Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa PSPF Bw. Adam Mayingu akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wadau wa mfuko huo katika semina iliyoshirikisha waandishi wa habari pamoja na baadhi ya wadau wa mfuko huo kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na mfuko huo na fursa mbalimbali pamoja na mafao mbalimbali yanayotolewa na mfuko huo ambapo wakuu wa vitengo mbalimbali wameelezea jinsi mfuko huo unavyofanya kazi zake na ukusanyaji wa michango ya wanachama, Mfuko huo umewaasa waandishi wa habari kujiunga na mpango wa hiari ambao una faida kubwa sana kwa mwanachama atakayejiunga na PSPF, Semina hiyo imefanyika katika ukumbi wa JB Belmont Hotel jengo la Golden Jubilee Towers jijini Dar es salaam.Mamaa Thauda wa Nguvu kutoka Chanel 5/ EATV ameshiriki katika semina hiyo hapa akisikiliza mambo muhimu yaliyokuwa yakielezwa katika semina hiyoNeema Muro Mkurugenzi wa Uwekezaji katika mfuko huo akitoa mada juu ya uwekezaji katika mfuko wa PSPF.Mkurugenzi wa Fedha Masha Mushomba akizungumzia masuala ya fedha na ukusanyaji pamoja na ulipaji mafao kwa wanachama wa mfuko huo.Andrew Nkangaa Mkurugenzi wa Tehama katika mfuko huo akizungumzia jinsi wanachama wanavyoweza kuchangia mfuko huo kwa kutumia mitandao ya simu na kurahisisha shughuli zao za kila siku badala ya kufuata ofisi za PSPF zilipo kwa ajili ya kwasilisha michango yao.Mkurugenzi wa mtandao wa www.fullshangweblog.com Bw. John Bukuku kulia akiwa na Mkurugenzi wa 8020fashion Shamimu Mwasha katika semina hiyoAndrew Nkangaa Mkurugenzi wa Tehama kulia akiweka mambo sawa kabla ya kuwasilisha mada yake katika semina hiyo.Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika semina hiyoWaandishi wa habari wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa katika semina hiyoMwandishi wa Habari Abdull Saiboko kutoka TSN akisikiliza kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa katika semina hiyo.Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika semina hiyoAdam Mayingu Mkurugenzi mkuu Mfuko wa PSPF akizungumza na kufanya ukaribisho katika semina hiyo, katika picha kutoka kulia ni Masha Mashomba Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Gabriel Silayo mkurugenzi Uwekezaji na kutoka kushoto ni Andrew Nkangaa Mkurugenzi wa TEHAMA, Mwanja Sembe Meneja wa PSPF na Neema Muro Mkurugenzi Uendeshaji.
No comments:
Post a Comment