TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, October 3, 2014

MAELFU YA WAKAZI WA TUNDURU WAJITOKEZA KUMPOKEA PROF IBRAHIM LIPUMBA

 Wanachama wa Chama cha Wananchi CUF wakiwa katika msafara wa mapokezi ya Mwenyekiti wa chama hicho,Prof Ibrahim Lipumba
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF,Prof Ibrahim Lipumba mwenye shati jekundu na kofia nyekundu akiwapungia mkono wanachama wa chama cha CUF mara tu baada ya kufika katika ofisi za CUF Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma
 Polisi wakiwa katika ulinzi wa Prof Ibrahim Lipumba
Naibu Mkurugenzi wa Oganaizesheni Uchaguzi na Bunge wa Chama Cha Wananchi CUF – Shaweji Mketo akiwahutubia  wakazi wa wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma,kutokufanya makosa  wakati  wauchaguzi wa serikali  za mitaa uliotangazwa  kufanyika Disemba 14 mwaka huu wahakikishe wanakipigia Chama cha Wananchi CUF
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF,Prof Ibrahim Lipumba akiwahutubia maelfu ya wananchi waTunduru waliojitokeza kumsikiliza katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja baraza  la Iddi Tunduru mjini.

RASIMU YA KATIBA MPYA NA WAJUMBE BUNGENI MJINI DODOMA


Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Deo Sanga akisakata muziki katikati ya Ukumbi wa Bunge hilo baada ya kutangazwa kwa matokeo ya kura zilizopigwa kupitisha Rasimu ya Mwisho ya Katiba inayopendekezwa mjini Dodoma jana 

Picha na Edwin Mjwahuzi


Dodoma/Dar.
Licha ya upinzani kutoka makundi kadhaa ya wananchi, Bunge la Katiba jana lilihitimisha kazi yake kwa kupitisha Katiba inayopendekezwa baada ya kupata theluthi mbili za wajumbe wa kila upande wa Muungano.


Matokeo hayo yaliyohitimisha mchakato huo, yalifanikishwa kwa tofauti ya kura mbili za wajumbe katika baadhi ya ibara na nyingine kwa kura moja tu, ikimaanisha kuwa iwapo kura hizo mbili zingekosekana hadithi ingekuwa tofauti.

Kutangazwa kwa matokeo hayo kuliwafanya wajumbe walioshiriki mchakato hadi hatua ya mwisho baada ya wenzao wa kundi la Ukawa kususia, kulipuka kwa furaha, nyimbo, tambo, vijembe na vigelegele huku wakijimwaga ukumbini kusakata dansi.

Akitangaza matokeo hayo, Naibu Katibu wa Bunge hilo, Dk Thomas Kashililah alisema hali ya upigaji kura ilikuwa ni nzuri na kila kura za kila upande zilitosheleza na kutoa uhalali wa Katiba inayopendekezwa kupelekwa kwa wananchi.

Katibu huyo alianza kutoa matokeo ya upande wa Zanzibar ambako wajumbe wengi walikuwa na wasiwasi kuwa huenda usipate akidi ya kura 146 iliyotakiwa.

Kwa jumla, kura za ‘ndiyo’ za Zanzibar zilikuwa ama 147 au 148 na ‘hapana’ ama saba au nane; wakati kwa matokeo ya Tanzania, wajumbe waliopiga kura walikuwa 335 na kura moja tu ndiyo ilikataa ibara zote na kura mbili zilichomoza kukataa baadhi ya ibara.

Matokeo hayo yalithibitishwa na mawakala Amina Makilagi na Waziri Rajabu Salum ambao walisimama na kueleza namna ambavyo kura hizo zilihesabiwa kwa uhuru mpana.

Kuserebuka bungeni
Baada ya matokeo hayo, Ukumbi wa Bunge ulihanikizwa kwa nyimbo za mipasho na mafumbo zikiambatana na kuwashwa vipaza sauti bila ya utaratibu na wajumbe kurukaruka na kukumbatiana kwa furaha.

Hali hiyo, iliwalazimu walinzi wa viongozi kuingia ndani ya ukumbi kwa kuweka hali ya amani kwani wajumbe walianza kuvamia viti vyao kwa nia ya kuwapongeza.

Hali ilipozidi, walinzi wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda walimwondoa haraka na kumweka katika chumba maalumu hadi hali ilipotulia huku idadi kubwa ya walinzi ikisogea kwa Mwenyekiti wa Bunge, Samuel Sitta.

Baada ya kuwatuliza, Sitta alisema walichokuwa wanafanya ni kuvunja kanuni, lakini kwa kuwa mwenyekiti naye alikuwa akicheza basi hakuna tatizo na amewasamehe.

Filikunjombe, Lugora wakwama
Wabunge wawili, Deo Filikunjombe (Ludewa- CCM) na Kangi Lugola (Mwibara-CCM) ambao hawakuwapo wakati wa mchakato, jana waliingia ukumbini lakini Sitta alitangaza kuwa haikuwapo tena nafasi ya kupiga kura.

“Nitangaze leo kuwa hakuna nafasi ya kupiga kura kwa wajumbe ambao hawakupata nafasi hiyo, nasema hivyo kwa kuwa matokeo yote tunayo hapa na hivyo hakuna sababu za kupiga kura tena,” alisema Sitta.

Wakati wa upigaji wa kura, majina ya wabunge hao yalipoitwa wajumbe waliitikia kwa sauti “ukawa haooo”.

Baada ya tangazo hilo, wabunge hao waliamua kuondoka ukumbini na kutokomea. Lugola hakupatikana kwa simu kuzungumzia hali hiyo lakini Filikunjombe alipokea simu na kusema alikuwa kwenye mkutano.

Ukawa: Harakati kuendelea
Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, Freeman Mbowe alisema harakati za kuipata Katiba bora yenye masilahi ya wananchi zitaendelea bila kusimama.

“Tumeona kichekesho na dhihaka iliyotokea Dodoma, kwa mustakabali wa Taifa hili. Ni vyema CCM wakawa makini kutotumia vibaya fursa hii ya kuiongoza nchi kwa kuzingatia hoja na matakwa ya kuipata Katiba, bila kutumia rushwa wala nguvu ya dola.

“Bado tunajadiliana ili tutoe tamko la pamoja. Rasimu iliyopitishwa ina maswali mengi kuliko majibu. Baada ya muda mfupi wa kujadiliana baina yetu tutasema msimamo wetu,” alisema.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Issa Musoke alisema wananchi hawana sababu ya kuikubali rasimu iliyopitishwa kwa kuwa ni batili.

“Rasimu iliyopitishwa ni ya kamati ya uandishi na siyo ya Taifa hili kwa sababu imekiuka kanuni. Rais aliunda Tume ya kukusanya maoni ya wananchi ambayo yangejadiliwa katika Bunge Maalumu la Katiba, kama taratibu zilivyoainisha. Bunge hilo lilikuwa na jukumu moja la kutunga Katiba kutokana na maoni ya wananchi,” alisema na kuongeza:

“Watanzania tumekuwa waoga wa kupitiliza. Hatutaki kusema ukweli hata kama unahitajika. Kwa kilichofanyika ni kwamba wananchi hawakutendewa haki.”

Aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Humphrey Polepole alisema wajumbe wanafurahia kupitisha Katiba inayopendekezwa katika mazingira ya kushindwa.

“Wameshindwa kutupatia Katiba inayotokana na maoni ya Watanzania. Wametoa maoni ya wananchi na kuweka yao. Huwezi kupata Katiba nzuri kama hakuna maridhiano huku mijadala yote ikitawaliwa na itikadi za vyama vya siasa na mizengwe,” alisema.

Alisema kitendo cha Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Othman Masoud Othman kupiga kura ya ‘hapana’ kinaonyesha kuwa Zanzibar imegawanyika zaidi na hilo lilidhihirika baada ya mwanasheria huyo kutaka kupigwa na wajumbe wenzake kutoka huko.

Alisema wajumbe wa Tume hiyo wataendelea kuitetea Rasimu ya pili ya Katiba iliyotolewa na Tume hiyo kwa sababu ilitokana na maoni ya wananchi.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Ardhi (HakiArdhi), Yefred Myenzi alisema Katiba inayopendekezwa ni kichekesho kwa sababu licha ya kupingwa na wananchi wengi, imeongezwa sura mpya ya ardhi ambayo haijajibu mambo manne ya msingi kuhusu ardhi.

Alitaja mambo yaliyokosekana katika sura ya ardhi iliyoongezwa kuwa ni; kutoeleza ardhi inamilikiwa na nani, vyombo vya kusimamia ardhi, mfumo wa matumizi ya ardhi na uhusiano kati ya ardhi na rasilimali nyingine.

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema, “Zoezi la upigaji kura lilikosewa na lilikosa uwazi, hasa kwa wajumbe waliopiga kura kwa njia ya faksi na baruapepe. Ilitakiwa tuelezwe idadi yao kamili pamoja na majina yao ili kujiridhisha kama kweli kura hizo siyo za maruhani.”

Aliongeza, “Kwa kutumia vyanzo vyangu nilifanikiwa kuona kura ya mmoja wa wajumbe waliopiga kwa njia ya mtandao. Kwa jinsi ilivyokuwa, ilikuwa rahisi kwa kura hizo kuchakachuliwa.”

Dk Slaa aliponda kitendo cha wajumbe wa Bunge hilo wakati wakipiga kura, kutamka kuwa wanapiga kura kwa niaba ya kundi fulani kwa sababu kitendo hicho ni kinyume na kanuni za uchaguzi ni sawa na kufanya kampeni.

“Wajumbe wa Bunge la Katiba pia walikosea sana kusema kuwa Katiba iliyopendekezwa imetambua haki za makundi yote bila kuwaeleza wananchi kuwa Ibara ya 20 ya Rasimu ya Katiba inakataza haki hizo kudaiwa mahakamani,” alisema.

Aliyekuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (Saut), Dk Charles Kitima alisema: “Katiba inayopendekezwa ina uhalali wa kisheria lakini inakosa uhalali wa wananchi.

“Haikuwa busara kupuuza maoni ya wananchi na Tume ya Katiba. Katiba hii imepitishwa kwa ubabe wa CCM na watu watambue kuwa siku wananchi wakipata fursa ya kujitawala kidemokrasia wataidai Katiba yao tu.”

Mhadhiri wa Chuo Kikuu Ruaha, Profesa Gaudence Mpangala alisema: “Jambo la msingi si kupata theluthi mbili ya wajumbe kupitisha Katiba. Katiba lazima ipatikane kwa maridhiano na si kwa ubabe kama ilivyotokea Dodoma.

“Unaweza kutumia ubabe katika hatua ya kupiga kura kupitisha Katiba inayopendekezwa, lakini huwezi kutumia ubabe huo katika upigaji wa kura ya maoni. Tangu mwanzo nilipinga mchakato huu kwa sababu watu waligawanyika na ilitakiwa maridhiano yafanyike kwanza.”

Profesa wa Sheria UDSM, Chris Peter Maina alisema: “Utaratibu uliotumika utawagawa wananchi. Katiba haipatikani kwa namba, bali kwa maridhiano. Siombei mabaya lakini ukweli ndiyo huo, hii Katiba itatugawa na si jambo la kushangilia hata kidogo.”

Alisema Katiba inayopendekezwa ni dhaifu kwa sababu haina maoni ya msingi yaliyotolewa na wananchi ambayo yalikuwa katika rasimu iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambayo kwa miezi 20 ilifanya kazi ya kukusanya maoni ya wananchi.

Wakili Mwandamizi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Harold Sungusia alisema: “Nina uchungu sana kwa sababu kwa mara nyingine Tanganyika tumeizika. Hata hivyo, LHRC tunafanya tathmini ya mchakato mzima wa Katiba na tutatoa tamko rasmi.”MWANANCHI

SHIGONGO AZINDUA VITABU VYAKE VIPYA MAREKANI

Vitabu viwili vya Eric Shigongo alivyozindua nchini Marekani juzi.
 
Eric Shigongo akihojiwa na Shaka Ssali (kulia) katika kipindi cha Straight Talk Africa kabla ya uzinduzi huo.
MKURUGENZI Mtendaji wa Global Publishers, Eric James Shigongo amezindua vitabu vyake viwili vipya vya namna ya kuondokana umaskini vyenye majina ya 10 Laws-How to Move From Poverty to Prosperity na 26 Secrets- How to Defeat From Enemies and Make Millions of Dollars.
 
10 Laws-How to Move From Poverty to Prosperity.
Shigongo alizindua vitabu hivyo vya ujasiriamali alipokuwa akihojiwa na Kituo cha Runinga cha Voice of America (Voa) kwenye Kipindi cha Straight Talk of Africa nchini Marekani juzi.
26 Secrets- How to Defeat From Enemies and Make Millions of Dollars.
Kwa mujibu wa Shigongo vitabu hivyo vitakuwa vikiuzwa duniani kote ili kuikomboa jamii kwenye wimbi la umaskini.

Makaa ya Mawe ya Ngaka kuanza kutumika kupikia


169Mtaalamu wa viwango kutoka mgodi wa Ngaka, Boscow Mabena akionyesha tofali maalumu (briquette) zilizobuniwa na mgodi huo kwa ajili ya matumizi ya kupikia majumbani na katika taasisi. Tofali hizo zina uwezo wa kuwaka kwa zaidi ya saa nne.
………………………………………………………………
Na Mohamed Saif – Mbinga
Mgodi wa Makaa ya Mawe wa Ngaka uliopo wilayani Mbinga mkoani Ruvuma upo mbioni kuanza kuuza makaa yanayozalishwa na mgodi huo kwa ajili ya matumizi ya kupikia katika taasisi na majumbani.
Hayo yalielezwa hivi karibuni na Mtaalamu wa Viwango katika mgodi huo, Boscow Mabena alipokuwa akizungumza na ujumbe kutoka Wizara ya Nishati na Madini uliofanya ziara mgodini hapo kwa lengo la kufanya ukaguzi wa kimazingira.
Mabena alieleza kuwa utafiti wa kupunguza joto katika Makaa hayo ili kuweza kutumika kwa ajili ya kupikia umefanywa kwa kushirikiana na kikundi cha kina Mama cha Mbarawala Women Group kilichopo wilayani humo pamoja na Chuo cha VETA- Ruvuma.  
Aliongeza kuwa utafiti huo umefanyika kwa kipindi kirefu na tayari umekamilika na hivi sasa kinachosubiriwa ni kibali kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ili makaa hayo yaanze kuuzwa.
Mtaalamu huyo alieleza kuwa wamebuni tofali maalumu (briquette) kutokana na makaa hayo ambazo zitatumika kwa ajili ya matumizi ya kupikia kwa kutumia majiko maalumu ambayo yamebuniwa na wataalamu kutoka Chuo cha VETA.
Aidha, alibainisha kuwa tofali moja la mkaa huo (briquette) lina uwezo wa kuwaka kwa saa zisizopungua nne na hivyo kumuwezesha mtumiaji kupika vyakula mbalimbali kwa kutumia tofali kimoja.
Kuhusu suala la bei, Mabena alifafanua kuwa kila tofali litauzwa kwa kuanzia shilingi mia mbili na majiko yatatofautiana bei kulingana na mahitaji ya mtumiaji. “Unajua kuhusu jiko, inategemea mtu anahitaji jiko la namna gani, kuna majiko makubwa ya taasisi na pia madogo, hivyo mteja atatuambia anahitaji jiko la namna gani maana tuna uwezo wa kumjengea jiko maalumu lisilohamishika,” alisema.
Mabena alisema matumizi ya mkaa huo yanatazamiwa kupunguza uharibifu wa mazingira hususan ukataji hovyo wa miti kwa ajili ya mkaa na kuni.
Alieleza kuwa, tayari taasisi mbalimbali zimeonyesha nia ya kutumia majiko hayo. Mtaalamu huyo alizitaja baadhi ya taasisi kuwa ni Magereza wilayani Songea pamoja na Chuo cha Ualimu cha Songea. “Tulikuwepo siku ya Maonesho ya Nane Nane hapo Songea na wananchi wengi walivutiwa na mkaa huu na hii ilitusaidia tushike nafasi ya kwanza kwa ubunifu,” aliongeza.

KINANA AWASILI TANGA MJINI

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akivuka na kivuko cha MV.Pangani kuelekea Wilaya ya Tanga mjini ambapo anatazamiwa kukagua miradi mbali mbali na kushiriki ujenzi wa maendeleo,wengine pichani ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (kushoto) na Mwenyekiti wa CCM Pangani Ndugu Hamis Mnegero.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi wa Pangani baada ya kuvuka na MV.Pangani
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi waliojitokeza kumuaga wakati akielekea Tanga mjni.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa kata ya Kigombe ,Pangani ambapo  aliwaeleza lazima kuwa makini katika kuchagua viongozi wa kijiji kwani wengi wamekuwa wakiuza ardhi ya wananchi kiholela na kusababisha matatizo makubwa ya ardhi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa Tanga mjini Mh.Omari Nundu wakati wa mapokezi katika kata ya Marungu wilaya ya Tanga mjini.
 Wananchi wa kata ya Marungu wakifurahia ujio wa Katibu Mkuu wa CCM kwenye kata yao
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimia wakazi wa kata ya Marungu
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea kadi za wanachama wa CUF na Chadema wa kata ya Marungu walioamua kurudi CCM,zaidi ya wanachama 60 wa kata ya Marungu kutoka upinzani wamejiunga CCM .
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha kadi za wanachama
wa CUF na Chadema wa kata ya Marungu walioamua kurudi CCM,zaidi ya
wanachama 60
 Bibi Saumu Ngoma mama mzazi wa Diwani wa kata ya Marungu Ndugu Bakari Mambeya akirudisha kadi ya CUF kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  na kujiunga na  CCM.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kuezeka ofisi ya CCM kata ya Marungu.
 Wazee wa kijiji cha Machui kata ya Tangasisi wakiwa kwenye mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambapo alishiriki kutoa kadi za mfuko wa afya ya jamii na kushiriki ujenzi wa nyumba ya mganga.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akiwasalimu wakazi wa kijiji cha Machui kata ya Tangasisi wilaya ya Tangamjini.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa nyumba ya mganga wa kijiji cha Machui katika kata ya Tangasisi
 Katibu Mkuu wa CCM akisalimiana na Wazee waasisi wa CCM Tanga mjini kwenye mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Tanga mjini.
Mzee Athumani Makalo (wa kwanza kulia) akiwa na wazee waasisi nadi ya ukumbi wa mkutano ambapo Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Tanga mjini.

