Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (katikati meza-kuu)
akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Serikali kuunda timu
maalumu ya kutembelea maeneo yaliyosugu kwa utekaji na mauaji ya albino
nchini ambapo timu hiyo inatarajiwa kuanza kazi wiki mbili zijazo kwa
kuanza na mikoa sugu ya matukio hayo ambayo ni Mwanza, Geita, Simiyu,
Tabora na Shinyanga na baadaye itafuata mikoa mingine. Pia Waziri
Chikawe katika mkutano huo, alitangaza kupiga marufuku wapiga ramli wote
nchini kwa kuwa wanasababisha kuendelea kwa matukio ya kinyama
wanayotendewa albino. Hata hivyo, katika mapambano ya kusambaratisha
unyanyasaji huo, waziri huyo alitangaza kushirikiana ipasavyo na
viongozi wa dini pamoja na mashirika ya kijamii ili kusaidia kutoa elimu
kwa wananchi kutokana na uhalifu huo dhidi ya albino. Kulia meza kuu ni
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu na kushoto ni
Mwenyekiti wa Chama cha Albino nchini (TAS), Ernest Kimaya. Mkutano huo
ulifanyika katika ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo, jijini Dar es
Salaam leo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
No comments:
Post a Comment