WADAU WAOMBWA KUJITOKEZA KUDHAMINI
Pichani wa tatu kulia ni Mkurugenzi wa Habari na Matukio wa Kampuni ya Angels Moment ya
jiji Dar,akizungumza mbele ya Wanahabari (hawapo pichani) mapema leo
kwenye moja ya ukumbi wa mikutano ya Serena Hotel,kuhusiana tamasha la
kwanza na
la aina yake kufanyika nchini Tanzania, lenye lengo la kuongeza na
kuchochea uelewa wa wanawake katika kuchangamkia fursa mbalimbali za
kujiwekea akiba.
“Tamasha
hili limeandaliwa ili kuwaonesha wanawake na vijana umuhimu wa kuweka
akiba, aina tofauti za kuweka akiba na njia mbalimbali za kuweka akiba
pamoja na fursa za kuweka akiba kimkakati kupitia uwasilishaji wa mada
na maonesho,” alisema Bi Pamela. Pichani kulia ni Meneja Mawasiliano wa kampuni ya Angels Moment,Bi.Beatrice Millinga,Mratibu
wa Matangazo na Mahusiano kutoka kampuni ya
AZAM/Bakharessa,Bwa.Mohameda Ramadhani (Mdhamini wa tamasha hilo),pamoja
na mwisho kushoto ni Mratibu wa tamasha hilo kutoka kampuni ya MONTAGE
LTD,Bi,Teddy Mapunda.
Pichani ni baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Angels Moment ya jiji Dar wakiwa katika picha ya pamoja,mara baada ya mkutano kumalizika.
==========================================================
WADAU WAOMBWA KUJITOKEZA KUDHAMINI TAMASHA LA KWANZA LA KIPEKEE LA KUWAWEZESHA WANAWAKE NA VIJANA KUFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM
Na Beatrice Millinga
Kampuni
ya Angels Moment ya jijini Dar es Salaam imetoa wito kwa wadau
wanaojihusisha na shughuli mbalimbali za kimaendeleo kujitokeza na
kudhamini tamasha la kwanza la kipekee kwa ajili ya wanawake na vijana
lililopewa jina la Mwanamke na Akiba na linalotarajiwa kufanyika kuanzia
Februari 19 - 21, 2014 kwenye Ukumbi wa Dar Live - Mbagala, jijini Dar
es Salaam.
Akizungumza
na waandishi wa wahabari katika ukumbi wa Serena leo, Mkurugenzi wa
Habari na Matukio wa Kampuni ya hiyo, Bibi Pamela David amesema kuwa
makampuni na mashirika mbalimbali yatapata fursa ya kujitangaza, na
kutangaza bidhaa na huduma zao, kwa lengo la kuongeza ufahamu wa bidhaa
zao kwa wanawake na vijana wa Kitanzania.
“Kwa
kudhamini Tamasha hili wadau watapata sio tu fursa ya kutangaza
biashara na huduma zao bali kujitangaza wao wenyewe na kutoa elimu kwa
umma maana si wananchi wote wanauelewa wa huduma zitolewazo na mashirika
na makampuni mbalimbali hapa nchini,” alisema Bi Pamela.
Kwa
mujibu wa Bi Pamela, Tamasha hilo ni la kwanza na la aina yake
kufanyika nchini Tanzania lenye lengo la kuongeza na kuchochea uelewa wa
wanawake katika kuchangamkia fursa mbalimbali za kujiwekea akiba.
“Tamasha
hili limeandaliwa ili kuwaonesha wanawake na vijana umuhimu wa kuweka
akiba, aina tofauti za kuweka akiba na njia mbalimbali za kuweka akiba
pamoja na fursa za kuweka akiba kimkakati kupitia uwasilishaji wa mada
na maonesho,” alisema Bi Pamela.
Aliongeza
kuwa washiriki watapata fursa ya kupata elimu juu ya kukabiliana na
hatari katika uhifadhi wa fedha na masuala mbalimbali yahusikanayo na
usimamizi wa fedha.
Akizungumza
mfumo utakaotumika kuendesha tamasha hilo, msemaji wa kampuni, Bi
Pamela alisema “Tamasha litakuwa kwenye mfumo wa maonesho pamoja na
vipindi vinne vya uwasilishaji wa mada mbalimbali toka kwa wanawake
wafanyabiashara waliofanikiwa na wataalamu waliobobea kwenye nyanja
hizo.
Kwa
mujibu wa msemaji huyo watoa mada wanaotarajiwa kuwasilisha ni pamoja
na Naibu Gavana Mkuu wa Benki Kuu ya Tanzania, Dkt. Natu Mwamba na
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko Ya
Hifadhi ya Jamii (SSRA) Bibi Irene Isaka.
Tamasha
linatarajia kuwavutia washiriki 5,000 na waonyesha bidhaa 50 kutoka
maeneo mbalimbali katika sekta ya usimamizi wa fedha. Pia, inatarajiwa
kuvutia washiriki toka sekta nyingine ikiwemo biashara zenye mahusiano
na suala zima la uhifadhi wa fedha na uwekaji wa akiba kwa wanawake.
Mgeni rasmi wa Tamasha hili anategemewa kuwa Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal.
Mualiko
wa Mama Asha kwenye Tamasha hili unachagizwa na ujasiri na mchango
wake, pamoja na kujitoa kwake kwa hali na mali katika kusaidia wanawake,
vijana na makundi mbali mbali yenye uhitaji nchini Tanzania.
Tamasha
limedhaminiwa na Said Salim Bakhresa (SSB), Shirika la Hifadhi ya Jamii
(NSSF), Benki ya CRDB, STANBIC, FINCA, Mamlaka ya Usimamizi na
Udhibiti wa Mifuko Ya Hifadhi ya Jamii (SSRA). Wadhamini wengine ni
pamoja na Mfuko wa UTT, Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Mfuko wa
Pensheni kwa Mashirika ya Umma (PPF) na Kampuni ya Ashton Media.
No comments:
Post a Comment