Na Mwandishi Wetu
IDADI ya mikoa ambayo imeomba iandae onesho la miaka 15 ya Tamasha la Pasaka sasa imefikia 17, waandaaji wamesema.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo
vya habari jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la
Pasaka, Alex Msama ilisema kuwa idadi hiyo ni kubwa na haijawahi kutokea
tangu walipoanzisha tamasha lao mwaka 2000.
“Tumepokea maombi ya wadau
kutoka mikoa 17 wakitaka tupeleke Tamasha la Pasaka mikoani kwao.
Tunachofanya kwenye kamati yangu ni kupokea maoni kwa njia mbalimbali
kwa wadau wetu wa huko.
“Lakini si kupendekezwa au
kuombwa tu na wadau ndiyo kigezo cha kupewa nafasi, lazima tuangalie na
mazingira ya mkoa husika katika mambo ya matamasha,” alisema Msama.
Aliitaja mikoa hiyo kuwa ni
Morogoro, Rukwa, Mara, Singida, Arusha, Ruvuma, Mbeya, Iringa, Tanga,
Dar s Salaam, Mtwara, Mwanza, Dodoma, Tabora, Shinyanga, Kilimanjaro na
Zanzibar.
Alisema kamati yake inatarajia
kukutana Jumatano wiki hii na kufanya tathmini ya maombi kwa wadau wao
wa maeneo hayo ili kupata mikoa sahihi ambayo tamasha hilo litafanyika
mwaka huu.
Tamasha la Pasaka linaandaliwa
na Kampuni ya Msama Promotion ya jijini Dar es Salaam, ambayo pia
huandaa Tamasha la Krismas kila mwaka, lakini wanataka Tamasha la Pasaka
mwaka huu liwe bora zaidi kwa sababu wanasherehekea miaka 15 tangu
waanzishe tamasha hilo.
No comments:
Post a Comment