TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, June 20, 2013

MATUKIO KATIKA MITAA YA JIJI LETU DAR ES SALAAM.

 Mcheza Shoo wa Mashujaa Musica, Mdogo wa Nyakwela, akibadili maarifa kwa kuburudika na mchezo wa Pool
 Mkazi wa jiji la Dar es Salaam, akiwa kauchapa Usingizi majira ya saa tisa usiku katika mabanda ya wafanyabiashara huko Vingunguti, hali inayoonyesha ni kwa kiasi gani ugumu wa maisha unavyowasumbua vijana mbalimbali hapa nchini, Serikali iangalie namna ya kupunguza Ukali na Ukata mbalimbali nili kuondokana na hali hii.
 Mtoto Callen Paul Siboka, anayetafsiliwa kuwa Mtoto mwenye akili nyingi ukilinganisha na waotot wengine, ni mkazi wa jiji la Dar es Salaaam.
Mfadhili wa Wanamuziki wa Mashujaa Bendi, akijaribu kuelezea kikubwa kinachomgusa kusaidia wanamuziki kwa kiasi chote katika maisha haya ya kila siku.
(Picha Zote kwa Hisani ya Miss Demokrasia Tanzania).

MASHUJAA MUSICA YAPAGAWISHA WAKAZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM, WAMIMINIKA vINGUNGUTI- LEO NI SANSIRO SINZA

 Shabiki wa Musiki wa Dance na Mkereketwa wa Mashujaa Musica, China, akisakata Rhumba
 Wacheza Shoo wa Bendi hiyo(kutoka kushoto) , Veronica Deogratius , Koku Kibangu, Suzy Manzaka, na Sweety Beby, wakipagawisha mashabiki
 Wanamuziki wa Mashujaa Musica, wakicheza wakati wa Onyesho hilo, kutoka kulia) Raja Radha, Pasia Bundansi(Kengele), Masooud na Jado Fid, 
 Jado Fid
 Rais wa Bendi Mkongwe, Charles Baba, akipagawisha mashabiki wake
 Rais wa Bendi ya Mashujaa Charles Baba, akitumia mwanya pia kuwasikiliza mashabiki wake kile wanachotaka(kushoto ni Shabiki nguli wa Bendi hiyo- AISHA MATATA
 Mashabiki waliojitokeza katika onyesho hilo wakijitokeza kuingia kusakata Rhumba.
 Rais wa Bendi hiyo Charles Baba na Masoud wakionyesha Pozi baada ya kazi kubwa
 Shabiki na Moja ya wafadhili wa Mashujaa Bendi, Mzee wa Vingunguti, akiwa katika moja ya machafuzi katika uwanja wa Mashujaa Pub. kushoto ni DJ'S mkali wa Mashujaa. kijana wa Kihiyo.
 Mkali wa Music, wa Bendi ya Mashujaa akionyesha Vidole 5 kama ishara ya TUZO tano.
 Masouud bingwa wa kuimba, akiwapa raha mashabiki wake katika ukumbi wa Mashujaa Pub
Mkali wa kucheza Tanzania na Afrika nzima, Star wa kunengua, Sweety Baby akiwa katika Onyesho la Jana katika Ukumbi wa Mashujaa Pub.(Picha Zote kwa Hisani ya Miss Demokrasia Tanzania).

Tuesday, June 18, 2013

KAZI ZA WASANII ZIPEWE KIPAUMBELE-WADAU WA SANAA WASEMA

Watu wote wanao fanya kazi za kuandaa matamasha na Burudani mbalimbali wametakiwa kuwapa haki zao wasanii wote wanaofanya kazi za Sanaa mbalimbali hapa nchini, hayo yamesemwa na baadhi ya wadau wa Muziki na Sanaa mbalimbali kutokana na wasanii wachanga kutopewa haki zao mara baada ya kufanya shuguli zao jukwaani.Pichani ni baadhi ya Vikundi vya Sanaa wakiwa katika moja ya Majukwa ya kazi zao.
(Picha kwa Hisani ya Miss Demokrasia Tanzania)

SAFARI YA MAZIKO YA NDUGU YETU MPENDWA LANGA KILEO-KINONDONI DAR ES SALAAM

 Mwili wa Langa Kileo ukiwa katika Kaburi muda mfupi kabla ya maziko.
 Wazazi wa Langa wakiwa katika masikitiko wakati wa maziko
 Jeneza la Mwili wa Msanii wa Muziki Langa Kileo
Wazazi wa Langa wakitoa Heshima za Mwisho(kuweka Udongo) wakati wa kufukia Mwili wa Mpendwa Mwana wao  na ndugu yetu Mwanamuziki Langa Kileo katika Makaburi ya Kinondoni Dar es Salaam
 Baadhi ya ndugu na Marafiki wa Karibu wakitoa Heshima za Mwisho kwa kuweka Udogo katika Jeneza wakati wa maziko ya Langa.

 Ndugu na Rafiki wa Mwanamuziki Langa wakiwa katika Masikitiko wakati wa kuuzika mwili wa Marehemu
 Ndugu wa Mwanamuziki Langa akiwa katika Masikitiko makubwa wakati wa maziko ya ndugu yake
 Wakereketwa na mashabiki, ndugu na jamaa wakishuhudia Mwili wa Langa ukiingizwa Kaburini
 Baadhi ya wasanii wakiwa makundi makundi katika kujadili ili na lile wakati wa maziko
 Vijana wakazi  wa Dar es Salaam na Mashabiki wa Muziki wa ndugu Langa wakijadili jambo wakati wa maziko ya Mwanamuziki huyo

Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza kusindikiza mwili wa ndugu yetu Langa katika Makaburi ya Kinondoni Dar es Salaam.
(Picha Zote kwa Hisani ya Miss Demokrasia Tanzania).