WAFANYAKAZI WA UNFPA, TUSHIKAME PAMOJA FOUNDATION NA PROJECKT INSPIRE WAONYESHA UPENDO KWA WAZEE MSIMBAZI CENTRE

IMG_2450Daktari kijana Brian Mushi wa Projeckt Inspire akionyesha upendo kwa mmoja wa wazee wanaoishi kwenye kituo hicho kilichopo Msimbazi Centre mara baada ya kumpima Presha wakati wa maadhimisho ya siku ya wazee duniani.
Na Mwandisi wetu
WAZEE wanaoshi katika makazi ya Msimbazi Centre Jijini Dar es salaam karibu na kanisa la Mtakatifu Maria wa Fatma, Msimbazi walipata faraja kubwa baada ya kutembelewa na makundi matatu ya jamii.
Makundi hayo ni pamoja na wafanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) hapa nchini, Tushikamane Pamoja Foundation na madaktari vijana wanaounda kundi la Projeckt Inspire chini ya mradi wa Inspire Healthy.
Makundi hayo yalifika katika kituo hicho katika kuadhimisha siku ya wazee duniani.
Wakiwa na lengo kuu la kuwafariji, kukagua afya zao na kuheshimu uwepo wao, makundi hayo pia yaliwapa zawadi za vyandarua, sabuni za kufulia na kuogea, pampers, Thermos Flask, vikombe vya chai, sahani za kulia, vijiko, sukari, njugu mawe, Tshirts, viatu, nguo, vyombo vya kufanyia usafi .
Pia walipiga picha za pamoja za ukumbusho.
Siku ya Wazee Duniani imetengwa kwa ajili ya kuweaenzi na pia kuwakumbuka kwa mambo waliyofanya kuendeleza kizazi cha wanadamu.
IMG_2514Dr. Brian Mushi wa Projeckt Inspire akimpima presha mmoja wa wazee wanaoishi kwenye kituo hicho.
IMG_2523Dr. Brian Mushi wa Projeckt Inspire akichukua vipimo vya damu kwa ajili ya kupima sukari kwa mmoja wa wazee wanaolelewa kwenye kituo hicho wakati wa maadhimisho ya siku ya wazee duniani.
IMG_2330Wafanyakazi wa UNFPA kutoka kushoto ni Clementina Njau, Mike Mwakuvila na mdau kutoka Tushikamane Pamoja Foundation wakionyesha upendo kwa mmoja wa wazeee wanaoishi kwenye kituo hicho wakati wa maadhimisho ya siku ya wazee duniani.
IMG_2351Dr. Majaliwa Marwa kutoka UNFPA akikabidhi moja ya vyandarua walivyovitoa kwenye kituo hicho kinacholelea wazee Msimbazi Centre wakati wa maadhimisho ya siku ya wazee duniani.
IMG_2383Sehemu ya msaada uliotolewa na makundi hayo.
IMG_2371
IMG_2364Wafanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) hapa nchini wakiongozwa na mtaalam wa mawasiliano kutoka UNFPA, Sawiche Wamunza(kushoto), wadau wa Tushikamane Pamoja Foundation pamoja madaktari vijana wanaounda kundi la Projeckt Inspire chini ya mradi wa Inspire Healthy wakiwa kwenye picha ya pamoja na masista wanaowahudumia wazee hao kwenye kituo hicho.
IMG_2574Wafanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) hapa nchini wakiongozwa na mtaalam wa mawasiliano kutoka UNFPA, Sawiche Wamunza(wa nne kushoto), wadau wa Tushikamane Pamoja Foundation pamoja madaktari vijana wanaounda kundi la Projeckt Inspire chini ya mradi wa Inspire Healthy kwenye picha ya pamoja.
IMG_2579Wafanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) hapa nchini, wadau wa Tushikamane Pamoja Foundation pamoja madaktari vijana wanaounda kundi la Projeckt Inspire chini ya mradi wa Inspire Healthy kwenye picha ya pamoja na mmoja wa wazee wanaoishi kituoni hapo.

