WAKAZI wa jiji la Mwanza na
Kanda ya Ziwa wameiomba Kampuni ya Msama Promotions inayoandaa Tamasha
la Pasaka na Krismasi kuwapa nafasi ya upendeleo kwa kuwapelekea
tamasha katika mkoa huo.
Sababu za kupewa kipaumbele katika Tamasha la Pasaka mwaka huu ni baada ya kulikosa Tamasha la Kirismasi ambalo lilifanyika kwenye mikoa ya Mbeya, Iringa na Songea .
Kwa mujibu wa wakazi hao
ambao waliwaomba waandaaji wa matamasha hayo ya injili, Kassim Mtolea
mwanafunzi wa Chuo cha SAUT wanamuomba Mkurugenzi wa Kampuni ya
Msama Promotions Alex Msama na kamati yake kuwafikiria kwa sababu
linashirikisha waimbaji wa Kimataifa.
Mtolea alisema wanamuomba
Msama kuwafikiria zaidi kwa sababu miaka yote tangu limeasisiwa
limekuwa likianzia jijini Dar es Salaam hivyo ni vyema waandaaji
wakabadilika na kulipeleka kwanza Jijini Mwanza.
Aniceth Nyahore ambaye ni
mkazi wa Maswa lalieleza kuwa iwapo tamasha hilo litaanzia Mwanza
litakutanisha mikoa ya Geita, Shinyanga, Mara na Kagera katika
uwanja wa CCM Kirumba na kueneza injili pamoja na burudani.
Nyahore alisema ubora wa
Matamasha hayo unatokana na ushiriki wa waimbaji wa Kimataifa
wanaotoka nchi za Afrika Kusini, Kenya, Uganda, Rwanda na Uingereza
ambao umekuwa ukivutia umati mkubwa wa mashabiki.
Daniel Mkate aliishauri Kamati
ya maandalizi kuzingatia kuanza na mkoa wa Mwanza baada ya kulikosa
Tamasha la Krismasi lililofanyika mwaka jana huku wakazi hao wakiwa na
kiu kubwa.
Sambamba na kuliomba tamasha
hilo mkoani humo pia aliishukuru Kamati ya Maandalizi kwa
kumleta muimbaji Rebecca Malope ambaye alishiriki tamasha la mwaka
juzi.
Aidha Mwenyekiti wa maandalizi
ya tamasha hilo, Alex Msama alikiri kupokea maombi haya ambapo alisema
ni vigumu kutoa maamuzi maana bado ni mapema mno, lakini aliahidi
kuyafanyia kazi.
No comments:
Post a Comment