Tunasikitika kutangaza kifo cha ghafla cha
dada yetu mpendwa Leticia Mattei Rwechungura kilichotokea hapa
Ujerumani tarehe 06.01.2015.Mazishi yatafanyika hapa Ujerumani
Königswinter, karibu na mji wa Bonn tarehe 24.01.2015. Misa itaanza saa
tano asubuhi (11:00 a.m.), katika Kanisa la St. Michael
Niederdollendorf, Petersbergerstr. 14, 53639 Königswinter.
Dada
Leticia Mattei alikuwa mfanyakazi wa Umoja wa Mataifa huko South Sudan
(UNMIS) - United Nations Mission in Südan, Eastern Equatoria State of
Torit-Sudan. Aliugua muda mfupi na kufariki dunia katika hospitali
iliyoko mjini Bonn hapa Ujerumani.
Watanzania wote walioko hapa
Ujerumani, nyumbani Tanzania na ulimwenguni kote wameshtushwa na kifo
hiki cha ghafla cha kuondokewa na mama yetu na dada yetu mpenzi Leticia
Mattei. Tutamkumbuka daima kwa kazi kubwa alizoifanyia nchi yetu ya
Tanzania, bara la Afrika na dunia nzima kwa ujumla. Mungu amlaze mahali pema Peponi - Amin! Kwa yeyote atakayependa kutoa sanda yake, tunaomba michango itumwe moja kwa moja kwa mtoto wa marehemu:
Tunaomba
sana ili tuweze kutekeleza mipango hii vizuri ya kumsindikiza dada yetu
kwa heshima zote, wale wanaopenda kuhudhuria mazishi haya wawasiliane
na mratibu wa shughuli hizi Nd. Majura, ili tupate orodha kamili ya wale
wanaokuja ili itusaidie kuandaa mambo mengi ya muhimu. Kwa wale
watakaopenda kupata malazi (ya hoteli), kadhalika tunaomba wawasiliane
na Dr. Isack Majura kuanzia sasa kupitia:
Serikali ya Tanzania itaendelea
kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji na kuendeleza ushirikiano na mahusiano mzuri
uliopo kati yake na nchi zinazounda umoja wa nchi za Ghuba (GCC).
Kauli hiyo imetolewa jana jijini Dar es salaam na Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima alipokuwa
akifunga mkutano wa siku mbili wa wafanyabishara kutoka Tanzania na nchi za GCC
ambao ulianza Januari 15 hadi 16 mwaka huu.
Malima alisema kuwa Watanzania
umefika wakati wa kuboresha biashara zetu ili kuweza kuuza bidhaa bora ndani na
nje ya nchi na kukabiliana na changamoto za soko la kimataifa.
“Viwango vya mazao yetu
vinapaswa viewe bora, ambapo ubora huo utaruhusu bidhaa zetu ziuzike nchi
nyingine” alisema Malima.
Akitolea mfano, Malima
alisema Tanzania imejaliwa kuwa na mifugo mingi inayoweza kuzalisha nyama
ambayo soko lake tunalo tayari ambalo ni nchi za GCC na kusisitiza kuwa nyama
hiyo inapaswa kuandaliwakatika
machinjio salama na ya kimataifa ili kufungua fursa ya kuuza nyama hiyo maana
milango sasa ipo wazi kwa serikali ikishirikiana na wafanyabiashara nchini.
Kwa upande wake Makamu
wa Rais wa Shirikisho la Wafanyabiashara kutoka nchi za Ghuba (FGCCC)
Abdulrahman Bin Saleh Al- Otainshan alisema kuwa jumuiya ya wafanyabiashara wan
chi za Ghubawameona na wanatarajia kufanya
biashara Tanzania katika sekta ya kilimo na mifugo ambapo wanategemea kupata
mzao mbalimbali yanayohitajika nchi za Uarabuni.
Mazao hayo
yanayohitajika ni pamoja na mchele, matunda, mboga mboga, asali na nyama.Zaidi ya hayo, Rais hyo
wa FGCCC alisema kuwa nchi zianazounda umoja huo zinatarajia kuwekeza Tanzania katika
sekta zakilimo, mifugo, elimu, maji,
afya, ufundi na utalii.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa
benki ya BADEA alisema kuwa Abdel Aziz Khelef alisema kuwa benki yake
itaendelea kuwa kiunganishi muhimu kati ya wafanyabiashara wa Tanzania na nchi
za GCC ambapo wamekuwa na uhusiano mzuri kwa zaidi ya miaka 40.
Nchi zinazounda umoja
wa GCC ni Kuwait, Oman, Bahrain, Qatar, UAE na Saud Arabia zinauhusiano wa
karibu na Tanzania kihistoria, lugha pamoja mila na desturi.
Ndugu
Elly David Akitoa Mada Kuhusu Vijana kujituma na kufanya kazi kwa Bidii
Kwa maendeleo ya taifa.Mtoa Mada huyo amesema kutokana na Ukosefu wa
ajira hususani kwa vijana ni vyeme vijana kujituma na kuwa wabunifu na
waweze kujiajiri kwa lengo la Kupambana katika Maisha.Katika
Kongamano hilo la Vijana lililofanyika Jijini dar es salaam Liliwapa
Fursa vijana kueleza Changamoto zinazowakabili na namna ya
Kuzikabili.Kongamano hilo lililoandaliwa na Elly David mara baada ya ya
kuona changamoto zinazowakabili vijana wa kitazania ili kuwapa fursa
vijana kukutana kubadilishana mawazo Pamoja na Kuangalia namna ya
kutatua changamoto zinazowakabili vijana wa Kitanzania/
MSAJILI wa Vyama Vya Siasa nchini,
Jaji Francis Mutungi amevitaka vyama vyote vya siasa kutekeleza wajibu
wao kwa mujibu wa sheria , katiba na kanuni ili kuepusha migogoro. Aidha msajili huyo amevitaka vyama hivyo mfano mzuri wa kwa jamii kwa kudumisha amani na utulivu ndani ya vyama vya siasa.
Kauli hiyo imetolewa leo na Msajili huyo katika taarifa yake
aliyoitoa kwa vyombo vya habari kufuatia kuwepo kwa wimbi kubwa la
migogoro ndani ya vyama hivyo. “Endapo kwa bahati mbaya mgogoro ukiibuka, unatakiwa utatuliwe
kwa utaratibu na namna ambayo itadumisha amani na utulivu ndani ya
chama,” alisema Jaji Mutungi.
Jaji Mutungi amewataka wanachama wa kawaida wa vyama vya siasa
kupenda amani na utulivu ndani ya chama na kuepuka migogoro kwa
kuheshimu na kufuata mfumo au taratibu za kuwasilisha malalamiko uliopo
ndani ya chama au taasisi husika. Pia wawe wavumilivu mpaka watakapopata
majibu ya malalamiko yao kutoka katika utaratibu huo uliowekwa na
taasisi husika.
Aliongeza kuwa ofisi yake inajitahidi kuepusha na kutatua
migogoro ndani ya vyama kwa kuchukua hatua zifuatazo, ambazo ni
kuvihimiza vyama vya siasa kuheshimu sheria,kuzingatia misingi ya
demokrasia na utawala bora,katiba na kanuni zake, kusuluhisha mgogoro
unapoibuka,“Na hivi sasa tumewasilisha Serikalini mapendekezo ya
marekebisho ya sheria yatakayosaidia kuepusha migogoro ndani ya vyama,”
alisisitiza.
Ameiomba jamii ikemee tabia ya migogoro isiyo na tija ,inapoona
vyama vya siasa havitekelezi wajibu wake, badala yake vinajikita katika
migogoro ndani ya ndani.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Baraza la Mawaziri
cha kwanza kwa mwaka huu wa 2015 Ikulu jijini Dar es salaam January
16, 2015. Kulia kwake ni Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali na
kushoto kwake ni Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda.
PICHA NA IKULU
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana jana
aliwasili Arusha kwa lengo la kufanya mazungumzo na makundi matatu ya chama cha SPLM ya
Sudani ya Kusini, mashauriano hayo yalilenga kukamilisha makubaliano baina ya
makundi hasimu. Baada
ya Mazungumzo Ndugu Kinana alisema ana matumaini ya kufikiwa makubaliano ya
kukiunganisha chama cha SPLM katika siku chache zijazoKutoka
kushoto ni Balozi David Kapya,Abdulrahman Kinana,Mwenyekiti wa
Mazungumzo Dk.John Samuel Malecela na Makamu Mwenyekiti wa mazungumzo
Dk. Hassan Kibelloh mazungumzo hayo yalifanyika Ngurdoto Arusha.
Viongozi
wa Makundi matatu kutoka chama cha SPLM kutoka Sudani ya Kusini wakiwa
kwenye mazungumzo ya kufikia makubaliano ya kuunganisha chama chao cha
SPLM. Hapa wakiwa na viongozi wa Tanzania wanaosaidia kumaliza tofauti
na yakiwa yanasimamiwa na Chama Cha Mapinduzi chini ya uongozi wa Katibu
Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana. ====== ====== ===== =======
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa
Jakaya Mrisho Kikwete alitangaza kuwa Tanzania imekubali kuwa msuluhishi wa
mgogoro wa kisiasa ndani ya chama tawala cha Sudan Kusini cha Sudanese People’s
Liberation Movement (SPLM), mgogoro
ambao ulisababisha kuzuka kwa vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.
Hata hivyo, Rais Kikwete alisema kuwa usuluhishi huo
utakuwa wa kichama na Chama cha Mapinduzi (CCM) ndicho kitaongoza usuluhishi
huo katika mazungumzo yatakayofanyika Arusha na kuwa jitihada hizo za Tanzania
hazitaingilia mazungumzo ya kujaribu kusimamisha mapigano nchini humo
yanayoendelea huko Addis Ababa, Ethiopia.
Rais Kikwete alisema kuwa ulikuwa uongozi wa SPLM na hasa
Mwenyekiti wa Chama hicho, Rais Salva Kiir ambao wameiomba Tanzania kusaidia
jitihada za kisiasa za kupatanisha pande ambazo zinavutana na kutofautiana
ndani ya SPLM wakiamini kuwa mapatano ndani ya chama yatafanikisha kumaliza
mgogoro wa kisiasa katika Serikali ya nchi hiyo ambayo imegawanyika na kusababisha vita vya wenyewe kwa
wenyewe.
Rais Kikwete alitangaza jitihada hizo za upatanishi za
Tanzania wakati alipohutubia maelfu kwa maelfu ya wananchi na kupitia kwao
Taifa kwenye Sherehe ya Kuzima Mwenge wa Uhuru, Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere
na Kilele cha Wiki ya Vijana kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
“Ni fahari kwetu kwamba wananchi wa Msumbiji, Zimbabwe,
Angola, Namibia na Afrika Kusini nao wako huru na tumetoa mchango wetu. Ni jambo la faraja kubwa kwamba nchi yetu
imeweza kupatia hifadhi ndugu zetu wa nchi jirani na hata mbali wakati maisha
yao yalipokuwa hatarini kwa sababu ya kukosekana kwa amani ama kukimbia mateso
ya uongozi wa kidikteta. Ndugu zetu wa Kongo, Burundi, Rwanda, Kenya na Comoro
wanaujua ukweli huo. Na, kwa Uganda tuliwasaidia kuling’oa Dikteta Idd Amin na
Comoro tulisaidia kuunganisha nchi yao tena.”
CORRECTS CROWNING DATE TO JAN
25 - FILE - In this Oct. 2, 2014 file photo, Miss Universe, Gabriela
Isler, of Venezuela, speaks during a news conference in Doral, Fla.
Isler's reign is in its final days, with the next woman to wear the
crown to be selected Jan. 25 in Miami. The classic tiara _ the one that
slipped off her head on the night she was crowned _ soon will be gently
placed atop someone else and after touring the world almost nonstop,
Isler is ready to see what the next chapter brings. (AP Photo/Wilfredo
Lee, File)
MIAMI (AP) — When
Gabriela Isler wakes up on Jan. 25, it will mark the 441st and final
time that she will begin a day while wearing the title of Miss Universe.
Then, as she put it, she becomes "just Gabby" again.
Isler's
reign is in its final days, with the next woman to wear the crown to be
selected Jan. 25 in Miami. The classic tiara — the one that slipped off
her head on the night she was crowned — soon will be gently placed atop
someone else and after touring the world almost nonstop, Isler is ready
to see what the next chapter brings.
"Before
all this, I was just a simple girl, no makeup, no hair, no heels, just a
normal girl finishing my education," Isler said in an interview with
The Associated Press. "This just changed my life. This made me feel
confidently beautiful. ... Now I'm happy with myself every day. I
learned to be happy. I grew up in every way, as a daughter, as a sister,
as a girlfriend, as a friend. It transformed my life."
The
5-foot-10 Venezuelan carries her country's flag with intense pride,
even as her nation continues to battle over economy and politics. Being
an example for women in her country was a top priority during her time
as Miss Universe, and once it ends Isler plans to step up her efforts by
combating a massive problem with teen pregnancy in her homeland.
"During
my reign, I discovered myself," Isler said. "I want to continue doing a
lot of things related to humanitarian efforts, so one of my new
chapters will be maybe becoming a spokesperson for different
organizations, but my first one is my baby — starting my own foundation
in Venezuela that can help create awareness and bring education and
family values to young girls and young women."
Choking levels of
inflation and shortages of basic goods are part of the norm in
Venezuela, where beauty pageants are big business and a source of
national pride.
"With all that's happening in Venezuela, to have a
chance to be a good-news person for my country I feel so satisifed,"
Isler said. "I did as much as I can — not just to represent the Miss
Universe organization but also my country."
There
is symmetry to her reign ending South Florida, which has a massive
Latin population and is the place that Isler says will be her second
home.
The Miss Universe pageant itself will be at Florida
International University in Miami, but many of the preliminary events
leading up to the big night will be in the nearby suburb of Doral,
Florida — which has an enormous Venezuelan population.
"I was
dreaming to give my crown in Venezuela," Isler said. "But to have this
opportunity to end this reign and close a chapter in my life around the
Venezuelan community, this Latin environment, this Latin energy, I
couldn't ask for a better place."
When
asked if one day stood out among all others during her reign, Isler
didn't hesitate. She quickly chose Sept. 3, the day she went to the
Vatican, heard Pope Francis speak about the role of women in the church
and received a blessing from the pontiff.
"I
was not able to sleep the day before because I was so excited," Isler
said. "I couldn't believe it was real. I was like, 'Really, I'm going to
meet the Pope?' I went to the Vatican and I couldn't stop crying and I
could cry again. It was a dream. ... I was in tears. I didn't know I was
awake. ... That day I realized, this was real."
Isler
expects to shed tears on pageant night, not because her time as Miss
Universe will be over but out of both fear and excitement for whatever
will happen next.
"I can't
wait to wake up and just enjoy the day," Isler said. "Have a breakfast
in bed and just have the opportunity to have the first official day
where I can make my own decisions and start my dreams."
She won't sit idle for long.
Her first meeting is already scheduled — for Jan. 26.
Maandamano nchini Pakistan kuonyesha kero la waumini wa kiisilamu kuhusu Charlie Hebdo
Polisi
nchini Pakistan wamekabiliana na waandamanaji, walioghadhabishwa na
uamuzi wa jarida na Ufaransa la Charlie Hebdo wa kuchapisha vibonzo vya
mtu wanayedai ni Mtume Mohammad.
Baada ya maombi ya ijumaa,
maafisa wa ulinzi walitumia magari yenye majai kuwamwagia maji
waandamanaji katika juhudi za kuwatwanya. Walikuwa wamekusanyika nje ya ubalozi wa Ufaransa mjini Karachi. Baadhi ya waandamanaji inaarifiwa walikuwa wamebeba bunduki. Watu watatu walijeruhiwa katika maandamano yenyewe. Mwandishi
wa BBC mjini Islamabad amesema idadi ya waandamanaji hao, kwa mujibu wa
idadi ya wasisilamu nchini Pakistan, ilikuwa ndogo. Maandamano
kama hayo yameitishwa katika nchi zingine zilizo na idadi kubwa ya
waumini wa Kiislamu kama vile Uturuki, Ufilipino,Kuwait, Mauritania na
Sudan.
Wapiganaji wa Boko Haram wamekuwa kero kubwa kwa wananchi wa Nigeria kwa miaka mingi sasa
Serikali
ya Cameroon imesema Chad itatuma kikosi kikubwa cha wanajeshi wake
kupambana na wapiganaji wa kiisilamu wa Boko Haram mpakani mwa Nigeria
na nchi hio.
Tangazo hili limetolewa siku moja baada ya Chad
kusema kwamba itaunga mkono jirani yake Nigeria katika harakati dhidi ya
wapiganaji wa kiisilamu wa Boko Haram. Hakuna taarifa zozote zimetolewa kuhusu idadi kamili ya wanajeshi watakaopelekwa huko au siku. Mnamo
siku ya Jumanne, Cameroon ilisema kwamba iliwaua wapiganaji 143 wa Boko
Haram, ambao walishambulia kambi zake katika eneo la Kolofata karibu na
mpaka na Nigeria. Ilisema kuwa mwanajeshi mmoja alifariki wakati
wa mashambulizi hayo ambayo yalisababisha ufyatulianaji risasi mkali
kati ya wanajeshi na waasi hao kwa muda wa saa tano. lilikuwa
shambulizi la kwanza kubwa kufanywa na Boko Haram dhidi ya Cameroon
tangu kundi hilo kutishia kiongozi wa nchi hio katika kanda ya video
waliyoiweka kwenye mtandao mapema mwezi huu. Wanamgambo hao
wameteka miji na vijiji kadhaa ambavyo wanavidhibiti Kaskazini Mashariki
mwa Nigeria katika harakati zao ambazo wameziendeleza kwa miaka sita
sasa.
Dubai
imejinyakulia sifa ya kipekee katika kupima Imani za jamii kwa pochi
iliyoangushwa mtaani,na mara ikarejeshwa kwa mhusika mara moja.
Katika
utafiti uliofanywa na mtengeneza Filamu mwenye asili ya Uingereza
katika mitaa ya Dubai, alijaribu mara arobaini na tano kuidondosha kwa
makusudi na katika kila tukio msamaria aliyeiokota aliirejesha pochi
hiyo kwa mmiliki wake.
Daniel Jarvis, mwenye miaka 26,akiwa
ameificha kamera yake na kurekodi mfululizo wa matukio hayo ya makusudi
akiwa pamoja na rafikiye aliyejipachika jina la utani la 'Digi' ama Dan,
mwenye miaka 25, walibarizi katika viunga vya Downtown na Bur vilivyoko
Dubai,siku za karibuni na kuweka swali je unaweza kuiba Dubai? Kutaka
kuichunguza jamii na kurushwa vipande vyake katika YouTube ambapo mpaka
kufikia jana usiku watazamaji walikuwa ni zaidi ya 70,000 .
Jarvis
aliiambia 7DAYS walishangazwa na utafiti huo na kikubwa
kilichowasangaza ni kwamba waliookota pochi hiyo hawakujishughulisha
kutazama ndani kuna nini? Wakati pochi hiyo ilikuwa imesheni euro za
kutosha na fedha ya Falme za Kiarab dirham kadhaa.
Mtaa wa kwanza
walioufanyia majaribio ni mtaa uliko katika barabra ya Sheikh Zayed
karibu na soko kuu la kibiashara na jirani kabisa na mnara wa Emirates
lakini kila aliyeiona pochi hiyo aliirejesha,lakini baadaye tukafikiri
sababu ya kurejeshwa pochi hiyo kuwa walioko eneo hilo ni matajiri.
Basi
utafiti wetu tukauhamishia eneo la Bur ,Dubai, mahali ambapo
palionekana duni kidogo cha ajabu watu waliendeleza utamaduni ule ule wa
kurejesha pochi kama ilivyo, na hali eliendelea hivyo mara kadhaa.
Jarvis
anasema wameshafanya utafiti kama huo katika mji wa London nchini
Uingereza. Na huko walistaajabu walipoidondosha tu aliyeiokota alianza
kukimbia nayo wa nako hakuna aliyethubutu kuichukua pochi hiyo.
Jarvis,
alivalia suti nadhifu na kuigiza kudondosha pochi anaonekana kwenye
video hiyo anaeleza hisia za kurejeshewa kitu ulichondondosha kuwa ni
raha iliyoje .lakini akaendelea kusema kuwa anadhani vyombo vya habari
hupotosha ukweli,kwakuwa kulikuwa na kichwa cha habari kuwa kuna mtu
alihukumiwa miaka 15 jela kwa kuiba mdoli wenye taswira ya dubu, utafiti
wetu umegundua tofauti na wayasemayo.
Trollstation ina wanachama
wapatao 230,000 na utafiti wao kutoka Falme za Kiarab unaelekezwa Ulaya,
Marekani na hatimaye Afrika .
Inawezekana katika maeneo watakayopita kuvunja rekodi ya Dubai tusubiri wakati uwadie, ni kauli yake Jarvis .
Mhubiri mmoja nchini Iran amewaacha watu vinywa wazi kwa kuvalia vazi la rangi ya manjano.
Hoseyn
Khademian alionekana kwenye televisheni akivalia shati la manjano ,
viatu na hata saa ya rangi hiohio. Taarifa hii ni kwa mujibu wa shirika
la habari la Mehr. Wahubiri nchini Iran, kwa kawaida huvalia
mavazi meupe na joho la rangi isiyong'aa sana huku viatu vyao vikiwa
vyeusi au vya hudhurungi. Lakini mavazi ya Khademian yalikejeliwa na kufanyiwa gumzo sana kwenye mitandao ya kijamii. Wakati
baadhi ya watu kwenye Facebook walimzomea wakisema anajitakia tu sifa,
wengine walimfananisha na ndizi lilioivaa kupitiliza. '' Msomaji mwengine alisema, '' angependeza zaidi ikiwa angevalia kilemba cha waridi,basi angependeza sana''. Wakati
mwonekano wake umegonga vichwa vya habari nchini Iran, bwana Khademian
anasema yeye haoni kwa nini watu wanamsema sana kwani sio mara yake ya
kwanza kuvalia mavazi ya manjano. Mara ya mwisho alionekana
kwenye TV akiwa amevalia mavazi ya waridi, anahoji ''kwa nini watu
hawakunisema sana wakati huo,''ikilinganishwa na sasa rangi ya mavazi
yangi sio kitu kipya,'' alisema Bwana Khademian. Rangi ya manjano ni
rangi ya kawaida kama rangi nyinginezo''.
Waziri mkuu wa Ethiopia (kulia) Hailemariam
Desalegn amekuwa akikosolewa na kuwa na sheria kali za kupambana na
ugaidi
Raia wawili wa Uingereza na msomali mmoja wamefungwa jela nchini Ethiopia kwa kupanga njama ya kuunda dola ya kiisilamu.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa kituo cha redio kinachounga mkono serikali. Taarifa hii imethibitishwa na ofisi ya mambo ya nje ya Uingereza. Wanaume
hao watatu waliohukumiwa kifungo cha kati ya miaka minne na saba
walidaiwa kuwa na uhusiano na kundi la wapiganaji wa kiisilamu. Ethiopia ina sheria kali sana za kupambana na ugaidi. Kwa mda mrefu imekuwa ikiendesha harakati dhidi ya kundi la wapiganaji wa kiisilamu wa Al shabaab nchini Somalia. Nchi
hio pia imekuwa ikikabiliwa na madai ya kuwafunga jela wakosoaji wa
serikali wakiwemo wanablogu maarufu nchini humo ambao wanakabiliwa na
tisho la kufungwa jela kwa madai ya kuhusika na ugaidi na wamekuwa
wakizuiliwa tangu Aprili mwaka 2014. Hata hivyo kiongozi wa nchi hio ametetea sana sheria kali za ugaidi ambazo nchi hio hutumia. Kulingana
na FBC, washukiwa wawili waingereza, Ali Adros Mohammad na Mohammad
Sharif Ahmed walikuwa wanaishi mjini London wakati Mohammad Ahmed akiwa
na mizizi yake Hargeisa eneo la Somaliland. Watuhumiwa hao watatu
inaarifiwa walikuwa na mawasiliano na wanachama wa kundi la wapiganaji
wa kiisilamu tangu mwezi Disemba mwaka 2012 na walisafiri kwenda mjini
Adama, ambako walikuwa wanapanga kufanya mashambulizi ya kigaidi. Mahakama
kuu mjini Addis Ababa, iliarifiwa kuwa Ali Adros aliingia nchini
Ethiopia kutoka Kenya kwa mafunzo ya kijeshi na kwamba pia alikuwa na
makubaliano na kundi la waasi la (OLF), kufanya mashambulizi nao.
Ni
miaka 26 tangu tuone viatu vikijifunga kamba zenyewe kama ilivyokuwa
kwenye matangazo ya biashara ya viatu vya Nike vyake Marty McFly
vikijifunga miaka hiyo. hio
Hilo lilikuwa tu tangazo la bishara
zamani sana lakini kuna mtu ambaye aliwaza hivyo miaka hiyo na kusema
atakuja kuzindua viatu vyenye uwezo wa kujifunga kamba. Na kwake ndoto
hio imetimia. Wahandisi nchini Ujerumani wamebuni viatu ambavyo vina uwezo wa kujifunga kamba. Walifanikiwa
kufanya hivyo kwa kuweka 'cherger'mfano kama ile ya simu kwenye viatu
hivyo ambavyo vinatumia kawi kujionea wenyewe itakavyokuwa kwenye miguu
tofauti. Pindi unapovaa kiatu hicho, sensa ya kiatu inakiambia
kwamba mguu uko sawasawa na kuchochea kawi kwenye kiatu kile kuamrisha
kamba kujifunga zenyewe. Wakati unataka kuvua viatu utahitajika
kubonyeza au kugonga wayo wa kiatu kile mara mbili na vile vile kuna
miale inayoamrisha kamba za viatu vile kujifungua kwa kuzilegeza kamba. Wanasema
kiatu hicho hakihitaji kuwekwa kwenye charger au kubadilisha betri kwa
sababu kawi inatokana na hatua za kuukanyaga mguu chini kwa mvaaji au
anapotembea zile hatua ndizo zinakipatia kiatu nguvu au kawi. Mmoja wa wahandisi waliokitengeza kiatu hicho, anasema kwamba kiatu hicho kitawasaidia watu wengi. Miongoni
mwa watakaofaidi ni watu wanaokumbwa na ulemavu wa miguu au wenye
matatizo ya kutembea lakini pia vinaweza kuwasaidia watoto au kwa
wanaotaka tu kubadili mfumo wao wa maisha. Saa moja ya kutumia viatu hivyo inatosha kuweza kurejesha kawi ya kufunga kamba. Bwana
Ylli na kikundi cha wahandiisi wengine wanashughulikia kifaa kingine
ambacho kitawezesha viatu kumuonyesha mvaaji mwelekeo anakokwenda.
Waziri wa habari,
vijana, utamaduni na michezo Dkt Fenella Mukangara akizungumza jambo
kwenye hafla fupi iliyoandaliwa na Proin Promotion kwa ajili ya kuzindua
mpango wa kuuza filamu kupitia njia ya mtandao.
Waziri
wa habari, vijana, utamaduni na michezo Dkt Fenella Mukangara akizindua
rasmi mpango wa kuuza filamu zake kwa njia ya mtadao wa kwanza kulia
ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania, Bi Joyce Fissoo pamoja na Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin, Johnson Lukaza(wa kwanza kushoto)
Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin, Johnson Lukaza akizungumza jambo kwenye uzinduzi wa mpango wa kuuza filamu zake kwa njia ya mtandao
Waziri
wa habari, vijana,
utamaduni na michezo Dkt Fenella Mukangara akizungumza jambo baada ya kuzindua
mpango wa kuuza filamu kwa njia ya mtandao. Wa kwanza kulia ni Rais wa shirikisho
la filamu nchi Tanzania (TAFF), Bw. Simon
Mwakifamba na kulia ni Katibu Mtendaji
Bodi ya Filamu Tanzania, Bi Joyce
Fissoo
Waziri
wa habari, vijana,
utamaduni na michezo Dkt Fenella Mukangara akitazama moja ya filamu iliyonunuliwa
kwenye uzinduzi wa kuuza filamu kwenye mtandao wa kwanza kulia ni Katibu Mtendaji
Bodi ya Filamu Tanzania, Bi Joyce
Fissoo
Msanii wa maigizo
Elizabeth Diana Michael "Lulu" akieleza jambo kwa Waziri
wa habari, vijana,
utamaduni na michezo Dkt Fenella Mukangara kwenye uzinduzi wa kuuza filamu kwa kutumia mtandao katikati ni Katibu Mtendaji
Bodi ya Filamu Tanzania, Bi Joyce
Fissoo
Baadhi ya wadau waliofika kwenye hafla hiyo
Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin, Johnson
Lukaza(kulia) akibadishana mawazo na baadhi ya wadau waliofika kwenye
hafla hiyo fupi iliyofanyika jana kwenye Hoteli ya Southern sun ya
jijini Dar
Naibu waziri wa maliasili na utalii MAHAMUOD MGIMWA ambaye ni mbunge wa jimbo la mufindi kusini akiwa ziarani
Na Fredy Mgunda ,Iringa
Naibu waziri wa maliasili na utalii MAHAMUOD MGIMWA ambaye ni mbunge wa jimbo la mufindi kusini amewataka vijana kujituma na kutumia fursa mbalimbali ambazo zinatolewa na serikali.
“Eti asubuhi unawakuta vijana wamekaa kwenye vijiwe wakizungumza siasa na kucheza mabao wakati hawajui mchana watakula wapi na jioni watarudi na nini nyumbani”alisema MAHMOUD MGIMWA
MGIMWA ameendelea kuwaomba vijana wengi wenye fursa ya kurudi au kuingia shuleni upya warudi kwa kuwa dunia ya sasa inataka wasomi wengi kutokana na mabadiliko ya kiuchumi na sayansi na teknolojia na ndio sababu inayopelekea hata watu wazima kurudi shuleni.
“Vijana mnatakiwakujifunza kutoka kwa watu wazima ambavyo wamekuwa wakijituma kufanya kazi kwa bidii na kujituma ilimradi kuwatengenezea watoto maisha mazuri pamoja na kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla”alisema MAHMUOD MGIMWA
Lakini Naibu waziri wa maliasili na utalii MAHAMOUD MGIMWA
ambaye ni mbunge wa jimbo la mufindi kusini amewataka wakinamama kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi wa kumi mwaka huu.
MGIMWA ameeleza kuwa wanawake waondoe hofu ya kugombea hasa kukiwa na ushindani wa wagombea wanaume kwa kuogopa kuchafuliwa kwa mambo yasiyokuwepo.
Ameendelea kusema kuwa wananchi wasishawishiwe na propaganda za wanasiasa na badala yake wachague viongozi bora wenye uwezo wa kuongoza kutoka katika chama chochote.
Aidha ameongeza kuwa viongozi wawe na sera za kutekelezeka ili kuwatendea haki wapiga kura wao hali itakayowafanya waaminike katika jamii.
Mbali na hayo MGIMWA amewakumbusha vijana kutokubali kutumiwa na baadhi ya wanasiasa katika kuleta vurugu hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu na badala yake wachague kiongozi mwenye weredi na sifa za kuwa kiongozi kutokana na sera za chama chake.
Ameendelea kusema kuwa vijana wajitokeze kwa wingi katika kupiga kura ndiyo katika katiba iliyopendekezwa ili kuweza kufanya uchaguzi ulio wa haki na amani pia kujitokeza katika kujiandikisha katika daftari la wapiga kura pamoja na kupiga kura.
Amemaliza kwa kuwataka wananchi wa jimbo la mufindi kusini kuwa na imani nae kwa kuwa amefanya yote ambayo aliwaahidi katika uchaguzi wa mwaka wa 2010 na amewaomba waendelee kuwa na imani naye katika kutekeleza mambo mapya ambayo wamejitokeza kwa lengo la kuleta maendeleo ya jimbo hilo.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na viongozi wa Benki ya Arab Bank for
Economic Development in Africa (BADEA) baada ya kukutana nao kwenye
Ofisini kwake jijini Dar es salaam Januari 16, 2015.Kutoka kushoto ni
Abdulrahman Bin Saleh Al-Otaishan na Abdelaziz Khelef.(Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Waziri
wa Fedha Saada Mkuya (kushoto) akiteta na Kiongozi wa Benki ya Arab
Bank for Economic Development in Africa (BADEA) , Abdulrahm Hassan Naq
baada ya mazungumzo kati ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na ujumbe wa
Benki hiyo, Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Januari 16,
2015.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda na Waziri wa Fedha Saada Mkuya (wapili kushoto)
wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Benki ya Arab Bank for
Economic Development in Africa (BADEA) baada ya mazungumzo kwenye Ofisi
ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Januari 16, 2015.Kutoka kushoto ni
Abdulrahm Hassan Naq,Abdulrahman Bin Saleh Al-Otaishan na Abdelaziz
Khelef.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Meneja
wa Skylight Band Aneth Kushaba AK47 akitoa burudani kwa mashabiki wa
Skylight Band Ijumaa iliyopita kwenye kiota cha Thai Village Masaki
jijini Dar
Kifaa
kipya ndani ya Skylight Band John Music akiimba kwa hisia kaliii huku
akipewa sapoti na Wenzake wa kwanza kushoto ni Baby na wa pili kutoka
kushoto ni Meneja wa Skylight Band Aneth Kushaba AK47 na kulia ni Jessie
Wanaume wa shoka wa Skylight Band kutoka kushoto ni Joniko Flower, Sony Masamba na Sam Mapenzi
wakionyesha mbwembwe zao za kulisakata sebene kwa mashabiki wao, ambapo
jioni ya leo watakuwepo kama kawaida kwenye kiota cha maraha Thai
Village
Jessie(katikati) akiimba kwa raha zakee ndani ya Thai Village akipewa sapoti na Baby pamoja na Aneth Kushaba AK47
John
Music akiiendelea kutoa burudani ya nguvu huku akipewa sapoti na
Wenzake wa kwanza kushoto ni Meneja wa Skylight Band Aneth Kushaba AK47
na wa pili kutoka kushoto ni Baby na kulia ni Jessie
Sam
Mapenzi akiimba Naija Flava njoo leo umshuhudie kwa macho yako…Skylight
Band ndio kila kitu huna haja ya kwenda disco unapata kila kitu hapa
hapa.
Kikosi
kazi cha Skylight Band kikiongozwa Meneja wa Band Aneth Kushaba AK47,
Sam Mapenzi na Sony Masamba kwa pamoja wakiwapa raha mashabiki wa bendi
hiyo (hawapo pichani) kwenye kiota cha maraha cha Thai Village Masaki
jijini Dar Ijumaa iliyopita ambapo leo wataendelea kutoa kuwaburudisha
mashabiki wake kama kawaida kuanzia saa tatu usiku.
Mashabiki
wa Skylight Band wakiburudika na muziki safi kabisa wa ladha na vionjo
vya kila aina ikiwemo Reggae, Kwaito, Naija Flava, R&B, Zouk na
zingine kibao bila kusahau sebene pale kati Joniko Flower anahusika sana
sambamba na Sony Masamba.