Kuhusiana
na mwanariadha Oscar Pistorius aliyeko kifungoni, imeelezwa kwamba sasa
anaweza ama kuruhusiwa kukumbatiana na wageni wake na hata kuwabusu
wanaomtembelea ,anaruhusiwa kusikiliza redio na hata kuvaa vitu vya
thamani ikiwemo vito vya thamani akiwa ndani ya gereza.
Mtuhumiwa
huyo wa mauaji,amepewa ruhusa ingine ya kuwa huru kupiga simu
atakavyo,vile vile bajeti yake inayodaiwa kuwa kubwa, imekubaliwa aweze
kununua vyoo atakavyo na hata akitaka chipsi ataletewa,na huu ni uamuzi
wa bwana jela anaye angalia wafungwa na hadhi zao naye Pistorius yuko
kundi B.
Ikumbukwe kwamba Oscar alimuua mpenzi wake mnamo mwezi
kama huu na siku inayotajwa kuwa muhimu ulimwenguni tarehe ya kumi na
nne Valentine's Day,mwaka wa jana akiwa nyumbani kwake.
Akiwa jela
Pistorius anajaribu kuyazoea mazingira ya jela na inamuwia vigumu
kukubali kuwa ameupoteza uhuru wake, na pia kuonekana kama tishio la
usalama na hivyo yumo ndani
Msemaji wa familia ya Pistorius
mwanamama,Annalise Burgess, amemzungumzia mwanariadha huyo aliyekuwa
maarufu duniani kiasi cha kupachikwa jina la Blade Runner,sasa
amepandishwa hadhi na kuwa daraja la A .
Familia ya Oscar ina
Whatsapp la familia yao ambalo linafuatilia taarifa zote za mwanariadha
huyo na pia hutumia akaunti hiyo kujadiliana masuala ya biashara za
familia.
Inaelezwa kuwa watu wanaoongoza kumtembelea Oscar
Pistorius Jela ni kaka na dadake Aimee Carl na wakiisha kuonana naye
hutuma taarifa na picha katika kundi hilo na kinachoendelea kumhusu yeye
gerezani.
Kupandishwa kwa Oscar kuna maanisha kuwa anaruhusiwa
kutembelewa na wageni zaidi ikiwemo familia yake.Hapo mwanzo kila
anayemtembelea huzungumza naye kwa njia ya simu akiwa ametengwa na mgeni
wake na vioo, na hakuruhusiwi kuguswa,lakini mambo sasa yamebadilika.
Sasa
Oscar mwenye umri wa miaka ishirini na nane, anaweza kuwakumbatia jamaa
zake wamtembeleapo,na muda wa kumuona umeongezwa kutoka saa mbili hadi
tatu kwa mwezi,na wageni wamtembeleao bado wanakabiliwa na sheria ya
kupekuliwa kabla ya kuonana ma mfungwa huyo ambaye bado anatakiwa kuvaa
sare za jela zenye rangi ya samawati ama ita orange
No comments:
Post a Comment