Dubai
imejinyakulia sifa ya kipekee katika kupima Imani za jamii kwa pochi
iliyoangushwa mtaani,na mara ikarejeshwa kwa mhusika mara moja.
Katika
utafiti uliofanywa na mtengeneza Filamu mwenye asili ya Uingereza
katika mitaa ya Dubai, alijaribu mara arobaini na tano kuidondosha kwa
makusudi na katika kila tukio msamaria aliyeiokota aliirejesha pochi
hiyo kwa mmiliki wake.
Daniel Jarvis, mwenye miaka 26,akiwa
ameificha kamera yake na kurekodi mfululizo wa matukio hayo ya makusudi
akiwa pamoja na rafikiye aliyejipachika jina la utani la 'Digi' ama Dan,
mwenye miaka 25, walibarizi katika viunga vya Downtown na Bur vilivyoko
Dubai,siku za karibuni na kuweka swali je unaweza kuiba Dubai? Kutaka
kuichunguza jamii na kurushwa vipande vyake katika YouTube ambapo mpaka
kufikia jana usiku watazamaji walikuwa ni zaidi ya 70,000 .
Jarvis
aliiambia 7DAYS walishangazwa na utafiti huo na kikubwa
kilichowasangaza ni kwamba waliookota pochi hiyo hawakujishughulisha
kutazama ndani kuna nini? Wakati pochi hiyo ilikuwa imesheni euro za
kutosha na fedha ya Falme za Kiarab dirham kadhaa.
Mtaa wa kwanza
walioufanyia majaribio ni mtaa uliko katika barabra ya Sheikh Zayed
karibu na soko kuu la kibiashara na jirani kabisa na mnara wa Emirates
lakini kila aliyeiona pochi hiyo aliirejesha,lakini baadaye tukafikiri
sababu ya kurejeshwa pochi hiyo kuwa walioko eneo hilo ni matajiri.
Basi
utafiti wetu tukauhamishia eneo la Bur ,Dubai, mahali ambapo
palionekana duni kidogo cha ajabu watu waliendeleza utamaduni ule ule wa
kurejesha pochi kama ilivyo, na hali eliendelea hivyo mara kadhaa.
Jarvis
anasema wameshafanya utafiti kama huo katika mji wa London nchini
Uingereza. Na huko walistaajabu walipoidondosha tu aliyeiokota alianza
kukimbia nayo wa nako hakuna aliyethubutu kuichukua pochi hiyo.
Jarvis,
alivalia suti nadhifu na kuigiza kudondosha pochi anaonekana kwenye
video hiyo anaeleza hisia za kurejeshewa kitu ulichondondosha kuwa ni
raha iliyoje .lakini akaendelea kusema kuwa anadhani vyombo vya habari
hupotosha ukweli,kwakuwa kulikuwa na kichwa cha habari kuwa kuna mtu
alihukumiwa miaka 15 jela kwa kuiba mdoli wenye taswira ya dubu, utafiti
wetu umegundua tofauti na wayasemayo.
Trollstation ina wanachama
wapatao 230,000 na utafiti wao kutoka Falme za Kiarab unaelekezwa Ulaya,
Marekani na hatimaye Afrika .
Inawezekana katika maeneo watakayopita kuvunja rekodi ya Dubai tusubiri wakati uwadie, ni kauli yake Jarvis .
No comments:
Post a Comment