Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana jana
aliwasili Arusha kwa lengo la kufanya mazungumzo na makundi matatu ya chama cha SPLM ya
Sudani ya Kusini, mashauriano hayo yalilenga kukamilisha makubaliano baina ya
makundi hasimu.
Baada ya Mazungumzo Ndugu Kinana alisema ana matumaini ya kufikiwa makubaliano ya kukiunganisha chama cha SPLM katika siku chache zijazo Kutoka kushoto ni Balozi David Kapya,Abdulrahman Kinana,Mwenyekiti wa Mazungumzo Dk.John Samuel Malecela na Makamu Mwenyekiti wa mazungumzo Dk. Hassan Kibelloh mazungumzo hayo yalifanyika Ngurdoto Arusha. Viongozi wa Makundi matatu kutoka chama cha SPLM kutoka Sudani ya Kusini wakiwa kwenye mazungumzo ya kufikia makubaliano ya kuunganisha chama chao cha SPLM. Hapa wakiwa na viongozi wa Tanzania wanaosaidia kumaliza tofauti na yakiwa yanasimamiwa na Chama Cha Mapinduzi chini ya uongozi wa Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana.
====== ====== ===== =======

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa
Jakaya Mrisho Kikwete alitangaza kuwa Tanzania imekubali kuwa msuluhishi wa
mgogoro wa kisiasa ndani ya chama tawala cha Sudan Kusini cha Sudanese People’s
Liberation Movement (SPLM), mgogoro
ambao ulisababisha kuzuka kwa vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.
Hata hivyo, Rais Kikwete alisema kuwa usuluhishi huo
utakuwa wa kichama na Chama cha Mapinduzi (CCM) ndicho kitaongoza usuluhishi
huo katika mazungumzo yatakayofanyika Arusha na kuwa jitihada hizo za Tanzania
hazitaingilia mazungumzo ya kujaribu kusimamisha mapigano nchini humo
yanayoendelea huko Addis Ababa, Ethiopia.
Rais Kikwete alisema kuwa ulikuwa uongozi wa SPLM na hasa
Mwenyekiti wa Chama hicho, Rais Salva Kiir ambao wameiomba Tanzania kusaidia
jitihada za kisiasa za kupatanisha pande ambazo zinavutana na kutofautiana
ndani ya SPLM wakiamini kuwa mapatano ndani ya chama yatafanikisha kumaliza
mgogoro wa kisiasa katika Serikali ya nchi hiyo ambayo imegawanyika na kusababisha vita vya wenyewe kwa
wenyewe.
Rais Kikwete alitangaza jitihada hizo za upatanishi za
Tanzania wakati alipohutubia maelfu kwa maelfu ya wananchi na kupitia kwao
Taifa kwenye Sherehe ya Kuzima Mwenge wa Uhuru, Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere
na Kilele cha Wiki ya Vijana kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
“Ni fahari kwetu kwamba wananchi wa Msumbiji, Zimbabwe,
Angola, Namibia na Afrika Kusini nao wako huru na tumetoa mchango wetu. Ni jambo la faraja kubwa kwamba nchi yetu
imeweza kupatia hifadhi ndugu zetu wa nchi jirani na hata mbali wakati maisha
yao yalipokuwa hatarini kwa sababu ya kukosekana kwa amani ama kukimbia mateso
ya uongozi wa kidikteta. Ndugu zetu wa Kongo, Burundi, Rwanda, Kenya na Comoro
wanaujua ukweli huo. Na, kwa Uganda tuliwasaidia kuling’oa Dikteta Idd Amin na
Comoro tulisaidia kuunganisha nchi yao tena.”
No comments:
Post a Comment