Askari wa Kikosi Maalum cha Kutuliza Ghasia Magerezani (KMKGM) cha Ukonga jijini Dar es salaam wakionesha aina mbalimbali za mzoezi ya kujihami na kuanguka bila kuumia katika kukabiliana na hatari yoyote, mblele ya Kamishna wa Magereza nchini Zambia Percy Chato (hayupo pichani)
Kamishna wa Magereza nchini Zambia yuko katika ziara ya siku sita nchini kufuatia mwaliko uliotolewa kwake na Kamishna Jenerali wa Magereza wa Tanzania John Minja mwezi Septemba mwaka, 2013 alipotembelea Magereza nchini Zambia. Ziara ya Kamishna Percy pamoja na maafisa wengine watatu ni kudumisha ushirikiano uliopo kwa muda mrefu baina ya nchi hizi mbili na magereza kwa ujumla. Akiwa nchini Tanzania Kamishna Percy atatembelea baadhi ya Magereza na Vyuo vya Mkoa wa Dare es salaam, Kilimanjaro na Arusha ili kujionea shughuli za urekebishaji wa wafungwa zinavyofanywa kwa vitendo na kuona maeneo ambayo taasisi hizi mbili zinaweza kubadilishana uzoefu.
======================================================
KAMATI KUU YATEUA MGOMBEA WA CCM KALENGA
==================================
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimtambulisha kwa waandishi wa habari, mgombea wa Ubunge katika uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga, Iringa, Godfrey William Mgimwa (kushoto), leo, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Nape amemtambulisha Godfrey ambaye ni mtoto wa Marehemu Dk. William Mgimwa, baada ya Kamati Kuu ya CCM kumpitisha, leo kuwania nafasi hiyo ya Ubunge.
=============================================================
MAGEREZA YAZINDUA DUKA LA “DUTY FREE SHOP” – RUANDA, MBEYA
===================================
Mpango huu wa ujenzi wa Magereza “Duty Free Shops” katika Mikoa ya Kimagereza Kiutawala unatekelezwa kwa Mafanikio makubwa na Uongozi wa Jeshi la Magereza unaosimamiwa kimkakati na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja hivyo kutimiza adhima ya Serikali ya Awamu ya Nne ya kuwasogezea huduma za bidhaa muhimu na zenye manufaa Maafisa, Askari wa Jeshi la Magereza pamoja na familia zao katika maeneo yao ya kazi.
Aidha, mpaka sasa jumla ya “Duty Free Shops” tano (05) zimezinduliwa sehemu mbalimbali hapa nchini hususani katika Mikoa ya Dar es Salaam(Ukonga), Dodoma(Gereza Isanga), Morogoro(Chuo cha Ufundi na Udereva Kingolwira), Kilimanjaro(Gereza Karanga, Moshi) na Mwanza(Gereza Butimba).
Kuzinduliwa kwa Magereza “Duty Free Shop” – Ruanda, Mbeya kunafanya idadi yake kuongezeka na kufikia jumla ya Magereza “Duty Free Shop” sita(06) ambazo zimekamilika hapa Nchini katika Mikoa ya Kimagereza Kiutawala.
Vyombo vya Habari ikiwa wadau muhimu katika dhima ya kuuhabarisha umma vinakaribishwa kwenye tukio la uzinduzi rasmi wa Magereza “Duty Free Shop” – Ruanda, Mbeya kesho Februari 12, 2014 kuanzia saa 3:30 asbuhi katika Viwanja vya Ofisi za Magereza Mkoa wa Mbeya.
=============================================================
Mabingwa Airtel Rising Stars wasichana wajazwa noti
==================================
Timu hiyo ilitwaa taji hilo baada ya kuifunga Kenya bao 1-0 lililofungwa na Donisia Daniel katika fainali hiyo.
Akipokea
fedha hizo jana (Februari 10, 2014) Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu
Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Msanifu Kondo alisema wanaishukuru Kampuni
ya Airtel kwa kutimiza ahadi yao ya zawadi ya fedha hizo na tayari
wamezikabidhi kwa makocha na wachezaji wa timu hiyo.
Alisema
kila mchezaji amepewa Sh 850,000 wakati kocha mkuu wa timu hiyo
Rogasian Kaijage amepewa Sh milioni moja na laki mbili na kocha msaidizi
amepewa Sh milioni moja.
“Tunawashukuru Airtel kwa kutoa fedha hizo za zawadi kwa timu hii na sisi tumewakabidhi wahusika,” alisema.
Kwa
upande wake Afisa Uhusiano wa Airtel Tanzania Jane Matinde alisema wao
kama wadhamini wa mashindano hayo wametimiza ahadi yao kwa kukabidhi
fedha hizo kwa mabingwa hao.
“Kwa
niaba ya Airtel Tanzania tunaipongeza timu ya wasichana ya Tanzania kwa
kutwaa ubingwa huo, lakini pia tumetekeleza ahadi yetu ya kukabidhi
zawadi, kama mnavyofahamu kampuni yetu imekuwa mstari wa mbele katika
kusaidia mambo ya kijamii lakini pia michezo ikiwemo soka kupitia
michuano ya vijana ya Airtel Rising Stars kwa kushiriki na klabu ya
Manchester United,” alisema.
No comments:
Post a Comment