Mkurugenzi wa Mradi wa “AIDS free”, Bw. Samson Kironde(wa pili kushoto)
akitoa maelezo mafupi namna mradi huo utakaotekelezwa ndani ya Jeshi la
Magereza na Polisi katika mazungumzo rasmi yaliyofanyika Ofsini kwa
Kamishna Jenerali wa Magereza leo februari 20, 2015(wa pili kulia) ni
Mkurugenzi wa Operesheni na Fedha, Bw. Mike Hames(wa kwanza kushoto) ni
Afisa Mwandamizi anayeshughulikia masuala ya UKIMWI kutoka USAID, Bw.
Erick Mlang’ha. Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akisisitiza jambo
katika mazungumzo rasmi yaliyofanyika Ofsini kwake leo februari 20, 2015
kati ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza, Polisi na Wasimamizi
Wakuu wa Mradi wa “AIDS – free” utakaotekelezwa ndani ya Jeshi la
Magereza.
Baadhi
ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza walioshriki katika
mazungumzo rasmi kuhusu Mradi wa “AIDS – free” unaotarajiwa kutekelezwa
ndani ya Jeshi la Magereza(wa kwanza kulia) ni Kamishna Huduma za
Urekebishaji, Deonice Chamulesile(wa pili kulia) ni Kamishna wa Sheria
na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa pili kushoto) ni Kamishna
Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Gedion Nkana(wa kwanza kushoto) ni
Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Nsajigwa Mwakenja. Maofisa
Wasimamizi wa Sekta ya Afya kutoka Jeshi la Polisi wakifuatilia
mazungumzo rasmi kuhusu Mradi wa “AIDS – free”(wa kwanza kushoto) ni
Dkt. Nyanda Lushina(katikati) ni Mrakibu wa Polisi, Husein Yahya.
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(meza kuu) akiongoza
mazungumzo rasmi yaliyofanyika Ofsini kwake leo februari 20, 2015 kati
ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza na Wasimamizi Wakuu wa Mradi
wa “AIDS – free” utakaotekelezwa ndani ya Jeshi la Magereza(Picha zote
na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
No comments:
Post a Comment