pira wa miguu ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo waki wa katika picha ya pamoja kabla ya mtanange dhidi ya RAS Simiyu leo katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) mjini Morogoro.
Timu ya Habari SHIMIWI yatoa kipigo kwa RAS Simiyu.
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
29/09/2014
Timu ya mpira wa miguu ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo imejiweka kwenye nafasi nzuri ya kusonga mbele katika
mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Watumishi wa Wizara na Idara za
Serikali (SHIMIWI) yanayoendelea mjini Morogoro.
Wakicheza kwa kuonana timu hiyo ikiongozwa na Nahodha wao Carlos
Mlinda walilisakama lango la wapinzani wao RAS Simiyu ambapo katika
kipindi cha kwanza mcheza aliyevalia jezi yenye namba 11 Erick Mfugale
aliwapatia goli la kuongoza kwa kipindi cha kwanza hadi mapumziko.
Kipindi cha pili kilinza kwa timu zote kusaka ushindi ili kujihakikishia hatua inayofuata.
Dakika ya saba ya kipindi cha pili mchezaji aliyevalia jezi
namba 8 Maurus Ndenda ndiye aliwanyanyua mashabiki wa timu ya Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa kufunga goli la pili kwa shuti
kali na kuingia wavuni.
Hadi kipenga cha mwisho cha mwamuzi wa mchezo huo Ramadhani
Omari, timu ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imeshinda 2
na RAS Simiyu hawajapata kitu ambapo ubao wa matokeo ulisomeka (Habari
2-Simiyu 0).
Aidha kwa upande wa mpira wa pete timu ya Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo leo bahati haikuwa yao wamefungwa goli 39
kwa 10 na wapinzani wao Wizara ya Ardhi, Nyumba Na Maendeleo ya Makazi.
No comments:
Post a Comment