TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 30.09.2014.
- KIKONGWE WA MIAKA 90 AUAWA KWA KUKATWA NA KITU CHENYE NCHA KALI WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA
- MWANAFUNZI WA DARASA LA SITA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUANGUKIWA NA KIFUSI CHA MCHANGA.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
KIKONGWE MWENYE UMRI WA MIAKA 90
ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA BAPONDO NGAO MKAZI WA KIJIJI CHA UKWILE
WILAYANI MBOZI ALIUAWA KWA KUKATWA NA KITU CHENYE NCHA KALI SEHEMU ZA
KICHWANI NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA.
MWILI WA MAREHEMU UMEKUTWA MNAMO
TAREHE 29.09.2014 MAJIRA YA SAA 10:00 ASUBUHI HUKO KATIKA KIJIJI UKWILE,
KATA YA ISANDULA, TARAFA YA VWAWA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA.
INADAIWA KUWA, WATU HAO WALIMVIZIA MAREHEMU AKIWA AMELALA NDANI YA
NYUMBA YAKE NA KISHA KUMVAMIA NA KUANZA KUMKATAKATA NA KUPELEKEA KIFO
CHAKE.
CHANZO CHA MAUAJI HAYO BADO
KUFAHAMIKA. MWILI WA MAREHEMU UMEKUTWA NA MAJERAHA MAKUBWA MAWILI YA
KUKATWA NA KITU CHENYE NCHA KALI SEHEMU ZA KICHWANI. MAREHEMU ALIKUWA
ANAISHI PEKE YAKE MAENEO YA MASHAMBANI UMBALI WA ZAIDI YA KILOMITA TANO
[05] KUTOKA MAKAZI YA WATU.
HAKUNA MTU/WATU WALIOKAMATWA KUHUSIANA NA TUKIO HILI, MSAKO MKALI UNAENDELEA KUWATAFUTA WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO ILI AZITOE
MARA MOJA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAHUSIKA WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE
MKONDO WAKE.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MWANAFUNZI WA DARASA LA SITA
KATIKA SHULE YA MSINGI SANZYA WILAYA YA MOMBA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA
VALIUD SIAME@KIMUNDE (13) MKAZI WA KIJIJI CHA KAONGA ALIFARIKI DUNIA
BAADA YA KUANGUKIWA NA KIFUSI CHA MCHANGA.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE
29.09.2014 MAJIRA YA SAA 13:00 MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI CHA KAONGA,
KATA YA CHILULUMO, TARAFA YA KAMSAMBA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA.
INADAIWA KUWA, WAKATI TUKIO HILO LIKITOKEA MAREHEMU ALIKUWA NA WANAFUNZI
WENZAKE WAKICHIMBA NA KUBEBA MCHANGA KWA AJILI YA UJENZI WA NYUMBA ZA
KULALA WAALIMU SHULENI HAPO.
MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI WA KITABIBU NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
WAZAZI/WALEZI KUWA MAKINI KWA KUTOA UANGALIZI WAKUTOSHA IKIWA NI PAMOJA
NA KUWASIMAMIA WATOTO KATIKA SHUGHULI WANAZOWATUMA KUFANYA ILI KUEPUKA
MADHARA YANAYOWEZA KUEPUKIKA.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment