TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, November 22, 2011

LAKAIRO MWANZA YADHAMINI MISS UTALII VYUO VIKUU KANDA YA KATI 2011-2012


 Hoteli ya kitalii ya Lakairo Hotel ya jijini Mwanza,imejitokeza kudhamini shindano la Miss Utalii Vyuo Vikuu - Kanda ya kati,lililopangwa kufanyika Dodoma siku ya uhuru tarehe 9-12-2011. 

Akithibitisha udhamini huo, mkurugenzi wa hoteli hiyo inayomilkiwa na Mheshimiwa Lameck Okambo Airo mbunge wa wa jimbo la Rorya,Daniel Airo alisema kuwa hoteli hiyo inatoa jumla ya shilingi lakitano (500,000/=) kwa ajili ya kuchangia zawadi za washindi wa shindano hilo,linaloshirikisha wanafunzi wa vyuo vikuu vilivyopo mikoa ya kanda ya kati,ikiwemo mikoa ya Dodoma,Singida na Tabora. Daniel alisema kuwa wameamua kudhamini shindano hilo kwa kutambua umuhimu na mchango wake katika kukuza sekta ya utalii nchini,aliongeza kuwa ushiriki wa wanafunzi wa vyuo vikuu katika shindano hilo ni fulsa nyingine ya pekee ya kukuza utalii wa ndani ,kwani iwapo wasomi hao wakihamasika na suala zima la utalii hususani utalii wa ndani basi ni rahisi jamii kuiga na kufuata mfano wa wasomi hao,ambao pia ndio viongozi watarajiwa katika nyanja mbalimbali nchini baada ya kuhitimu masomo yao.

Wadhamini wengine waliojitokeza kudhamini shindano hilo ni Duka la mavazi na vipodozi la Happy Fashion wanaotoa zawadi yenye thamani ya shilingi laki tatu (300,000/),Master Pub , NAM Hotel,Becko Qulity Centre wanatoa zawadi yenye thamani ya laki tatu kwa mshindi wa vipaji,New Soft Saloon,CF Communication & Stationary, Club 84 na Royal Village Hotel,PAPA MSOFE.

Washindi wa 1-5 na wa taji la vipaji watawakilisha Vyuo vikuu kanda ya kati katika fainali za taifa za Miss Utalii Tanzania 2011/12 zilizopangwa kufanyika mwezi February 2012, ambapo washindi wa taifa watawakilisha Tanzania katika mashindano ya dunia ya Miss Tourism World,Miss United Nations,Miss Tourism United Nations,Miss Heritage World,Miss Globe International,Miss Tourism University World na United World International Pageant

WASHIRIKI MISS UTALII VYUO VIKUU KANDA YA KATI DODOMA-KATIKA MAPOZI

























Picha zote ni baadhi ya washiriki miss utalii vyuo vikuu kanda ya kati Dodoma 2011, wakiwa katika maandalizi ya Fainali zitakazofanyika siku ya tarehe 9 mwezi wa kumi na mbili.(picha zote na Shaaban Mpalule)

REDDS FASHION SHOW ILIVYOKUWA MJINI DODOMA NDANI YA ROYAL VILLAGE-WANAUME





Mashindano haya ya Redds Fashio show yalifana na kumalizika bila mizengwe, je ungekuwa ni wewe umepewa kazi ya kuwa mwamuzi ungemchagua nani?(Picha Zote na Shaaban Mpalule-DODOMA).

REDDS FASHION SHOW ILIVYOKUWA MJINI DODOMA NDANI YA ROYAL VILLAGE





shindano la kumtafuta mkali wa mitindo lilimalizika mjini dodoma hivi karibuni ambapo idadi lukuki ya watazamaji walijitokeza siwezi kusema ni kwa sababu ya kutokuwa na kiingilio lakini watu walikuwa ni wengi na shoow ilifana vilivyo mimi nikiiwa shahidi namba moja kama unavyoona katika picha hizi(Picha Zote na Shaaban Mpalule DODOMA)

kuzaliwa Sekela Jakobo Mwaipungu iliyofanyika Dodoma jana

 Sekela Jakobo Mwaipungu, akiwa katika utulivu wakati wa sherehe yake ya kuzaliwa jana
 Emmanuel G. Msangi(kulia) akiwa na ndugu na jamaa katika hafla ya kuzaliwa kwa Sekela Jakobo Mwaipungu, iliyofana jana
 Marafiki wa Sekela Jakobo Mwaipungu, wakiwa katika sherehe hiyo
 Emmanuel G. Msangi akiwa kwenye sherehe ya rafiki yake kipenzi Sekela Jakobo Mwaipungu jana.
 Hii ndiyo keki ya Sekela Jakobo Mwaipungu
 Sekela Jakobo Mwaipungu, akikata keki hiyo
 Sekela Jakobo Mwaipungu, akimlisha mgeni Rasmi ambaye alikuwa Rais wa Miss Utalii Tanzania, Ndugu Gideon Chipungahelo
 Sekela Jakobo Mwaipungu, akimlisha keki Rafiki yake Kipenzi Emmanuel G. Msangi
 Mgeni Rasmi Gideon Chipungahelo akimlisha keki mtoto Sekela Jakobo Mwaipungu.
 Mtoto Sekela Jakobo Mwaipungu, akikabidhi keki kwa mdogo wake, OLGA
Mtoto Sekela Jakobo Mwaipungu, akinong'oneza jambo na dada yake-HELLEN

MISS UTALII VYUO VIKUU KANDA YA KATI KATIKA PICHA, WALIPOSHINDANA KATIKA TUZO YA KIPAJI CLUB 84.


 Picha zote za juu ni washiriki wa Miss Utalii Vyuo Vikuu Kanda ya kati waliposhindana kutafuta washindi watano watakaowania tuzo ya mshindi wa kipaji
 washiriki wa Miss utalii Vyuo Vikuu kanda ya kati Dodoma walipotembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano(katikati ni Mwandishi na mpiga picha  Maarufu nchini Shaaban Mpalule).
Baadhi ya washiriki wa Miss Utalii Vyuo Vikuu wakiwa na walimu wao Jamida Abdul na Mariam Hamisi(picha zote na shaaban Mpalule)