Timu ya Kata ya Rasibura wakikabidhiwa Kikombe na Kamanda wa Mkoa wa Lindi kutoka Takukuru Ndg. Chami baada ya Kuibuka washindi kwa kuifunga Timu ya Kata ya Makonde.
Hashimu
Hamisi au D7 (anaefananishwa na Cristiano Ronaldo) akiwa na tuzo yake
baada ya kuibuka mshindi wa Mchezaji Bora wa Mashindano ya RPC - CUP
2016 akiichezea Timu ya Kata ya Mnazi Mmoja.
Kikundi
cha Ushangiliaji kutoka Rahaleo kikikabidhiwa Zawadi yao mara baada ya
kuibuka washindi wa kwanza katika Ligi ya RPC - CUP 2016 ambayo
imemalizika leo hii ndani ya uwanja wa Ilulu.
Na. Fungwa Kilozo, Lindi
Michuano ya Kombe la RPC-CUP Lindi 2016 imemalizika ambapo mchezo wa fainali umezikutanisha timu mbili za kata ya Makonde na Rasibura zote zikitokea Manispaa ya Lindi.
Mchezo huo ulioshuhudiwa na Mashabiki lukuki kutoka katika pande mbalimbali za Manispaa hiyo ulivuta hisia ya kipekee kwani timu hizo zilikuwa katika Kundi moja kabla ya fainali hiyo ambapo mchezo wa awali timu ya Makonde iliibuka kidedea lakini leo mambo yamekuwa ndivyo sivyo.
Fainali hiyo ilianza kurindima mnamo majira ya saa Kumi kamili za Jioni na hadi Kipyenga cha mwisho cha Mwamuzi wa mchezo huo kinapulizwa kuashiria mchezo umemalizika hakuna Timu iliyoona lango la mwenzie na kuamriwa kupigwa kwa mikwaju ya penati.
Wachezaji wa Makonde hawakuweza kuzitumia vizuri kwani waliweza kupata mkwaju mmoja tu kati ya Nne ya zile zilizo pigwa na Timu ya Rasibura kuweza kuitumia vizuri mikwaju hiyo kwani waliweza kufunga penati zote Nne na kuibuka washindi wa Fainali hizo.
Kamanda wa Mkoa wa Lindi kutoka Takukuru Ndg. Chami ambaye alikuwa ndiye mgeni rasmi wa Mchezo huo aliweza kukabidhi zawadi mbalimbali kutoka kwa washindi mbalimbali wa fainali hizo.
Zawadi ya Mshindi wa Tatu ilikwenda
kwa Timu ya Kata ya Mingoyo na kuweza kupata zawadi ya Medali za Shaba
na Pesa kiasi cha Tsh 400,000.00 huku Mshindi wa pili ikienda kwa Timu
ya Kata ya Makonde na kuweza kupata Medali ya Fedha na Pesa Tsh
600,000.00 pamoja na Kikombe.
Mshindi wa kwanza aliweza kuzawadiwa
Kikombe Medali ya Dhahabu pamoja na Pesa tasilimu Tsh Milioni Moja
(1,000,000.00).
Hata hivyo zawadi zingine zimekwenda kwa Mfungaji BoraMchezaji bora, Kipa Bora, chini ya udhamini kutoka kwa Big Bon, Mashujaa Radio, Mpalule Blogs, Pimak LTD, GSM, Haloteli, Miss Demokrasia Tanzania, Balozi wa Demokrasia Tanzania, Mellenium Buss Service.
Kikosi
cha Kwanza cha Timu ya Kata ya Makonde Kilichocheza mechi ya Fainali
dhidi ya Timu ya Kata ya Rasibura leo hii ndani ya Uwanja wa Ilulu.
Kikosi cha Kwanza cha Timu ya Kata ya Rasibura Kilichocheza mechi ya Fainali dhidi ya Timu ya Kata ya Makonde leo hii ndani ya Uwanja wa Ilulu.
Waamuzi wa Mchezo wa Fainali ya RPC - CUP 2016 Leo hii.