Ujumbe
wa Waziri wa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa
William Lukuvi umemaliza ziara yake nchini Singapore huku ukiwa
umejifunza mambo muhimu ikiwemo kuwepo utawala wa sheria katika
usimamizi wa ardhi, kutokuwepo rushwa, nidhamu na uaminifu mkubwa wa
watumishi wa umma, jamii inayopenda kujitegemea na usalama wa hali ya
juu. Yafuatayo ni matukio ya ziara hiyo kwenye Mamlaka ya Uendelezaji wa
Mji wa Singapore(URA) kama yalivyoratibiwa na Muungano Saguya. Ujumbe
wa NHC ulipokutana na baadhi ya wawekezaji wakubwa wa sekta ya
uendelezaji Miliki wa Singapore ili kuwahamasisha kuwekeza vitega uchumi
vya hoteli nchini Tanzania. Ujumbe huu umekutana na Bw. Henry Ngo
ambaye ni Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bonvest na Hoteli ya
Sheraton Singapore ambao pia wamewekeza Zanzibar Hoteli ya Kitalii.
Ujumbe
wa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa William
Vangimembe Lukuvi ukiwa katika Mamlaka ya Uendelezaji wa nchi ya
Singapore(Urban Redevelopment Authority –URA) kujionea namna mamlaka
hiyo inavyoratibu ukuaji wa sekta ya nyumba kwa kuweka mipango madhubuti
ya matumizi bora ya ardhi kulingana na mahitaji ya Taifa hilo
linalotegemea zaidi utalii.
Mchoro
unaoonyesha ramani ya nchi ya Singapore ulioko Makao Makuu ya Mamlaka
ya Uendelezaji nchi hiyo ukionyesha majengo mbalimbali yaliyoko katika
nchi hiyo yenye uhaba mkubwa wa ardhi.
Ujumbe
wa Tanzania ukiangalia ramani yenye matumizi mbalimbali yaliyotengwa
kwenye ardhi ya Taifa la Singapore. Katika nchi hiyo hakuna uwezekano wa
mtu yeyote kuvamia kipande chochote cha ardhi kwa kuwa kila ardhi
imepangiwa matumizi yake na kusimamiwa na sheria madhubuti.
Ujumbe
wa Tanzania ukitizama maeneo yaliyoendelezwa yenye matumizi mbalimbali
nchini Singapore kwenye jengo la makumbusho ya kihistoria ya hatua za
ukuaji wa mji huo.
Kamishna
wa Ardhi Dk Moses Kusiluka(kushoto)na watendaji wa NHC na Wizara
wakipata maelezo kwa njia ya video ya namna mji wa Singapore
ulivyopangwa kulingana na ardhi iliyopo na mahitaji ya Taifa hilo.
Ujumbe
wa Tanzania ukiangalia kwa chini mchoro wenye ramani ya nchi ya
Singapore na jinsi matumizi ya ardhi yanavyoratibiwa ulipotembelea
Mamlaka ya Uendelezaji nchi ya Singapore jana.
Makamu
wa Rais wa Shirika linalosimamia mipango Miji la Singapore Bw. Anandan
Karunakaran(aliyeinama) akimueleza Waziri Lukuvi maeneo mapya
yaliyotengwa kwa ajili ya uendelezaji mpya wa mji wa Singapore baada ya
kufukia vipande vya bahari(land reclamation) ili kukidhi mahitaji ya
sasa na ya baadaye ya idadi ya watu wa nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment