Mbunge
wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Catherine Magige (kushoto)
akiwasili kuzindua rasmi duka la urembo la ZuRii House of Beauty
linalomilikiwa na mwana Diaspora ambaye pia ni mwanalibeneke Jestina
George Meru (kulia) ndani ya jengo la Dar Free Market jijini Dar es
Salaam jana.
Na Mwandishi Wetu
Mbunge
wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Catherine Magige leo amezindua
rasmi rasmi duka jipya la vipodozi na vitu mbalimbali linalofahamika kwa
jina la ZuRii lililopo katika jengo la Dar Free Market lililopo katika
barabara ya Alli Hassan Mwinyi Jijini Dar es Salaam.
Akizindua
duka hilo ambalo linamilikiwa na mwana Diaspora ambaye pia ni
mwanalibeneke Jestina George, Magige alisema kwamba amevutiwa na namna
Jestina alivyoweza kurudi na kuwekeza nyumbani hali ambayo imeweza
kuzalisha ajira kwa watanzania na kuwa mfano wa kuigwa.
“Kabla
ya yote nachukua fursa hii kumpongeza Jestina kwani ameonesha mfano wa
umuhimu wa kujiajiri hasa kwa wanawake pia huu ni mfano wa kuigwa kwa
wanadiaspora , wengine warudi na kuja kuwekeza nyumbani kwani fursa
nyingi zipo hivyo waje wazitumie” alisema Magige.
Aidha
alitoa rai kwa wanawake wengine hapa nchini ambao wanauwezo wa kuwa na
mitaji ya kuanzisha biashara wajiajiri na kutoa ajira kwa wengine pia
natoa wito kwa watanzania wengine waje katika duka la ZuRii kuja kutoa
sapoti kwa Jestina, alisema Magige.
Wakati
huohuo mmiliki wa duka hilo la ZuRii Jestina alisema kwamba yeye ameona
fursa za kuwekeza nyumbani hivyo ameamua kuzitumia ipasavyo.
“Natoa
wito kwa kwa wanadiaspora wenzangu ni kwamba wasiwe na tabia za kuja
likizo nyumbani nakuinjoi tu fedha zao tu bali wajitahidi kuja kuwekeza
kwani fursa zipo, kuanzisha duka hili ni ndoto yangu ya siku nyingi
hivyo haya ni matokeo ya njozi yangu namshukuru Mungu kwa kutimiza ndoto
hii”.
Mbunge
wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mh. Catherine Magige akikata utepe
kuzindua rasmi duka la ZuRii House of Beauty linalomilikiwa na Mwana
Diaspora ambaye pia ni Blogger Jestina George Meru (anayeshuhudia tukio
hilo).
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mh. Catherine Magige akiingia ndani ya duka hilo mara baada ya kulizindua.
Mmiliki
wa duka la urembo la ZuRii House of Beauty na mwana Diaspora ambaye pia
ni mwanalibeneke Jestina George Meru akitoa maelezo ya baadhi ya bidhaa
zake za urembo ambazo ni original kutoka nchini Uingereza na Marekani
kwa Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mh. Catherine Magige.
Mbunge
wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mh. Catherine Magige akiangalia
bidhaa za urembo wa nywele ndani ya dula la ZuRii House of Beauty
lililopo ndani ya jengo la Dar Free Market linalomilikiwa na Mwana
Diaspora Jestina George Meru.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mh. Catherine Magige akikagua moja ya bidhaa za nywele ndani ya duka hilo.
Mmiliki
wa duka la urembo la ZuRii House of Beauty na mwana Diaspora ambaye pia
ni mwanalibeneke Jestina George Meru akitoa ushauri na maelezo kwa
baadhi ya wateja waliofika dukani kwake mara baada ya kuzinduliwa rasmi
jana jijini Dar.
Raia wa kigeni nao walivutiwa na bidhaa za duka la ZuRii House of Beauty.
Mwanalibeneke Khadija Khalili akiangalia baadhi ya bidhaa ndani ya duka ZuRii House of Beauty.
Wateja
wakiendelea kumiminika na kujichagulia bidhaa mbalimbali vikiwemo
vibanio vya nywele vya wakubwa kwa watoto ndani ya duka ZuRii House of
Beauty.
Mbunge
wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mh. Catherine Magige akizungumza
na waandishi wa habari (hawapo pichani) waliohudhuria uzinduzi huo
uliofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Mmiliki
wa duka la urembo la ZuRii House of Beauty na mwana Diaspora ambaye pia
ni mwanalibeneke Jestina George Meru akimpa mkono wa shukrani ya
kubariki uzinduzi duka hilo Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha,
Mh. Catherine Magige jana jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment