Mwenyekiti wa kikundi cha Vijana
Songambele akifurahia jambo pamoja na maafisa kutoka wizara ya
Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo walipokuwa wakizungumza mara baada ya
kuwa tembelea hivi karibuni (wapili kushoto) ni Mkurugenzi Msaidizi wa
Ufuatiliaji na Tathimini Bibi. Verdiana Mushi.
Picha na Anitha Jonas – Maelezo Misungwi
……………………………………………………………………………………..
Na: Anitha Jonas, Maelezo – Misungwi
Vijana wa kikundi cha Songambele
katika Kata ya Misungwi Soko Kuu wameishukuru Serikali kupitia Mfuko wa
Maendeleo ya Vijana kwa kuwapatia mkopo wa shillingi milioni uliosaidia
kuanzisha Mradi wa wakala wa M-pesa katika Wilaya ya Misungwi na Kwimba.
Mwenyekiti wa kikundi hicho Bw. Josephat Mabele alitoa shukrani
kwa niaba ya kikundi chake alipotembelewa na maafisa kutoka Wizara ya
Habari ,Vijana, Utamaduni na Michezo katika eneo la Mradi huo kwa ajili
ya kufanya tathimini na ufuatiliaji kwa Wilaya ya Misungwi,
“Mradi huu wa M-pesa umetusaidia kwa kiasi kikubwa kwani
tunaweza kupata faida ya zaidi ya laki tano kwa mwezi kupitia mradi huu
na hivyo kufanya kipato chetu kukuwa kwa kiasi kikubwa na hata kubadili
hali zetu za maisha”,alisema Bw. Mabele.
Naye Mkurugenzi Msaidizi wa Ufuatiliaji na Tathimini Bi.
Verdiana Mushi kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo
aliwapongeza vijana hao na kuwaasa kuwa makini katika utekelezaji wa
mradi huo kwani biashara ya fedha matapeli ni wengi hivyo ni vyema
kumdai kitambulisho kila mteja anayeenda kwa ajili ya kupata huduma.
Bibi Mushi amewata wanakikundi kuwa na mwongozo mzuri
utakaowasaidia kufanya marejesho ya mkopo huu kwa wakati ili vijana
wenzao nao waweze kunufaika na fursa ya kukopeshwa mkopo kupitia Mfuko
wa Maendeleo ya Vijana.
Kwa upande wake Afisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Bw. Eliakim Mtawa aliwashauri vijana hao kuendeleza
umoja katika kikundi kufikia malengo waliyokusudia na kutoa elimu kwa
vijana wenzao ili waweze kukomboka kama wao walivyojikomboa.
Aidha Afisa Vijana kutoka Halmashauri ya Misungwi Bw. Allan
Jackson alisema kuwa Halmashauri ya Misungwi kwa kushirikana na Misungwi
Vijana Saccoss itaendelea kusimamia vijana hao katika miradi yao na
kuhakikisha wanarejesha mkopo kwa wakati kwa ajili ya kupatiwa vikundi
vingine vya vijana katika Halmashauri yake.
No comments:
Post a Comment