Shirika la Nyumba la Taifa lafanya mkutano na wadau wa mabenki Dar

Kaimu Meneja Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa, Sophia Mwema akifafanua jambo kwenye mkutano maalumu ulioandaliwa na Shirika la Nyumba la Taifa wa uendelezaji mawasiliano baina ya NHC na Benki iliyoingia nazo mkataba wa kutoa mikopo ya nyumba. Mkutano huo umefanyika leo New Africa Hotel. (Picha kwa Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii cha Shirika la Nyumba la Taifa)
 Maafisa Mawasiliano na wateja wa mabenki tofauti waliofika kwenye mkutano maalumu ulioandaliwa na Shirika la Nyumba la Taifa wa uendelezaji mawasiliano baina ya NHC na Benki iliyoingia nazo mkataba wa kutoa mikopo ya nyumba, wakifuatilia jambo.
 Watendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa wakifuatilia mkutano huo maalumu ulioandaliwa na Shirika la Nyumba la Taifa wa uendelezaji mawasiliano baina ya NHC na Benki iliyoingia nazo mkataba wa kutoa mikopo ya nyumba.
Maafisa Mawasiliano na wateja wa mabenki tofauti waliofika kwenye mkutano maalumu ulioandaliwa na Shirika la Nyumba la Taifa wa uendelezaji mawasiliano baina ya NHC na Benki iliyoingia nazo mkataba wa kutoa mikopo ya nyumba, wakifuatilia jambo.
Maafisa Mawasiliano na wateja wa mabenki tofauti waliofika kwenye mkutano maalumu ulioandaliwa na Shirika la Nyumba la Taifa wa uendelezaji mawasiliano baina ya NHC na Benki iliyoingia nazo mkataba wa kutoa mikopo ya nyumba, wakifuatilia jambo.
Maafisa Mawasiliano na wateja wa mabenki wakiwasili kwenye mkutano maalumu ulioandaliwa na Shirika la Nyumba la Taifa wa uendelezaji mawasiliano baina ya NHC na Benki iliyoingia nazo mkataba wa kutoa mikopo ya nyumba, wakifuatilia jambo.
 Maafisa Mawasiliano na wateja wa mabenki tofauti waliofika kwenye mkutano maalumu ulioandaliwa na Shirika la Nyumba la Taifa wa uendelezaji mawasiliano baina ya NHC na Benki iliyoingia nazo mkataba wa kutoa mikopo ya nyumba, wakifuatilia jambo.
Maafisa Mawasiliano na wateja wa mabenki tofauti waliofika kwenye mkutano maalumu ulioandaliwa na Shirika la Nyumba la Taifa wa uendelezaji mawasiliano baina ya NHC na Benki iliyoingia nazo mkataba wa kutoa mikopo ya nyumba, wakifuatilia jambo.
Kaimu Meneja Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa, Sophia Mwema akifafanua jambo kwenye mkutano maalumu ulioandaliwa na Shirika la Nyumba la Taifa wa uendelezaji mawasiliano baina ya NHC na Benki iliyoingia nazo mkataba wa kutoa mikopo ya nyumba.
Timu ya maofisa mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa kutoka kulia ni Narindwa Norbert, Olivia,, Bhoke Wambura na Salma Mwinyi, wakijadili jambo kabla ya mkutano huo kuanza.
Maafisa Mawasiliano na wateja wa mabenki tofauti waliofika kwenye mkutano maalumu ulioandaliwa na Shirika la Nyumba la Taifa wa uendelezaji mawasiliano baina ya NHC na Benki iliyoingia nazo mkataba wa kutoa mikopo ya nyumba, wakifuatilia jambo.

