TAARIFA KWA UMMA
Bodi ya Filamu na Michezo ya
Kuigiza Tanzania inawaagiza Wamiliki wote wa kumbi za filamu Tanzania
Bara kutofanya maonesho ya hadhara ya filamu yenye jina la FIFTY SHADES
OF GREY inayoongozwa na Sam Taylor Johnson na kutengenezwa na Michael De
Luka, Dana Brunetti na E.L. James.
Hatua hiyo imechukuliwa baada ya Bodi ya Filamu na Michezo ya
Kuigiza Tanzania kukagua filamu hiyo yenye urefu wa saa 2:05 na kugundua
kwamba haizingatii sheria na kanuni zinazosimamia tasnia ya filamu
nchini. Maamuzi haya yamefanywa kulingana na ukiukwaji wa Sheria ya
Filamu na Michezo ya Kuigiza Na. 4 ya mwaka 1976 kifungu cha 15 (i) na
kifungu 18(i na ii) ambayo ufafanuzi wa utekelezaji wake uko katika
Kanununi za Sheria hiyo Kifungu cha 24 vifungu vidogo vya a,b,d,e,n na
t.
Filamu ya FIFTY SHADES OF GREY hairuhusiwi kuonyeshwa popote
Tanzania. Aidha, Bodi ya Filamu na Michezo ya Kuigiza Tanzania
inawakumbusha kwa mujibu wa Sheria tajwa hapo juu Wamiliki wote wa kumbi
za sinema na maeneo yote ya kuonyeshea filamu kuwasilisha filamu katika
Bodi hiyo ili zikaguliwe na kupangiwa daraja kabla hazijaanza
kuonyeshwa na kutofanya hivyo ni ukiukwaji wa sheria.
Pia uzinduzi wowote wa filamu unaofanywa katika kumbi za sinema
na maeneo yoyote ya kuonyeshea filamu ni lazima uwe na kibari kutoka
Bodi ya Ukaguzi wa Filamu na Michezo ya Kuigiza.
No comments:
Post a Comment