi ya watu waliofulika kuangalia michuano hiyo |
Meya wa Kinondoni akizungumza wakati wa kufunga mashindano hayo |
Mjumbe wa maendeleo ya wanawake katika mchezo wa masumbwi nchini Aisha Vonialis katikati akiwa na mabondia wa kike waliopigana na kunyakuwa zawadi mbalimbali |
Katika picha ya pamoja
Rais wa Shilikisho la ngumi za Ridhaa Nchini BFT Mutta Rwakatare akimzawadia kocha wa timu ya kawe baada ya kuibuka washindi wa tatu katika mashindano hayo |
WANAMICHEZO WATAKIWA KUJIWEKEA AKIBA
WANAMICHEZO
wametakiwa kuwa na uelewa wa kuanza kujiwekea akiba wangali wakiwa
wadogo, ili kujitengenezea mazingira mazuri ya kuishi pindi
wanapostaafu.
Wito huo umetolewa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Mpango wa uchangiaji wa hiyari (PSS), kutoka Mfuko wa Pensheni kwa watumishi wa Umma (PSPF), Godfrey Ngonyani, wakati wa bonanza la michezo lililowakutanisha wanamichezo na wadau mbalimbali wakiwemo wafanyakazi wa taasisi hiyo kwa lengo la kuhamasisha wanamichezo nchini kujiunga na huduma hiyo kwa manufaa ya baadaye.
“Tumeamua kusambaza na kutangaza huduma zetu kupitia michezo ili kutoa fursa kwa wanamichezo mbalimbali kama ngumi na mpira wa miguu, kwani baadhi yao bado hawajui umuhimu wa kujiwekea akiba pindi wakiwa vijana.
“Tunaamini kupitia PSS, ambao unawalenga zaidi watu wa sekta binafsi kama wanamichezo, elimu hii itaweza kuwafikia na wengi wataweza kutambua umuhimu huo kwani kwa sasa tayari tunamafao sita ya kujiunga, ikiwemo fao la uzeeni, elimu, ulemavu na la kujitoa, ambayo mteja hutakiwa kulipa kwa kila mwezi sh.10,000 au zaidi,”alisema Ngonyani.
Kwa upande wake muandaaji wa bonanza hilo lililojulikana kama ZUGO, Zuwena Kipingu, alisema wanamichezo wa kipindi hiki wanabahati ya kupata elimu ya kujiwekea akiba bure ikilinganishwa na wakipindi cha nyuma.
“Tunawashukuru PSPF kwa kudhamini bonanza hili lakini pia kwa kutupatia elimu ya kujiunga na huduma zao kwani kiukweli wanamichezo wengi huwatunajisahau sana pindi tunapokuwa maarufu bila kujua ipo siku umaarufu utaisha na bila kuwa na akiba yoyote.
“Lakini leo hii tunapata mwanya huu bila gharama zozote, kwahiyo hatuoni sababu ya kuendelea kuishi bila ya kujiwekea akiba kwani katika dunia ya leo maisha bila akiba hamna maana,”alisema.
Wito huo umetolewa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Mpango wa uchangiaji wa hiyari (PSS), kutoka Mfuko wa Pensheni kwa watumishi wa Umma (PSPF), Godfrey Ngonyani, wakati wa bonanza la michezo lililowakutanisha wanamichezo na wadau mbalimbali wakiwemo wafanyakazi wa taasisi hiyo kwa lengo la kuhamasisha wanamichezo nchini kujiunga na huduma hiyo kwa manufaa ya baadaye.
“Tumeamua kusambaza na kutangaza huduma zetu kupitia michezo ili kutoa fursa kwa wanamichezo mbalimbali kama ngumi na mpira wa miguu, kwani baadhi yao bado hawajui umuhimu wa kujiwekea akiba pindi wakiwa vijana.
“Tunaamini kupitia PSS, ambao unawalenga zaidi watu wa sekta binafsi kama wanamichezo, elimu hii itaweza kuwafikia na wengi wataweza kutambua umuhimu huo kwani kwa sasa tayari tunamafao sita ya kujiunga, ikiwemo fao la uzeeni, elimu, ulemavu na la kujitoa, ambayo mteja hutakiwa kulipa kwa kila mwezi sh.10,000 au zaidi,”alisema Ngonyani.
Kwa upande wake muandaaji wa bonanza hilo lililojulikana kama ZUGO, Zuwena Kipingu, alisema wanamichezo wa kipindi hiki wanabahati ya kupata elimu ya kujiwekea akiba bure ikilinganishwa na wakipindi cha nyuma.
“Tunawashukuru PSPF kwa kudhamini bonanza hili lakini pia kwa kutupatia elimu ya kujiunga na huduma zao kwani kiukweli wanamichezo wengi huwatunajisahau sana pindi tunapokuwa maarufu bila kujua ipo siku umaarufu utaisha na bila kuwa na akiba yoyote.
“Lakini leo hii tunapata mwanya huu bila gharama zozote, kwahiyo hatuoni sababu ya kuendelea kuishi bila ya kujiwekea akiba kwani katika dunia ya leo maisha bila akiba hamna maana,”alisema.
No comments:
Post a Comment