TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Saturday, December 29, 2012
Tanzania haiwezi kukwepa maendeleo ya bioteknolojia ya utandawazi duniani
Naibu
katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Eng. Ngosi Mwihava akifungua Warsha
kwa maafisa wa mipakani kuhusu usimamizi wa mazao na bidhaa zitokanazo
na Bioteknolojia ya kisasa. Kulia ni Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya
Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Julius Ningu na kushoto ni Afisa Mazingira
Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi Esta Makwaia. Warsha hii imefanyika leo
kwenye Hotel ya La kairo jijini Mwanza
Washiriki
wa Warsha ya Usimamizi wa mazao na bidhaa zitokanazo na bioteknolojia
ya kisasa wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi (katikati) Mara
baada ya kufungua warsha hiyo kwenye Hoteli ya La kairo Jiji Mwanza
…………………………………………….
Lulu Mussa na Ali Meja
Mwanza
Imeelezwa kuwa Tanzania kama nchi
nyingine haiwezi kukwepa maendeleo ya bioteknolojia kutokana na
utandawazi na maendeleo duniani kote, kwa kuwa bioteknolojia ya kisasa
ni nyenzo muhimu katika kukuza uchumi na kupunguza umaskini, kuboresha
kilimo, uzalishaji viwandani, afya na hifadhi ya mazingira.
Hayo yamesemwa leo na Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Eng. Ngosi Mwihava katika warsha ya
siku moja kwa maafisa wa mipakani kutoka mikoa ya kanda ya ziwa, warsha
iliyolenga kukuza uelewa kwa watendaji wanaosimamia mazao na bidhaa
zitokanazo na bioteknolojia ya kisasa.
Amesema, Serikali kwa kutambua
mchango mkubwa unaoweza kupatikana kutokana na matumizi ya bioteknolojia
ya kisasa katika sekta za afya, kilimo, viwanda na mazingira, imeridhia
Itifaki ya Cartagena ya Mkataba wa Bioanuai mwaka 2003 kwa lengo la
kuhifadhi mazingira kwa kuzingatia usalama katika usafirishaji, kuunda
na kupitisha mfumo wa kitaifa wa usimamizi wa matumizi salama ya
Bioteknolojia mwaka 2007.
Eng. Mwihava amewaasa watendaji
katika maeneo ya mipakani kuwa na usimamizi madhubuti katika maeneo yao
ya kazi kwa kuwa mipaka kati ya Tanzania na nchi nyingine ndiyo njia kuu
za uingizaji wa mazao na bidhaa zitokazo nje.
Pamoja na faida za bioteknolojia
hiyo ya kisasa Eng. Mwihava amewataka watendaji hao kuwa makini na
athari zinazoweza kutokana na matumizi ya teknolojia hiyo pale
itakapotumiwa bila kufuata taratibu za usalama zilizowekwa.
Warsha hii ya siku moja kwa
imewashirikisha maafisa forodha, Maafisa Afya na watafiti wa Mazao
kutoka Mikoa ya Mwanza, Mara na Kagera, kutoka Idara , wakala za
Serikali na sekta binafsi.
KUTANO WA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO TASWA WAFANYIKA BAGAMOYO LEO
Mwenyekiti
wa kamati ya Kusaidia timu ya Taifa ya Vijana Serengeti Boys Bw.
Ridhiwan Kikwete akifungua mkutano mkuu wa chama cha waandishi wa
habari za michezo TASWA unaofanyika kwenye Hoteli ya Kiromo View
Bagamoyo mkoani Pwani ambao unajadili mambo mbalimbali ya Maendeleo na
changamoto zinazokabili chama hicho.
Waanishi wa habari za michezo ambao ni wanachama kutoka vyombo mbalimbali nchini wanahudhuria mkutano huo ambao ni wa siku moja.
Mwenyekiti
wa Chama cha waandishi wa habari za michezo TASWA Bw. Juma Pinto
akimkaribisha mgeni rasmi ili kufungua mkutano huo leo asubuhi
unaofanyika kwenye hoteli ya Kiromo View Bagamoyo.
Katibu
wa Chama cha Waandishi wa habari za michezo TASWA Bw. Amir Mhando
akizungumza katika mkutano huo, kutoka kulia ni Makamu Mwenyekiti wa
TASWA Maulid Kitenge, Mwenyekiti Juma Pinto, Mgeni rasmi Ridhiwan
Kikwete na kushoto ni George John Katibu Msaidizi.
Mtaalam
wa SACCOS kutoka Manispaa ya Ilala Bw. Luambano akitoa mada kuweka na
kukopa kwa waandishi wa habari wanachama wa TASWA waliohudhuria katika
mkutano huo
Kutoka
kulia ni waandishi wakongwe Mwina Kaduguda, Mzee Wlly Chiwango na Mzee
Salim Said Salim kutoka Zanzibar wakiwa katika mkutano huo.
Kutoka kulia ni Shafii Dauda, Erasto na Ibrahim Masoud wakiwa katika mkutano huo.
Kutoka kulia ni Elizaberth Mayemba , Timzo Kalugira na Crala Alphonce wakifuatilia mada katika mkutano huo.
Kutoka kushoto ni Elius Kambili, Alfred Lucas na Salum Jaba wajumbe wa kamati ya utendaji ya TASWA wakiwa katika mkutano huo.
Kutoka kulia ni Mgaya Kingoba, Salum Jaba, Richard Mwaikenda na Tulo Chambo wakifuatilia mada katika mkutano huo.
Wajumbe
mbalimbali wakihudhuria mkutano wa Chama cha Waandishi wa habari za
michezo TASWA kwenye hoteli ya Kiromo View mjini nje kidogo ya mji wa
Bagamoyo mkoani Pwani .
Flightlink yawaandalia chakula cha jioni wafanyakazi wake na familia zao katika kuuaga mwaka
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Ndege ya Flightlink,Munawer Dhiren akizungumza
wakati wa hafla ya chakula cha usiku kilichokuwa kimeandaliwa maalum kwa
ajili ya kukutana kwa wafanyakazi wote wa kampuni hiyo pamoja na
familia zao ikiwa ni sehemu pia ya kuuaga mwaka iliyofanyika kwenye
Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ndege ya Flightlink,Munawer Dhiren akiendelea kuzungumza.
Sehemu
ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Ndege ya Flightlink pamoja na familia zao
wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo,Munawer
Dhiren (hayupo pichani) wakati alipokuwa akizungumza nao wakati wa hafla
ya chakula cha usiki iliyokuwa imeandaliwa maalum kwa ajili ya kukutana
kwa wafanyakazi wote wa kampuni hiyo pamoja na familia zao ikiwa ni
sehemu pia ya kuuaga mwaka iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini
Dar es Salaam jana.
Mazungumzo ya hapa na pale kwa wadau wa Kampuni ya Flightlink yakiendelea wakati wa hafla hiyo.
Wakati wa Chakula uliwadia na kila mmoja alipita kuchukua chakula akipendacho.
Baadhi
ya wafanyakazi wa Kampuni ya Flightlink wakipozi kwa picha wakati wa
hafla ya chakula cha usiki iliyokuwa imeandaliwa maalum kwa ajili ya
kukutana kwa wafanyakazi wote wa kampuni hiyo pamoja na familia zao
ikiwa ni sehemu pia ya kuuaga mwaka iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena
jijini Dar es Salaam jana.
Picha ya pamoja kwa wafanyakazi wote wa Kampuni ya Ndege ya Flightlink.
Wakurugenzi wa Kampuni ya Flightlink wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wageni waalikwa.(Picha zote na Othman Michuzi).
