TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, February 20, 2014

DC HANDENI ATOA AGIZO LA UJENZI WA NYUMBA BORA NA UPANDAJI WA MITI KUZUIA MAJANGA

Na Mohammed Mhina, Handeni
Mkuu wa Wilaya ya Handeni mkoani Tanga Bw. Muhingo Rweyemamu, amewataka wananchi wilayani humo, kujenga nyumba imara na kupanda miti ya vivuli na matunda ili kustawisha mazingira na kuzuia upepo kuvuma kwa kasi na kuleta madhara.
 
Akizungumza kwa niaba yake Afisa Tawala wa wilaya hiyo Bi. Pendo Magashi, alisema kuwa upandaji wa miti inaweza kuwanufaisha wananchi mbali ya kupata matunda lakini pia itasaidia kuvuta mvua na kuzuia uwezekano wa upepo kuvuka kwa kasi.
 
Bi. Pendo alikuwa akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Mzeri “B” kilichopo katika kata ya Misima wilayani Handeni alipokwenda kuwafariji baada ya upepo mkali ulioambatana na mvua kubwa kuezua mapaa ya nyumba 36 kijijini hapo na kuwaacha wananchi 238 bila ya makazi.
 
Kwa upande wa majengo, Bi. Pendo alisema kuwa nyumba nyingi zimeezuliwa kutokana na kukosa ujenzi hafifu usiohimili majanga ya kimaumbile.
 
Afisa Tawala huyo pamoja na ujumbe wake pia walipata nafasi ya kumtembelea mama Tabu Mhailo, ambaye siku ya tukio hilo Februali 14, mwaka huu akiwa na motto mchanga chumba alinusurika baada ya paa la nyumba yao kuezuliwa na upepo huku milango ikiwa imejifunga.
 
Akizunguzia tukio hilo, Mama Tatu alisema siku ya kimbunga hicho alilazimika kuingia mvunguni mwa kitanda kwa lengo la kujinusuru maisha yake yeye na pamoja na mtoto wake na kutoka baadaye baada ya mvungu huo wa kitanda pia kujaa maji.
 
Wakati wa mkutano na viongozi hao, baadhi ya wananchi waliiomba Serikali kuangalia uwezekano wa kuwasaidia mahitaji muhimu kama vile chakula na mavazi vitu baada ambavyo viliharibiwa ama kusombwa na maji siku ya tukio hilo.
 
Aidha wameomba pia kupatiwa mahema ya kujikinga na maridi ama mvua kwani baadhi yao wanalazimika kulala nje ya mabaki ya nyumba zao baada ya kukosa maeneo ya kujihifadhi kutokana na wingi wa waadhirika wa kimbunga hicho.

No comments:

Post a Comment