Naibu
Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Bi Hindi Hamadi
Khamis katikati akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Zanzibar wa Abeid
Karume akisubiri kuwasili kwa Wajasiriamali, Wasanii na Waandishi wa
Habari waliokuwa nchini Oman kwa ajili ya maonyesho ya Tamasha la
Utamaduni yaliyofanyika nchini humo. (Picha na Miza Othman Maelezo,
Zanzibar)
Wajasiriamali,
Wasanii na Waandishi wa Habari waliopata nafasi yakwenda Oman kwa ajili
ya kuutangaza Utamaduni wao wakipokelewa na Naibu Waziri wa Habari
Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar. (Picha na Miza Othman Maelezo,
Zanzibar)
Naibu
Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Bi Hindi Hamadi
wa mwanzo kulia akiwasalimia wasanii hao baada ya kuwasili uwanjani
hapo. (Picha na Miza Othman Maelezo, Zanzibar)
Baadhi
ya Waandishi wa Habari wakimuhoji mmoja kati ya Wasanii waliyopata
bahati ya kwenda nchini Oman kwa ajili ya maonyesho hayo.
(Picha na Miza Othman Maelezo, Zanzibar)
…………………………………………………………………
Na Ali Issa Maelezo-Zanzibar
Wasanii na Wajasiriamali kutoka Zanzibar waliokuwa wakishiriki
Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Ujasiriamali yaliyokuwa
yakifanyika nchini Oman hatimaye wamerudi Salama nchini.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Bi
Hindi Khamis Hamad ndio kiongozi wa Serikali aliyekuja kuwapokea baada
ya kumaliza safari yao ya mwezi mmoja nchini humo.
Akizungumza na Waandishi wa habari Uwanja wa ndege wa kimatifa
wa Abeid Karume mara baada ya kuwasili Mkuu wa Msafara huo Khadija
Battashy amesema safari ilikuwa na mafanikio makubwa sana kwa Zanzibar
na Tanzania kwa ujumla kutokana na kuitangaza vyema nchi yao.
Amesema Wasanii hao waliweza kutumia vyema Vipaji vyao na kuweza
kuwavutia Watazamaji na watu mbalimbali waliofika katika Maonesho hayo.
Bi Khadija ameongeza kuwa fursa ambayo waliipata ni muhimu na
kwamba itaisadia Tanzania katika Sekta mbalimbali hasa biashara na
Utalii.
Amesema wamebaini kuwa Biashara ya Viuongo inakubalika sana na
kwamba Wajasiriamali walioenda kufanya bishara hiyo walifanikiwa vyema
katika bishara yao.
Kuhusu biashara ya Mavazi Bikhadija amesema ilikuwa na
changamoto kwao kutokana na Nguo walizopeleka kuwa Fupi jambo ambalo
liliwapa shida kuuza nguo hizo.
Hata hivyo Bikhadija amesema Changamoto hiyo wataifanyia kazi na
pale yatakapotokea Maonesho mengine Wataenda na Nguo ndefu ambazo
zinapendwa sana kulingana na Utamaduni wa Watu wa Oman.
Kwa upande wa Sekta ya Utalii Bi Khadija amesema Wanamatarajio
makubwa kwamba kiwango cha Watalii kinaweza kuongezeka kupitia Vivutio
mbalimbali vilivyomo nchini walivyovionesha katika Maonesho hayo.
Ameongeza kuwa wapo Watu wengi kutoka nchi tofauti ambao
wamevutiwa na hatimaye kujisajili kuja Tanzania kwa ajili ya Utalii
katika Mbuga za wanyama, Mlima Kilimanjaro na Zanzibar.
Akizungumzia kuhusu Wasanii walioenda kutumbuiza katika Tamasha
hilo Bi Khadija amesema kazi walioifanya ilikuwa ya kupigiwa mfano
kutokana na Ngoma za Asili ya Zanzibar kuwavutia wengi katika Tamasha
hilo.
Katika Msafara huo Jumla ya Watu 42 kutoka Tanzania Bara na
Zanzibar waliiwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzani katika Maonesho
hayo yaliyodumu kwa muda wa mwezi mmoja ambapo nchi mbali mbali Duniani
ziliweza kuonesha Vivutio na Kazi za Sanaa za Wananchi wake.
No comments:
Post a Comment