……………………………………………………………………………….
Na Anitha Jonas – Maelezo,Nzega
Serikali imewataka vijana kuitumia vyema mikopo wanayopata
katika kuteketeza miradi mbalimbali ya kimaendeleo ili kujikwamua
kiuchumi.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Ufutiliaji na Tathimini
toka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Bi.Verdiana Mushi
wakati alipotembelea Ofisi ya Halmashauri ya Nzega na kwa ajili ya
kukabidhi hundi ya kiasi cha shilingi milioni 21 itakayosaidia kukopesha
vikundi vya vijana walioko chini ya Vijana Saccoss Nzega.
“Serikali inaendelea kutekeleza ahadi yake ya kuwasaidia vijana
kujikwamua kiuchumi kwa kuwapatia mikopo ambayo itawasaidia kutekeleza
miradi mbalimbali ambayo itawaongezea kipato na kuwaondolea umasikini
kwani vijana ndiyo nguvu kazi ya nchi” Alisema Bi.Mushi.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Nzega Bw. Abrahaman Mndeme
ameishukuru serikali kwa kuwapatia mkopo huo vijana wa Nzega kwani kwa
kupitia mkopo huo vijana watafaidika sana na pia watachangia kukua kwa
pato la Halmashauri na kupunguza vijana wanaoka vijiweni na kushauriana
mambo yasiyo na maendeleo katika jamii.
“Uongozi wa Halmashauri kwa kushirikiana na Saccoss ya Vijana
Nzega utasimamia gawio la fedha hizo kwa vikundi husika na kuhakikisha
miradi iliyoandikwa na vikundi hivyo inatekelezwa, pamoja na kufuatilia
urejeshwaji mikopo hiyo kwa wakati ili vikundi vingine viendelee
kunufaika na mikopo hiyo inayotolewa na serikali”,alisema Bw.Mndeme
Akitoa hamasa kwa vijana Afisa Vijana kutoka Wizara ya
Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Bw.Eliakim Mtawa aliwaasa Vijana
kuunda vikundi na kujiunga katika Saccoss za Vijana zilizopo katika
halmashauri zao ili waweze kuomba mkopo utakao wasaidia kufanya shughuli
mbalimbali za kiuchumi badala ya kukaa vijiweni.
“Serikali imedhamiria kwa dhati kuwakomboa vijana kiuchumi kwa
kutambua changamoto ya ajira iliyopo katika taifa letu kwa sasa na dunia
nzima kwa ujumla”,alisema Bw.Mtawa.
Pamoja na hayo naye Mwenyekiti wa Vijana Saccoss Nzega
Bw.Emmanuel Mambo, ameishukuru serikali kwa niaba ya vijana wa Nzega
kupitia Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo na Mfuko wa
Maendeleo ya Vijana kuwapatia fedha hizo walizoomba kwa ajili ya kufanya
miradi mbalimbali ikiwemo ufugaji na kilimo itakayoongeza kipato chao.
No comments:
Post a Comment