WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema Serikali imepanga kuajiri walimu
zaidi ya 35,000 kwa ajili ya shule za sekondari ili kukabiliana na
tatizo la uhaba wa walimu nchini.
tatizo la uhaba wa walimu nchini.
Ametoa kauli hiyo jana jioni (Alhamisi, Februari 19, 2015) wakati
akizungumza na mamia ya wakazi wa kata ya Kiwere, mara baada ya
kukagua ujenzi wa maabara na kuzindua nyumba nne za walimu kwenye
shule ya sekondari ya Kiwere, tarafa ya Kalenga, wilayani Iringa.
Waziri Mkuu alisema walimu hao watagawanywa kwenye shule kulingana na mahitaji yaliyokwishawasilishwa na kwamba watakapopata mgao wao hawana budi kuziangalia kwanza shule zenye miundombinu iliyokamilika kama ilivyo kwa shule hiyo.