………………………………………………………………………..
Watendaji wanaoshughulikia masuala
ya Vijana Mkoa wa Dodoma wameshauriwa kuzingatia masuala nyeti
yanayowahusu vijana kwa kuyapa kipaumbele kwani vijana ndio sehemu kubwa
ya nguvu kazi ya taifa.
Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Deogratius Yenza alipokua akifungua semina ya Maafisa Vijana na Maafisa Ushirika kutoka Wilaya ya Kondoa, Bahi, Chamwino, Mpwapwa, Kongwa, Chemba na Dodoma Mjini kuhusu Sera ya Maendeleo ya Vijana na Mwongozo wa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana leo Mkoani Dodoma.
Bw. Yenza amewataka washiriki wa semina hiyo kusoma Sera ya Maendeleo ya Vijana ili waweze kushauri, kusimamia na kufuatilia shughuli za vijana na kuwajengea uwezo utakaowawezesha kujitegemea na kujiendeleza katika jamii wanayoishi.
“Maafisa Vijana wa kila wilaya muwe na tabia ya kuwajengea uwezo vijana wa wilaya zenu na kuwashauri katika shughuli wanazozifanya ili muweze kutathmini kuona vijana wanachangiaje katika pato la taifa hivyo kuwathamini na kuwaendeleza” amesema Bw. Yenza.
Akizungumza wakati wa ufunguaji wa semina hiyo mwezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa amewataka Maafisa Vijana na Maafisa Ushirika wa Mkoa wa Dodoma kuwaongoza vijana wawe na ari, uwezo na kujiamini katika kushiriki masuala ya kiuchumi na kijamii ili kuweza kuondokana na vijana tegemezi bali kuwa na vijana tutakaowategemea.
Aidha Kaimu Afisa Vijana wa Wilaya ya Chemba Bibi Madlina Kalinganira amesema kuwa kundi la vijana kwa sasa ni kubwa na pesa iliyotengwa katika Mfuko wa Maendeleo Vijana ni ndogo kufikia vijana wote hivyo kuiomba serikali kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuongeza bajeti ya fedha katika Mfuko wa Maendeleo ya Vijana ili vikundi vingine vya vijana vyenye ari na uwezo viweze kupatiwa mkopo huo.
Naye Afisa Ushirika Manispaa ya Dodoma Bw. Massawe Grayson ameiomba Wizara yenye dhamana na Vijana kuendeleza elimu ya kuwahamasisha vijana na kuwapa taarifa ya mfuko huo mara kwa mara kwani vijana wengi hawafikirii jinsi ya kuweka akiba kabla ya kupewa mkopo bali hufikiria kupatiwa mkopo mapema bila kuwa na malengo ya mkopo huo hivyo kuishia kutumia mkopo huo kiholela na kushindwa kurudisha pesa hizo kwa wakati.

No comments:
Post a Comment