Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dr. Rehema Nchimbi akipanda mti.
…………………………………………………………………………………………………………….
Na George Matiko akiwa Njombe
Wananchi wa Mkoa wa Njombe
wametakiwa kupanda miti kibiashara ili hatimaye kuongeza kipato katika
familia zao. Wameagizwa pia kuitunza miti wanayoipanda na kusubiri
ifikie umri wa kuvunwa ndipo ikatwe.
Maagizo hayo yametolewa na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dr. Rehema
Nchimbi juzi tarehe 10 Januari 2015 alipozungumza kama Mgeni Rasmi
katika maadhimisho ya Siku ya Taifa ya Kupanda Miti katika ngazi ya
Mkoa.
Katika maadhimisho hayo ambayo mwaka huu yalifanyika wilayani
Makete jumla ya miti 3,000 ilipandwa katika kitongoji cha Dombwela
kilichoko katika mji wa Makete.
Dr. Rehema Nchimbi aliitumia fursa hiyo kuagiza Halimashauri
zote za Mkoa wa Njombe kutenga maeneo maalum ya kupanda miti kwa ajili
ya watu wasiojiweza. Miti hiyo itachangia baadaye katika upatikanaji wa
fedha za kuwasomesha watoto wa familia hizo.
Vilevile Mkuu wa Mkoa alizitaka Halimashauri zote za Mkoa wa
Njombe kustawisha miche ya kutosha na kuwapatia wananchi waipande kwa
wingi kwa nia ya kuifanya miti kuwa zao maalum la uwekezaji katika mkoa
huo. Aidaha aliwataka wananchi wa Njombe wanaoishi nje ya mkoa kuwekeza
pia katika mkoa wao husuan katika upandaji miti ili kukuza uchumi mkoani
mwao.
Kwa namna ya pekee Dr. Nchimbi aliwapongeza wananchi wa mkoa
mzima wa Njombe kwa kuwa na utamaduni wa kupandamiti. Hata hivyo
akawataka kuipalilia inapokuwa midogo, kuitunza kitaalam na kuilinda
dhidi ya moto kichaa .
Aina ya miti iliyopandwa katika maadhimisho hayo ni Mizambarao
na Miturunga ambayo inafaa kuhifadhi vyanzo vya maji. Mkuu wa Mkoa
alichagua kupanda miti ya Miturunga kwa kuwa ni miti imara inayotoa mbao
zisizochakaa upesi.
Alipokuwa akipanda mti hiyo Mkuu wa Mkoa alichukua fursa hiyo
kuwataka wananchi wa mkoa wa Njombe, pamoja na kupanda miti ya biashara,
kuviimarisha vyanzo vyote vya maji katika mkoa wa Njombe kwa kupanda
miti inayofaa kuhifadhi maji.
Maadhimisho yaliyofanyika mkoani Njombe ni sehemu ya sherehe za
SIKU Ya TAIFA YA KUPANDA MITI ambazo huadhishwa kitaifa tarehe 1 Aprili
kila mwaka. Kaulimbiu ya mwaka huu nii:‘Panda Miti Kibiashara’.
No comments:
Post a Comment