Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amekamilisha
rasmi ziara yake katika mkoa wa Tabora. Waziri Muhongo alifanya ziara
katika mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Tabora lengo likiwa ni kukagua
miradi ya umeme vijijini pamoja na kuzungumza na wananchiWaziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akitoa
maelekezo kwa uongozi wa kijiji cha Tura wilayani Uyui mkoani Tabora
kuhakikisha umefanya mkutano na wananchi ili kufanya makubaliano jinsi
ya kusimamia mradi wa umeme wa kontena ili wananchi waanze kunufaika
mara moja.
Mtendaji
wa kijiji cha Tura wilayani Uyui mkoani Tabora Gundi Igonzo (kulia
aliyevaa koti la kijani) akitoa maelezo juu ya mradi wa umeme wa kontena
kijijini hapo mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter
Muhongo (katikati)
Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akitoa
maelekezo kwa uongozi wa kampuni ya kusambaza umeme katika wilaya ya
Uyui na Mirambo ya Chico – CCC ya China mara baada ya kutembelea eneo
palipohifadhiwa vifaa kwa ajili ujenzi wa miundombinu ya umeme katika
wilaya za Uyui na Mirambo.
Mtaalamu
kutoka Kampuni ya Chico – CCC, Luo Xiaoyong (kulia) akitoa maelezo kwa
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) juu ya
hatua iliyofikiwa ya utekelezaji wa mradi wa kusambaza umeme katika
wilaya za Uyui na Urambo mara Waziri alipotembelea eneo palipohifadhiwa
vifaa kwa ajili ya kazi hiyo.
No comments:
Post a Comment