Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akikabidhi dawa kwa mganga mkuu wa hospitali ya jimbo
la Mpendae Dr. Omar Shaban Amran wakati alipokabidhi sehemu ya madawa
kwa hospitali hiyo ambayo yametolewa na mbunge wa jimbo la Mpendae Mh.
Salum Turki kiasi cha makontena ya dawa manne yenye thamani ya shilingi
Bilioni Moja na pointi Nne yatakayosaidia katika hospitali zote za
Zanzibar, Kinana akiongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na
Uenezi amemalizia ziara yake leo katika mkoa wa Mjini Magharibi wilaya
ya Amani jimbo la Mpendae kabla ya kuendelea na ziara mikoa mingine ya
Zanzibar.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akishiriki kazi ya ukarabati wa barabara kwa
kusambaza kifusi katika barabara inayounganisha hospitali ya Jimbo la
Mpendae na Barabara kuu ya Mchina.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akikiwa ameshikilia toroli huku mbunge wa jimbo la
Mpendae Mh. Salum Turki akijaza kifuzi katika toroli hilo wakati Ndugu
Abdulrahman Kinana aliposhiriki ukarabati wa barabara hiyo.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizindua ofisi ya CCM tawi la
Kilimahewa juu ambalo lilichomwa na wafuasi wa Uamsho wakati wa vurugu
hizo mwaka juzi.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza mbunge wa jimbo la
Chumbuni Mh. Pereira Silima wakati akizungumza katika tawi la Kiungani
ambalo lilitembelewa na Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kazi ya utandazaji wa
mabomba ya mradi wa maji SEMUSO katika kijiji cha Wazee cha mjini
Zanzibar.
Mbunge
wa jimbo la Chumbuni Mh. Pereira Silima akiwa na viongozi wengine wa
CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Bint Amran
Mpendae wilaya ya Amani.
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akijumuika na viongozi hao wakati wa mkutano wa hadhara.
Mlezi
wa CCM Mkoa wa Mjini Magharibi Mh. Shamsi Vuai Nahodha akiwahutubia
wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Bint
Amrani jimbo la Mpendae.
Naibu Katibu Mkuu Zanzibar wa CCM Ndugu Vuai Ali Vuai akiwafafanulia wananchi faida za katiba mpya inayopendekezwa.
No comments:
Post a Comment