TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, February 21, 2014

MWIGULU NCHEMBA AZUNGUMZA NA WANANCHI WA JIMBO LAKE.

Hii leo nimefanya Mkutano wa Hadhara Viwanja Vya Kiomboi -Stendi Wilayani kwangu Iramba.Kubwa nimezungumza na Wananchi Kazi za Maendeleo na Kupokea Kero mbalimbali Wanazokutana nazo kwenye Maeneo Wanayoishi.Msisitizo Wangu nimeagiza Serikali kupitia kwa Mkuu Wa Wilaya Kuwachukulia hatua Kali Viongozi wote Wanaokwepa Kusoma Mapato na Matumizi ya Fedha za Umma.Wananchi Wanahitaji Uwazi wa Michango yao namna ilivyotumika,Kodi zao zilivyotumika.
Pia nimeendelea kusisitiza kuwa nimeamua kupigania Sera/Sheria ya Manunuzi Serikalini inatakiwa kurekebishwa na hili nitalifanyia Kazi.
Serikali inabeba Mzigo Mkubwa sana kwenye Manunuzi.Mf.Kiatu kinauzwa Tsh.10,000/=,Mwananchi wa Kawaida anaweza kununua kiatu hicho kwa Tsh. 10,000/=.Lakini kupitia Mzabuni Serikalini kiatu hicho hicho kitanunuliwa Tsh.50,000/=.Kwa maana hiyo kunafedha nyingi sana inapotea ya Serikali kupitia Mfumo huu tulio nao sasa wa Manunuzi.
Tuungane,Tulijenge Taifa letu.
Like · · · 9 hours ago ·

  • Peter J'quix and 35 others like this.
  • Nyakia Ally Hongera kaka! Hiyo ndiyo kazi ya siasa na uongozi sharti uwe karibu na watu wako na kusikiliza na kupokea kero zao, ili zitafutiwe ufumbuzi wa kuzitatu.
  • Stahimili Wanyaka kwa kuwa wewe ni naibu waziri-ww sasa uko kiserikali zaidi kuliko ki-chama. wewe kwa sasa ni waTZ wote na si Iramba tu, nikuombe mate wangu ufike maeneo mengine ya nje ya Iramba ikiwezekana na sehemu zilizosahauliwa pia. Tatizo langu ni hayo manunuzi k...See More
  • Juma Abdallah Sadick Hongera mh.hiyo ndiyo mikakati hai na endelevu itakayoinua na kuboresha maisha ya wana iramba na watanzania kwa ujumla.juhudi zaidi zielekeze kwenye kuondoa kero mbalimbali zinazowakabili wapiga kura wako.mfano wako ni wa kuigwa na naomba waheshimiwa wengine waige mfano wako ili waipe heshima zaidi CCM na serikali yake.Viva CCM,viva Jk,viva mwigulu aluta continua....
  • Mathew Mndeme Kwenye hili ulikua na support yangu hata kabla hujawa waziri. Kwa wanaojua kinachoendelea kwenye mfumo wa manunuzi, ni jambo la kusikitisha, kuumiza na kutoa machozi kwa jinsi tunavyopoteza fedha nyingi bila tija
  • Mpalule Shaban

Thursday, February 20, 2014

MSD YATOA TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU UTARATIBU WA MANUNUZI NDANI YA BOHARI YA DAWA

  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Cosmas Mwaifwani (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam, wakati akitoa taarifa kwa Umma kuhusu utaratibu wa manunuzi ndani ya bohari ya dawa. Kulia ni Mkurugenzi wa Manunuzi wa MSD, Heri Mchunga na Mwanasheria, Domonica Meena.
………………………………………………………………………………..
 Idara ya Bohari ya Dawa (MSD) iliundwa kwa sheria ya Bunge Na. 13 ya mwaka 1993. Ni Idara inayojitegemea chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ambayo ilianzishwa ili kuunda, kudumisha na kusimamia mfumo ulio bora na wenye gharama nafuu wa ununuzi, uhifadhi na usambazaji dawa na vifaa-tiba, vitendanishi kwa ajili ya hospitali  navituo vya kutolea huduma ya afya nchini
Takwimu zilizopo kwa sasa  zinaonyesha kuwa zaidi ya asilimia  Themanini (80%) ya mahitaji yote ya Dawa,Vifaa tiba, Vitendanishi nchini vinatoka nje ya nchi hivyo taratibu za manunuzi hufuata taratibu na miongozo ya  ndani ya nchi na ya kimataifa.
Utaratibu wa uagizaji na uingizaji wa dawa ndani ya nchi huratibiwa na kusimamiwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), kuwa dawa yoyote kabla ya kuingizwa chini lazima iwe imesajiliwa na Mamlaka na  hukaguliwa pindi inapogombolewa ili kuhakikisha ubora wake. Sambamba na ukaguzi huo pia Bohari inavyo vitengo vya Ukaguzi wa Ndani (Internal Audit) na Uthibiti Ubora (Quality Assurance) ili kujihakikishia zaidi  kuwa taratibu za manunuzi zinazingatiwa pia dawa zinazonunuliwa  zinakidhi viwango vilivyokwishawekwa.
Aidha taribu za manunuzi  katika Bohari kama ilivyo taasisi nyingine yoyote ya Serikali husimamiwa  na kuongozwa na sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2011 na
kanuni zake  za mwaka 2013. Taratibu za manunuzi huanza pale ambapo kuna  uhitaji wa dawa fulani kutoka katika vituo vya kutolea  huduma ya afya nchini. Mahitaji ya dawa kutoka katika vituo vya kutolea huduma ya afya huenda sambamba na mgawo wa  fedha kwa kila kituo husika. Bohari inayo Bodi 
ya Zabuni (MSD Tender Board)  kwa mujibu wa Sheria ya Manunuzi ya Umma yenye wajumbe ambao ni wafanyakazi katika Bohari wa ngazi za juu na wenye utaalamu tofauti. Bodi  ya Manunuzi 
ndiyo chombo cha juu chenye maamuzi ya manunuzi ndani ya Bohari hivyo manunuzi yote ndani ya Bohari husimamiwa na Bodi hii.
Njia  inayotumika katika manunuzi ya bidhaa ndani ya Bohari ni kwa kupitia zabuni za kimataifa na hii ni kutokana na ukweli kwamba zaidi ya asilimia 80 ya bidhaa hutoka nje ya nchi. Zabuni ya kimataifa iko wazi kwa kila mshitiri ndani na nje ya nchi bila kubagua nchi anayotoka. Kigezo cha  kwanza  kwa mshitiri  kushiriki katika zabuni ni kuwa na bidhaa yake imesajiliwa nchini na mamlaka zinazohusika na kigezo hiki cha kusajili hakina kinga  kwa mshitiri yoyote yule.
Utangazaji wa zabuni  hufuata  na kutumia  njia na machapisho ya kitaifa na Kimataifa kupitia tovuti (webistes) za Bohari (www.msd.or.tz) na ya Mamlaka ya Manunuzi ya Umma (www.ppra.go.tz). Aidha tunatumia Magazeti ya kimataifa, na ya kitaifa katika lugha za Kiingereza na Kiswahili ili kuwafikia watu wote. Zabuni hufunguliwa hadharani kwenye siku ambayo ilitamkwa kwenye gazeti na washitiri au wawakilishi wao hualikwa kwenye zoezi hilo ili kujiridhisha kuwa vigezo mbalimbali ikiwapo bei iliyotamkwa na uwepo wa nyaraka muhimu vimefuatwa
Baada ya ufunguzi hufuata mchakato  wa tathmini (evaluations) kwa kutumia wataalamu huru  kulingana na zabuni husika, wakati mwingine wataalam hao hutoka nje ya Bohari kulingana na  utaalam wao katika zabuni husika.
Baada ya mchakato wa tathmni hufuata zoezi la kuwapata washindi , zoezi ambalo hufanywa na Bodi ya zabuni. Washindi hupatikana kutokana na vigezo vilivyoweka na hupaswa kutimizwa. Washitiri wote hupewa mrejesho juu ya mchakato mzima jinsi ya zabuni ilivyokwenda na matokeo yake. Bohari hutumia mfumo  uliowazi, haki na usawa katika manunuzi ili kuhakikisha kunakuwa na ushindani na thamani fedha kwenye mali ya umma.
Sheria ya Manunuzi ya Umma inalinda haki za mshindani yeyote yule ambaye baada ya kwisha mchakato anaweza kuwa na hisia kuwa Bohari ya Dawa haikumtendea haki kwani inamruhusu kukata rufaa kwenye Mamlaka ya ya Manunuzi ya Umma (PPRA) ambao huitisha nyaraka zote toka Bohari na kuzipitia na kisha huzitolea maamuzi.
Ili kuhakikisha uwazi na haki, Sheria ya manunuzi inatutaka tuchapishe katika vyombo vya habari matokeo ya washindi wa zabuni wote kila mwisho  wa mwaka.  Taarifa ya zabuni yamwaka wa fedha wa 2012/ 13 iliiyotolewa kwenye Mwananchi la tarehe 27/ 12/ 13 na la The Guardian la  tarehe 31/ 12/ 13 nairudia hapa ili kuonyesha washindi wa zabuni hizo, thamani na nchi ambazo makampuni hayo yanatoka.
Namba ya Zabuni    Aina ya Bidhaa    Kampuni iliyoshinda    Thamani    Tarehe ya kutoa mkataba    Nchi 
PHARMACEUTICALS
IE-009/2012/2013/HQ/G/30/04    Supply of Pharmaceuticals    Samiro Pharmacy    $ 3,379,327    12/7/2013    Tanzania
IE-009/2012/2013/HQ/G/30/05    Supply of Pharmaceuticals    Tata Africa Holdings Ltd    $ 177,668    12/7/2013    Tanzania
IE-009/2012/2013/HQ/G/30/13    Supply of Pharmaceuticals    Nirma Limited    $ 1,214,951    12/7/2013    India
IE-009/2012/2013/HQ/G/30/07    Supply of Pharmaceuticals    Novo Nordisk A/S    $ 1,516,643    12/7/2013    Denmark
IE-009/2012/2013/HQ/G/30/14    Supply of Pharmaceuticals    Abacus Paraental Drugs Ltd    $ 2,914,336    12/7/2013    Uganda
IE-009/2012/2013/HQ/G/30/03    Supply of Pharmaceuticals    SG Star Pharmaceutical Limited Total    $ 470,150    12/7/2013    Tanzania
IE-009/2012/2013/HQ/G/30/16    Supply of Pharmaceuticals    Bahari Pharmacy Ltd Total    $ 1,820,539    12/7/2013    Tanzania
IE-009/2012/2013/HQ/G/30/06    Supply of Pharmaceuticals    Planet Pharmaceutical Ltd Total    $ 846,730    12/7/2013    Tanzania
IE-009/2012/2013/HQ/G/30/08    Supply of Pharmaceuticals    Serum Institute of India Total    $ 953,577    12/7/2013    India
IE-009/2012/2013/HQ/G/30/10    Supply of Pharmaceuticals    Medopharm PVT Ltd Total    $ 386,009    12/7/2013    India
IE-009/2012/2013/HQ/G/30/09    Supply of Pharmaceuticals    Pyramid Pharma Total    $ 1,422,933    12/7/2013    Tanzania
IE-009/2012/2013/HQ/G/30/18    Supply of Pharmaceuticals    Fresenius Kabi Total    $ 1,294,587    12/7/2013    India
IE-009/2012/2013/HQ/G/30/01    Supply of Pharmaceuticals    Jilichem (T) Ltd Total    $ 6,473,661    12/7/2013    Tanzania
IE-009/2012/2013/HQ/G/30/04    Supply of Pharmaceuticals    IDA Foundation Total    $ 797,802    12/7/2013    Netherlands
IE-009/2012/2013/HQ/G/30/15    Supply of Pharmaceuticals    Claris life  sciences Limited Total    $ 970,819    12/7/2013    India
IE-009/2012/2013/HQ/G/30/17    Supply of Pharmaceuticals    Keko Pharmaceticals Industries (1997) Ltd Total    $ 19,485,669    12/7/2013    Tanzania
IE-009/2012/2013/HQ/G/30/12    Supply of Pharmaceuticals    Galentic Pharma (India) PVT Ltd Total    $ 819,836    12/7/2013    India