Unique Model 2012 Mrembo wa Apatikana
Washiriki waliongia tano bora. |
Washiriki waliongia tano bora. |
Majaji wa shindano hilo kutoka kushoto ni Gymkhana Hilal kutoka Paka Wear , Asia Idarous na Martine Kadinda. |
Unique Model Talent of the year 2012 Vestina Charles akionyesha uwezowake wa kucheza jukwaani. |
Wakitumbuiza mashabiki mapema kabla ya kuingia kuonyesha mavazi ya aina mbalimbali. |
Washiriki 12 wa shindano hilo wakiwa wamejipanga tayari kusubiri kutangazwa mshindi. |
ARUSHA KUWA MAKAO MAKUU YA CHAMA CHA NGUMI ZA KULIPWA AFRIKA YA MASHARIKI NA KATI (ECAPBA).
Chama
cha Ngumi za Kulipwa Cha Afrika ya Mashariki na Kati (ECAPBA) kimepata
nyumbani baada ya Mstahiki Meya wa jiji la Arusha Mh. Gaudence Lyimo
kuomba kihamie Arusha ili kiweze kukaa karibu na “Jumuiya ya Afrika ya
Mashariki, EAC”Rais
wa ECAPBA Onesmo Ngowi alimhakikishia mstahiki meya kuwa ECAPBA
itahamishia makao yake makuu katika jiji la Arusha. Kwa sasa ECAPBA ina
makao yake makuu katika Halmashauri ya Manispaa ya Moshi.
Juhudi
za Mstahiki Meya Gaudence Lyimo za kukuza michezo na kukuza utalii
katika jiji la Arusha ni moja ya sababu zilizomfanya rais wa ECAPBA
kuamua kuhamishia makao makuu katika jiji la Arusha.
Uamuzi
huo uliungwa mkono na mmoja wa wanachama wa ECAPBA bw. Daudi Chikwanje
ambaye ndiye Katibu Mkuu wa Chama Cha Ngumi za Kulipwa Cha Malawi!
Nchi
ya Malawi ni mwanachama wa ECAPBA pamoja na Kenya, Zambia, Ethiopia,
Burundi, Sudan ya Kusini, DRC, Rwanda, Uganda na Sudan.
ECAPBA inaratibu ubingwa unaojulikana kama ECAPBF ambao unawapa mabondia wa ukanda huu kuwa mabingwa imara wa ngumi Afrika.
Friday, December 28, 2012
MATUKIO KATIKA PICHA
Kutokana na Hali ya Maisha Kuwa Ngumu, wakazi wa Manspaa ya mji wa Moshi wakiwa katika harakati na Biashara ya kuuza Matunda, katika kipindi hiki kuelekea Mwisho wa Mwaka (1)
Soko la Bidhaa za watu wenye imani ya Rasta inazidi kushamili huku bidhaa hizo pia zikizidi kuwekewa ubunifu kama inavyoonekana , Mkazi wa Manspaa ya Mji wa Moshi akiingia kupata moja ya Bidhaa hizo (1)
Matukio Mbali Mbali katika Picha
Mabango ya barabarani yanaendelea kuujaza mji wa Moshi kitendo ambacho kinakuwa kero, baada ya kujazana kila kona (2)
Mafundi wajenzi wa Manspaa ya mji wa Moshi wakiendelea za Ukarabati wa Mitalo katika Kipindi hiki cha Mwisho wa Mwaka (1)
Mjasilia Mali akiendelea na Pilika pilika wakati wa kutafuta chochote kitu
Mjasilia Mali(Mama Ntilie wa Migamoni Mama Lishe)wakiwajibika kuandaa chakula kwa ajili ya wateja wao (6)
Pamoja na kuwa na sifa ya Usafi Mji wa Moshi, Lakini Bado ustaarabu kwa watu wengine si kurizisha, hapa wakiendelea na usafi Watu wa Halmashari (Picha Mchimati@faceboo.com)
Subscribe to:
Posts (Atom)