Na Mwandishi Wetu
MSAMA Promotion kwa mara
nyingine tena imeandaa Tamasha kubwa la nyimbo za kumsifu Mungu
litakalofanyika wakati wa sikukuu ya Pasaka katika mikoa tofauti hapa
nchini.
Mwenyekiti wa Kamati ya
Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama anasema kwamba tamasha hilo
mwaka huu litakuwa na utofauti mkubwa ukilinganisha na matamasha mengine
yaliyopita, kwani limeboreshwa zaidi na watakuwa wanafurahia miaka 15
tangu lianzishwe.
“Kwanza kabisa tofauti na
matamasha yaliyopita, mwaka huu tutakuwa na waimbaji wengi zaidi wa
muziki wa Injili kutoka nchi za nje.
“Kutakuwa na waimbiaji kutoka
Kenya, Zambia, Afrika Kusini, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo
(DRC) na nje ya Afrika, ambapo lengo kubwa ni kulifanya tamasha hili
kuwa na utofauti,” anasema.
Moja ya maboresho makuwa katika
miaka 15 ya Tamasha la Pasaka la mwaka huu Msama amesema kwamba litakuwa
na kiingilio rahisi zaidi ili kila mmoja aweze kuhudhuria na kupata
baraka kutoka kwa waimbaji hao wanaomsifu Mungu.
“Waimbaji wote maafuru wa muziki
wa Injili watakuwepo, kwani tumejipanga vizuri mno kuhakiksha kwamba
tamasha hili litakuwa gumzo kila mahali,” anasema.
Anasema kutokana na ukumbwa na
maboresho mazuri zaidi ya tamasha hilo, kamati ya maandalizi
imewashirikisha watu 100, wakiwa ni wachungaji na Wainjilisti.
Anasema lengo kubwa la kuwashirikisha wachungaji na Wainjilisti ni kwa sababu watu wengi waweze kubarikiwa kiroho kwa kuwa tamasha hilo ni la kumsifu Mungu.
“Wapendwa wajiandae kushiriki kwa wingi kwani watashiba kiroho kutokana na kuwa na waimbaji wengi wenye hamasa ya kiroho.
“Tutaheshimu mno maoni ya
wapenzi wa tamasha hili kutoka sehemu mbalimbali na kila
watakalotushauri tutalifanyia kazi, lengo kubwa lilikuwa n kiboresha
tamasha letu,” anasema.
Mwaka huu Tamasha la Pasaka
linatimiza miaka 15 tangu kuasisiwa kwake na Kampuni ya Msama Promotions
ya jijini Dar es Salaam na limekuwa likijiongezea umaarufu na
kukubalika zaidi kutokana na ubunifu wake wa kufanya maadhimisho ya
Sikukuu za Pasaka na Krismasi kwa umahiri na mguso wa kiroho kupitia
matamasha hayo.
Umaarufu wa matamasha hayo
pamoja na mambo mengine, unatokana na ukweli kuwa yamekuwa yakifanyika
kwa ubunifu na umakini mkubwa huku kila mwaka yakiongezeka na kubadili
waimbaji mbalimbali wa nyimbo za Injili wa ndani na nje ya nchi.
Baadhi ya nyota waliowahi
kutumbuiza katika matamasha hayo ni marehemu Angela Chibalonza kutoka
Kenya, ambaye naye aliwahi kutikisa.Baadhi ya nyimbo zake zilizotikisa
na kukonga nyoyo ni Yahwe Uhimidiwe na Uliniumba Nikuabudu.
Wengine walioweka historia
nchini ni pamoja na Solly Mahlangu kutoka Afrika Kusini. Mwimbaji huyo
alivunja rekodi ya waimbaji wote licha ya kuwa hafahamu lugha ya
Kiswahili vilivyo, lakini aliweza kuimba nyimbo kadhaa za Kiswahili kama
Mwambamwamba ili kwenda sawa na Watanzania aliokonga nyoyo zao kwa
kuwapa neno la Mungu kupitia muziki wa Injili.
Sipho Makhabane, Rebeka Malope
nao kwa nyakati tofauti, walifanya vizuri ukiachilia mbali waimbaji
wengine kama Ephraim Sekeleti kutoka Zambia, Ambassadors of Christ
(Rwanda), Faraja Ntaboba na Solomoni Mukubwa (Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo), 24 Elders (Uganda) na Anastazia Mukabwa (Kenya).
Rebecca amewahi kutamba na
albamu za Saturday Nite (aliyoitoa Januari 1, 2009), Hlala Nami (Novemba
11, 2003), Siyabonga (Desemba 21, 2000), Free at Last (Novemba 18,
1997), African Classics (Mei 5, 2009) na Greatest Hits (Januari 10,
2006).
Kwa upande wa Mukubwa ambate
ametamba sana na wimbo wa Mfalme wa Amani amepata kutamba katika tamasha
hilo na albamu mbalimbali ikiwemo ya Usikate Tamaa yenye nyimbo kama
Mungu Wangu Nitetee, Niko na Yesu, Mke Si Nguo, Usikate Tamaa, Moyo
Tukuza Bwana, Chunga Ahadi Yako na Yesu Jina Zuri.Pia ana albamu
nyingine mbili ambazo ni Sijaona Rafiki na Mungu Mwenye Nguvu.
Sijaona Rafiki Kama Yesu ambayo ni albamu yake ya kwanza ina nyimbo za
Uwe Nami Bwana, Sijaona Rafiki Kama Yesu, Nitayainua Macho, Matendo ya
Mungu, Bwana Wastahili na Yesu Kimbilio. Albamu yake ya
pili ya Mungu Mwenye Nguvu ina nyimbo za Mungu Mwenye Nguvu, Mkono wa
Bwana, Mfalme wa Amani, Siku Moja, Tabia Ina Dawa na Roho Yangu
Ikuimbie.
Pia yupo msanii, Solly
Mahlangu ‘Obrigado’ wa Afrika Kusini ambaye ingawa alitumbuiza Tamasha
la Krismasi, lakini amekuwa na mvuto mkubwa kwa mashabiki.
Mahlangu ni
muimbaji ambaye anashika kasi katika anga ya muziki wa Injili Afrika
ambaye pia anamudu kuimba Kiswahili kizuri kwa baadhi ya nyimbo zake.
Mbali ya kuwa
maarufu katika nyimbo za Iinjili nchini mwake, pia ni Mchungaji ambaye
ana uwezo wa kufanikisha muziki wa Injili na kanisa lake ambalo ni Word
Praise Christian Centre Intenational lililoko Tembisa.
No comments:
Post a Comment