Mbunge wa viti maalumu Iringa mjini RITTA KABATI
……………………………………………………………………………………………
Mbunge wa viti maalumu Iringa mjini RITTA KABATI amewataka
wakinamama kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali katika
uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi wa kumi mwaka huu.
KABATI ameeleza kuwa wanawake
waondoe hofu ya kugombea hasa kukiwa na ushindani wa wagombea wanaume
kwa kuogopa kuchafuliwa kwa mambo yasiyokuwepo.
Ameendelea kusema kuwa wananchi
wasishawishiwe na propaganda za wanasiasa na badala yake wachague
viongozi bora wenye uwezo wa kuongoza kutoka katika chama chochote.
Aidha ameongeza kuwa viongozi wawe
na sera za kutekelezeka ili kuwatendea haki wapiga kura wao hali
itakayowafanya waaminike katika jamii.
KABATI amesema kuwa wanawake
wawemstari wa mbele kuchukua fomu za kugombea na kwamba wasikatishwe
tamaa na baadhi ya watu wanaodhani kwamba wanawake hawawezi kugombea na
kuongoza katika nafasi mbalimbali.
Aidha ameongeza kuwa Jamii iachane
na mitazamo tofauti kwa wanawake wanao jitokeza kugombea nafasi za
uongozi na kuwaasa wanawake wawe na misimamo pindi wanapoingia
madarakani, kujiamini na kutokubali
kutumiwa kama chombo cha starehe.
Mbali na hayo KABATI amewakumbusha
vijana kutokubali kutumiwa na baadhi ya wanasiasa katika kuleta vurugu
hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu na badala yake
wachague kiongozi mwenye weredi na sifa za kuwa kiongozi kutokana na
sera za chama chake.
Ameendelea kusema kuwa vijana
wajotokeze kwa wingi katika kupiga kura ndiyo katika katiba
iliyopendekezwa ili kuweza kufanya uchaguzi ulio wa haki na amani pia
kujitokeza katika kujiandikisha katika daftari la wapiga kura pamoja na
kupiga kura.
No comments:
Post a Comment