Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam, Said vMeck Sadick (kulia) akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar es jana juu ya kufanyika kwa maonyesho ya utalii
yanayoratibiwa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB). Picha: MPIGAPICHA WETU
Na Mwandishi Wetu
ONESHO la kimataifa la utalii ‘Swahili International Tourism Expo’
(SITE) linaloandaliwa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) linafunguliwa
rasmi leo (kesho Jumatano) katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City na
litamalizika Jumamosi.
Tayari maandalizi yote kuelekea
ufunguzi wa onesho hilo yamekamilika na kwamba watanzania wametakiwa
kujitokeza kwa wingi kuja kujionea vivutio adhimu wa taifa hili.
Shirika la Hifadhi ya Taifa
(TANAPA), Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) pamoja na
Shirika la Ndege la Ethiopia ndio wadhamini wa onesho hilo
linalotarajiwa kushirikisha mataifa mbalimnali ulimwenguni.
Wadhamini wengine ni pamoja na
Zanzibar collection, Hoteli za Sea Cliff, Serena hotel, Southern
Sun,NewAfrica, Hyatt Regency,Protea, Serena hotel, Bouganvillea Safari
lodge, Acacia Farm lodge na Soroi Tented Camp zimedhamini huduma ya
malazi kwa wageni maalumu.
Pamoja na washiriki wengine
onesho hilo linatarajiwa kushirikisha wafanya biashara wakubwa na
watalii kutoka Marekani, Uingereza, Ujerumani pamoja na wandishi wa
habari wa kimataifa wanaokuja kwa ajili ya onesho hilo.
Wakati Wizara ya Mambo ya Nje na
Uhusiano wa Kimataifa ikitoa udhamini wa mabasi ya kubebea washiriki
wakati wa onesho hilo, benki ya CRDB imetoa udhamini wa fedha taslimu na
inatarajiwa kuwa na banda ndani ya maonesho hayo ya aina yake.
Usafiri wa ardhini utadhaminiwa
na makapuni Zara Tours, Naeda Safaris Ltd, Wildlife Expedition Safari,
huku Azam Marine wakijitokeza kudhamini usafiri wa baharini kutoka
Zanzibar. Mashirika ya ndege ya Rwandair, Precision Air na Uturuki
(Turkish airline) yatatoa tiketi za ndege kwa ajili ya kuwasafirisha
baadhi ya wageni wakati wa onesho hilo.
Makampuni mengine yaliyojitokeza ni yale yanayomiliki majarida. Haya ni Event, Dar Life na 7th Floor Media kutoka hapa nchini na Go Places kutoka Kenya, ambavyo wanatangaza onesho hili kupitia majarida yao.
Aidha kampuni ya Montage imetoa udhamini wa kuwa mpambaji katika kumbi za mikutano.Boogie woogie pia wametoa udhamini na watakuwa na mgahawa wao wa chakula katika banda la utalii wa utamaduni ilhali wadhamini wengine Black Tomato wao watakuwa na banda la kuuza kahawa ya Tanzania.
‘Swahili International Tourism Expo’ litakuwa likifanyika kila mwaka mnamo mwezi wa Oktoba na kuhudhuriwa na washiriki kutoka ndani na nje ya Tanzania.
No comments:
Post a Comment