MAKAMU WA CCM BARA MH.PHILIP MANGULA AKUTANA NA WATANZANIA WAISHIO BEIJING CHINA

Makamu wa ccm bara MH.Philip Mangula akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watanzania wanaosoma na kufanya kazi nchini China katika mji wa Beijing baada ya kukutana nao kwa kikao kifupi katika kujadili mstakabali wa wasomi katika ujenzi wa taifa lao.Hii ilifanyika baada ya ziara fupi nchini aliyofanya MH,Mangula mwanzoni wa wiki hii.

Baadhi ya watanzania waishio nchini wakiwa katika picha ya pamoja na makamu wa ccm, bara MH.Philip Mangula
baada ya kikao cha kujadili mambo kadhaa ya mstakabali wa nchi yao katika ziara fupi aliyofanya mwanzoni wa wiki hii. 
MH.Mangula akibadilishana mawazo wadau Joel Kayombo na Shauku Kihombo ambao wapo nchini humo kwa masomo  katika moja ya vyuo vinavyopatikana mjini Beijing China

WATOTO MAPACHA WALIOTENGANISHWA NCHINI INDIA WAREJEA JIJINI DAR

Watoto mapacha kutoka wilayani Kyela mkoani Mbeya waliokuwa wamepelekwa na serikali chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kufanyiwa upasuaji mkubwa wa kuwatenganisha wakiwasili nchini Tanzania kutokea nchini India walipokuwa wakipatiwa matibabu katika hospitali ya watoto ya Appolo. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Magonjwa ya Nje wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Edward Sawe, mama mzazi wa watoto hao Bi. Grace Joel na Daktari aliyekuwa akiwaangalia nchini India Dkt.Glory Joseph.Picha na 2Watoto hao wakiwa wamebebwa na Daktari aliyekuwa akiwaangalia nchini India Dkt.Glory Joseph (kushoto) na mama mzazi wa watoto hao Bi. Grace Joel.Picha na 3Mzazi wa watoto hao Bi. Grace Joel akiwa amewabeba watoto wake Elikana Erick (kushoto) ns Eliud Erick (kulia) mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
 Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.
……………………………………………………………..
Na. Aron Msigwa – MAELEZO
 Dar es salaam.
Hatimaye watoto mapacha kutoka wilayani Kyela mkoani Mbeya waliokuwa wamepelekwa na serikali chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kufanyiwa upasuaji mkubwa wa kuwatenganisha jana jioni wamerejea nchini wakitokea nchini India katika hospitali ya watoto ya Appolo walikokuwa wanapatiwa matibabu.
Mara baada ya kuwasili katika  Uwanja ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wakiwa wameambatana  na mama yao mzazi Grace Joel na Daktari aliyekuwa akiwaangalia nchini India ambaye pia alikuwa masomoni akisomea magonjwa ya Moyo kwa watoto Dkt. Glory Joseph wamepokewa na Mkuu wa Kitengo cha Magonjwa ya Nje wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Edward Sawe  na baadhi ya wauguzi kutoka Taasisi ya Mifupa (MOI) .
Mapacha hao wa kiume wakiwa wenye  furaha na afya njema walichukuliwa katika gari maalum na kupelekwa katika Taasisi ya Mifupa (MOI) ambako watakaa kwa muda mfupi na kisha kuruhusiwa kuelekea wilayani Kyela jijini Mbeya ambako ndiko walikozaliwa.
 Kwa upande wake mama mzazi wa watoto hao akizungumza kwa furaha mara baada ya watoto wake kupatiwa matibabu ya kuwatenganisha kwa mafanikio makubwa amesema kuwa sasa maisha yake yamebadilika na ataishi kwa furaha na watoto wake.
“Najisikia furaha sana kwa hatua niliyofikia mpaka hapa watoto wangu Eliudi na Elikana sasa ni wazima naishukuru sana Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa msaada ilionipatia” amesema.
Kwa uipande wake Daktari aliyekuwa akiwaangalia nchini India ambaye pia alikuwa masomoni akisomea magonjwa ya Moyo kwa watoto Dkt. Glory Joseph akizungumzia matibabu ya watoto hao nchini India amesema kuwa hatua ya kuwatenganisha imekamilika na mwezi wa 8 mwaka huu watarudi tena nchini India kwa 
ajili ya uchunguzi na matibabu zaidi ya afya zao.
“Ni kwamba watoto hao wametenganishwa, kwa wakati huu wanaelekea MOI ambako watakaa kwa muda na baadaye wataruhusiwa kwenda kwao Mbeya kujumuika na jamaa zao” amesema.
Kwa upande wake msemaji wa wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bw. Nsachris Mwamwaja amesema kuwa watoto hao waliwasili jana jioni na ndege ya shirika la ndege la Oman baada ya kumaliza matibabu ya awamu ya kwanza.
Amesema upasuaji huo mkubwa wa kuwatenganisha watoto hao ulichukua saa 18 na kufafanua  kuwa kati ya hizo  saa 13 zilitumika kutenganisha viungo vilivyoungana sehemu ya chini ya uti wa mgongo,sehemu ya utumbo mpana,njia ya mkojo,kibofu cha mkojo na sehemu za uume huku saa 5 zikitumika kuunganisha sehemu zilizotenganishwa.
“Kumbukumbu zinaonyesha kuwa mpaka sasa duniani upasuaji wa aina hii umefanikiwa mara tano  kutenganisha mapacha watoto wa kiume walioungana” amesisitiza.
Ameongeza kuwa matibabu hayo ni juhudi za serikali katika kuhakikisha kuwa huduma za afya zinatolewa  kwa kila mwananchi kila inapowezekana na kutoa wito kwa jamii kujenga utaratibu wa kuwafikisha mapema kwenye vituo vya afya wale wote wenye matatizo ya kiafya badala ya kuwafikisha pindi hali zao zinapokuwa mbaya.

VIONGOZI WA VILABU VYA MICHEZO YA SHIMIWI KUNOLEWA FEBRUARI 24

Na Happiness Shayo
Shirikisho la Michezo Wizarani (SHIMIWI) limeandaa mafunzo ya uongozi,ualimu wa michezo na huduma ya kwanza viwanjani   kwa viongozi wa vilabu vya michezo ya SHIMIWI,yatakayofanyika mjini Morogoro  Februari 24-28 mwaka huu.
Hayo yalisemwa na Kaimu Katibu Mkuu wa SHIMIWI Bw.Moshi Makuka mapema leo ofisini kwake alipokuwa akitoa taarifa ya utekelezaji wa mikakati ya shirikisho hilo kwa mwaka wa fedha 2013/2014.
Bw.Makuka alifafanua kuwa lengo la mafunzo hayo kwa viongozi wa vilabu ni kuwajengea uwezo wa kuongoza shughuli za michezo,kuwapa ufahamu zaidi juu ya  katiba,sheria na kanuni za michezo ya SHIMIWI na kuwapa uelewa wa namna ya kutoa huduma ya kwanza katika viwanja vya michezo.
Akielezea sababu za Shirikisho hilo kuandaa mafunzo hayo Bw.Makuka alisema kuwa mafunzo hayo yanafanyika kutokana na na changamoto zilizojitokeza katika mashindano ya SHIMIWI ya miaka iliyopita  ambapo baadhi ya viongozi huvunja sheria na kanuni za michezo.
“Baadhi ya viongozi wa SHIMIWI katika Wizara ,Idara Zinazojitegemea,wakala wa Serikali na Ofisi za Wakuu wa Mikoa (SHIMIWI) wamekuwa wakilalamikiwa kutumia wachezaji ambao sio watumishi wa umma .”alisema Bw.Makuka.
Pia,aliongeza kuwa mafunzo hayo yatawahamasisha viongozi wa ofisi za Serikali zilizoshindwa kushiriki katika michezo ya mwaka jana ili iweze kushiriki mwaka huu kwa kuwa michezo kwa watumishi wa umma hujenga afya,mshikamano na pia huongeza ufanisi mahala pa kazi.
Michezo ya SHIMIWI ilianzishwa kwa madhumuni ya kuwakutanisha watumishi wa Serikali kwa lengo la kujenga nakuendeleza tabia ya ushirikiano,upendo na undugu hivyo hufanyika kila mwaka.Mafunzo haya hufanyika kila mwaka kwa mujibu wa kalenda ya SHIMIWI.

OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU YATOA SEMINA KWA WAHARIRI WA HABARI JUU YA KANZA INAYOONESHA VIASHIRIA VYA KIUCHUMI NA KIJAMII

 
Watanzania wameshauriwa kutumia kanza inayoonesha viashiria vya kiuchumi na kijamii (Tanzania Social Economic Database -TSED) ili kurahisisha upataji wa taarifa pindi wanapokuwa katika kazi zao za kila siku.
 
Akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari katika washa ya siku moja iliyoandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu leo jijini Dar es salaam, Meneja wa Teknojia ya habari na Masoko Bi. Mwanaidi Mahiza amesema kuwa TSED inasaidia kupata taarifa kwa haraka kwa njia ya mtandao bila kuzifuata katika ofisi mbalimbali za Serikali.
 
“TSED inasaidia kuondoa mlolongo wa upatikanaji wa taarifa uliopo kwenye baadhi ya ofisi nyingi ambapo wakati mwingine mteja utaambiwa uandike barua au urudi baada ya siku kadhaa,” amesema Mahiza.
 
Bi. Mahiza amesisita kuwa ni muhimu kutumia kanza hiyo kwa kuwa ndani yake kuna takwimu rasmi ambazo zinatoka katika vyanzo sahihi vyenye mamlaka ya kutoa takwimu hizo hapa nchini.
 
Kanza inayoonesha viashiria vya kiuchumi na kijamii ilizinduliwa rasmi mwaka 2001 ikiwa na viashiria 75 ambapo hivi sasa ina viashiria 940 na inapatikana katika mfumo wa DVD, CD ROMs na tovuti ya www.tsed.org.
Meneja wa Teknojia ya habari na Masoko Bi. Mwanaidi Mahiza akifafanua jambo kwa wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari (hawapo pichani) wakati wa washa ya siku moja iliyoandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu,katika hoteli ya JB Belmont jijini Dar es salaam leo.
Mchambuzi wa Mifumo ya Kiteknolojia kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu,Martin Kimario akitoa maelezo ya mtandao wa TSED kwa wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari (hawapo pichani) wakati wa washa ya siku moja iliyoandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu,katika hoteli ya JB Belmont jijini Dar es salaam leo.
Mmoja wa wahariri wa vyombo vya habari akichangia mada kwenye warsha hiyo.
Sehemu ya Wahariri wa vyombo vya habari wakiwa kwenye warsha hiyo.Picha Zote na Othman Michuzi.

KATIBU MKUU WIZARA YA ULINZI AWASILI MKOANI RUKWA KWA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU TATU, AAHIDI KUBORESHA MIUNDOMBINU YA VITEULE VYA JESHI VYA KIRANDO NA KASANGA MKOANI RUKWA

Katibu Mkuu wa Wiazara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Ndugu Job Masima akishuka kwenye ndege aina ya Auric Air katika uwanja wa ndege wa Sumbawanga mapema jana kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tatu Mkoani Rukwa kufuatia mwaliko wa Mkuu wa Mkoa huo Injinia Stella Manyanya.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya kulia akimtambulisha Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Symthies Pangisa kwa Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Ndugu Job Masima mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Sumbawanga jana.
Katibu Mkuu wa Wiazara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Ndugu Job Masima kulia akisalimiana na mwanasiasa Mkongwe nchini Ndugu Chrissant Mzindakaya katika uwanja wa ndege wa Sumbawanga, Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya. 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na msafara wa Katibu Mkuu wa Wiazara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Ndugu Job Masima ofisini kwake jana. Mkuu huyo wa Mkoa alimshukuru Katibu Mkuu huyo kwa kukubali mwaliko wake. Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ameahidi kuboresha miundombinu ya viteule vya jeshi vilivyopo Mkoani Rukwa ukiwepo usafiri, majengo na nishati ya umeme wa jua.
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Kimanta akisalimiana na rafiki yake wa siku nyingi Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Luten Kanali Sipe mara baada baada ya kuonana na msafara wa Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Ofisini kwake jana. 
(Na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)