Watanzania wameshauriwa kutumia kanza inayoonesha viashiria vya kiuchumi na kijamii (Tanzania Social Economic Database -TSED) ili kurahisisha upataji wa taarifa pindi wanapokuwa katika kazi zao za kila siku.
Akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari katika washa ya siku moja iliyoandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu leo jijini Dar es salaam, Meneja wa Teknojia ya habari na Masoko Bi. Mwanaidi Mahiza amesema kuwa TSED inasaidia kupata taarifa kwa haraka kwa njia ya mtandao bila kuzifuata katika ofisi mbalimbali za Serikali.
“TSED inasaidia kuondoa mlolongo wa upatikanaji wa taarifa uliopo kwenye baadhi ya ofisi nyingi ambapo wakati mwingine mteja utaambiwa uandike barua au urudi baada ya siku kadhaa,” amesema Mahiza.
Bi. Mahiza amesisita kuwa ni muhimu kutumia kanza hiyo kwa kuwa ndani yake kuna takwimu rasmi ambazo zinatoka katika vyanzo sahihi vyenye mamlaka ya kutoa takwimu hizo hapa nchini.
Kanza inayoonesha viashiria vya kiuchumi na kijamii ilizinduliwa rasmi mwaka 2001 ikiwa na viashiria 75 ambapo hivi sasa ina viashiria 940 na inapatikana katika mfumo wa DVD, CD ROMs na tovuti ya www.tsed.org.
Meneja wa Teknojia ya habari na Masoko Bi. Mwanaidi Mahiza akifafanua jambo kwa wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari (hawapo pichani) wakati wa washa ya siku moja iliyoandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu,katika hoteli ya JB Belmont jijini Dar es salaam leo.
Mchambuzi wa Mifumo ya Kiteknolojia kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu,Martin Kimario akitoa maelezo ya mtandao wa TSED kwa wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari (hawapo pichani) wakati wa washa ya siku moja iliyoandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu,katika hoteli ya JB Belmont jijini Dar es salaam leo.
Mmoja wa wahariri wa vyombo vya habari akichangia mada kwenye warsha hiyo.
Sehemu ya Wahariri wa vyombo vya habari wakiwa kwenye warsha hiyo.Picha Zote na Othman Michuzi.
No comments:
Post a Comment