Ofisa
Mratibu wa Shughuli za Uchaguzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu
(LHRC), Hamis Mkinde (kushoto), akisisitiza jambo wakati akizyungumza na
waandishi wa habari Dar es Salaam, leo, kuhusu Mtandao wa Asasi za
Kiraia wa kuangalia Chaguzi Tanzania (Tacceo) kutuma waangalizi 160
nchi nzima kwa ajili ya kuangalia uandikishaji wapiga kura kwa kutumia
mfumo mpya wa BVR katika wilaya zote za Tanzania Bara. Kulia ni
Mwenyekiti wa mtandao huo, Martina Kabisama.
……………………………………………….
Na Dotto Mwaibale
MTANDAO
wa Asasi za Kiraia wa kuangalia Chaguzi Tanzania (Tacceo) unategemea
kutuma waangalizi 160 nchi nzima kwa ajili ya kuangalia uandikishaji
wapiga kura kwa kutumia mfumo mpya wa BVR katika wilaya zote za Tanzania
Bara.
Hayo
yalibainishwa na Mwenyekiti wa TACCEO Martina Kabisama wakati
akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu uangalizi wa
uandikishaji wapiga kura kwa mfumo wa teknolojia ya alama (BVR),
unaotarajia kuanza Februari 23, 2015 mkoani Njombe na kuendelea nchi
nzima.
“Tunapenda
kutamka kuwa lengo kuu la uangalizi tunaotarajia kuufanya ni kuanisha
mambo chanya na mapungufu yanayoweza kujitokeza wakati wa mchakato wa
uandikishaji wapiga kura unaotarajiwa kuendeshwa na Tume ya Taifa ya
Uchaguzi ili kuweza kushauri namna ya kuboresha Daftari la Kudumu la
Wapiga kura kwa ajili ya kura ya maoni na uchaguzi mkuu utakaofanyika
Oktoba mwaka huu na chaguzi zingine zitakazofuata” alisema Kabisama.
Alisema
lengo lingine ni kuona kuwa mapungufu yote yanafanyiwa kazi na
yanarekebishwa mapema ili uchaguzi ujao uwe bora na wenye tija na
manufaa kwa watanzania wote.
Alisema
madhumuni makubwa ya uangalizi huo ni mchakato mzima na ushirikiashwaji
wa wananchi wa kujiandikisha wa upigaji kura, kushuhudia ni jinsi gani
mfumo wa sheria ya uchaguzi unavyomtambua na kumpa fursa mwananchi
kujiandikisha katika daftari la kudumu la Mpiga kura.
Alitaja
madhumini mengine kuwa ni makundi mbalimbali yakiwemo ya walemavu na
yale yaishio pembezo yanavyoshirikishwa katika jambo hilo ikiwemo elimu
ya uraia pamoja na kutathmin utendaji kazi wa mashine za BVR na
mengineyo.
Kabisama
alisema mtandao huo unatumia fursa hiyo kueleza kuwa hauridhishwi jinsi
mchakato wa uandikishaji wapiga unavyokwenda kwa kusuasua na kukosa
uwazi jambo ambalo ni hatari kwa mustakabali wa Taifa letu.
No comments:
Post a Comment