MKUTANO WA MAAFISA MIPANGO WAFUNGULIWA RASMI

Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango akisoma hotuba wakati wa mkutano wa mwaka wa wachumi na maafisa mipango unaofanyika jijini Dar es Salaam.
Mgeni Rasmi wa mkutano wa mwaka wa wachumi na maafisa mipango, Balozi Dkt. Matern Lumbanga akizungumza na washiriki wa Mkutano huo kabla ya kuufungua rasmi.
Baadhi ya viongozi wa wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakimsikiliza kwa makini Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (Hayupo pichani). Kutoka Kushoto ni Naibu Katibu Mtendaji (Uchumi Jumla), Prof. Longinus Rutasitara, anayemfuatia ni Bw. Paul Sangawe (Naibu Katibu Mtendaji anayeshughulikia Biashara za Kimataifa na Mahusiano ya Kiuchumi) na Kulia ni Naibu Katibu Mtendaji (Huduma za Jamii na Masuala ya Idadi ya Watu) Bibi Florence Mwanri.
Washiriki wa mkutano wa mwaka wa wachumi na maafisa mipango wakimsikiliza Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (Hayupo pichani).
Baadhi ya viongozi wa wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakimsikiliza kwa makini Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (Hayupo pichani). Kutoka Kushoto ni Naibu Katibu Mtendaji (Uchumi Jumla), Prof. Longinus Rutasitara, anayemfuatia ni Bw. Paul Sangawe (Naibu Katibu Mtendaji anayeshughulikia Biashara za Kimataifa na Mahusiano ya Kiuchumi) na Kulia ni Naibu Katibu Mtendaji (Huduma za Jamii na Masuala ya Idadi ya Watu) Bibi Florence Mwanri.
Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (Kulia) akimpongeza na kumshukuru Mgeni Rasmi wa mkutano wa mwaka wa wachumi na maafisa mipango, Balozi Dkt. Matern Lumbanga mara baada ya kuufungua rasmi mkutano huo.
Washiriki wa mkutano wa mwaka wa wachumi na maafisa mipango wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni Rasmi Balozi Dkt. Matern Lumbanga (katikati waliokaa) pamoja na viongozi waandamizi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
===========================================================
Mkutano wa kitaalamu ambao unawakutanisha wataalamu mbalimbali kutoka tasnia za mipango, uchumi, takwimu na maendeleo, wenye wajibu wa kusimamia uchumi na mipango umefunguliwa rasmi na kuwakutanisha kwa pamoja wakurugenzi wa sera na mipango, maafisa mipango kutoka kwenye wizara, Serikali za Mitaa, idara na wakala wa Serikali, pamoja na taasisi za kitaaluma na watafiti wanaojishughulisha na masuala ya maendeleo na uchumi.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, Balozi (Mstaafu) Dkt. Lumbanga alisema kuwa wachumi na maafisa mipango wana wajibu mkubwa katika kuishauri serikali juu ya njia bora na madhubuti za kupambana na umaskini na kuharakisha maendeleo kwa jamii ya Watanzania.
“Muna dhima kubwa katika kushauri kitaalamu juu ya namna nzuri za kupunguza tatizo sugu la umaskini miongoni mwa Watanzania,” alisema.
Balozi (Mstaafu) Dkt. Lumbanga aliwasihi washiriki kutumia fursa hiyo kujadili kwa kina na kubadilishana uzoefu juu ya sera, mipango na kujenga mtandao wa masuala ya maendeleo ya kitaaluma.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo, Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango alisema kuwa lengo kuu la mkutano huo ni kutoa fursa ya kuwakutanisha kwa pamoja wataalamu hao na kujenga uelewa wa pamoja juu ya uendeshaji wa shughuli mbalimbali za Serikali.
Aliongeza kuwa Mkutano huo, unatoa fursa za kujadiliana kwa pamoja juu ya mafanikio na njia za kukabiliana na changamoto kwa kubadilishana uzoefu na ujuzi kwenye masuala hayo.
“Mkutano huu ni muhimu katika kuimarisha utendaji kazi wa kada hizi kwa minajili ya kusukuma gurudumu la maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini,” alisema Dkt. Mpango.
Kwa mujibu wa ratiba ya mkutano huo, Mada mbalimbali zinawasilishwa kwa kutilia mkazo masuala mbalimbali ya kimaendeleo yanayojitokeza hivi sasa, ambapo mkutano huo unajadili masuala ya Maendeleo ya Tasnia ya Wapanga Mipango (wachumi, maafisa mipango na watakwimu) na Maandalizi ya Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2015/16 – 2020/2021).
Mada nyingine ni pamoja na Mwongozo wa Usimamizi wa Uwekezaji katika Sekta ya Umma ambao una lengo likiwa kuimarisha utendaji, ufanisi na uwajibikaji katika matumizi ya rasilimali za umma zilizotengwa kwa ajili ya miradi na program za maendeleo. Pamoja na mada ya Namna bora ya kujiandaa na Uchumi wa Gesi.
Washiriki wa mkutano huu ni pamoja na wakurugenzi wa sera na mipango, maafisa mipango kutoka kwenye wizara, Serikali za Mitaa, idara na wakala wa Serikali, pamoja na taasisi za kitaaluma na watafiti wanaojishughulisha na masuala ya maendeleo na uchumi.