BAADHI askari wa kike wa Jeshi
la Polisi nchini (WP), wameulalamikia uongozi wa jeshi hilo
kutowapandisha vyeo kwa muda mrefu tofauti na wenzao wa kiume ambao
wamekuwa wakipandishwa mara kwa mara.
Hatua hiyo imekuja baada ya
askari hao kukutana mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam katika kikao
cha siri chenye lengo la kutafuta suruhisho la tatizo hilo.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake
jijini Dar es Salaam jana, mmoja wa askari hao, kwa sharti la kutotajwa
jina, alisema suala la kutopandishwa vyeo limekuwepo kwa muda mrefu
bila hatua zozote kuchukuliwa na uongozi wa jeshi hilo.
Alisema anastaajabishwa na
utaratibu uliopo kwa sababu, licha ya kupewa mafunzo pamoja, bado
wanagandamizwa pindi wanaporudi kwenye vituo vya kazi, ambapo askari wa
kiume kupewa upendeleo wakupandishwa cheo haraka.
“Tunashangaa utaratibu huu
utaisha lini, kwani sheria za jeshi letu zinasema kuwa askari yoyote wa
kike au wa kiume anapaswa kupandishwa cheo baada ya muda mchache wa
kumaliza mafunzo” alisema askari huyo.
Askari huyo aliongeza kuwa
endapo ikitokea askari wakike kupandishwa cheo kwa muda sitahiki, eidha
ni kwa kujuana, ukabila na mkubwa fulani au kutoka kijiji kimoja.
Pamoja na hayo, aliivitaja
baadhi ya vyeo ambavyo wamekuwa wakivilalamikia kutopewa ni kama
Msaaidizi wa polisi, Msaidizi wa Inspekta wa polisi, Inspekta wa Polisi,
na vingine ambavyo wamekuwa wakitaka kupandishwa.
Kwa mujibu wa askari huyo, vyeo
ambavyo vimekuwa vikitolewa kwa askari hao ni usajenti na koplo ambavyo
hukaa navyo hadi kustaafu kazi au kufariki.
Alipoulizwa Mrakibu Msaidizi wa
Polisi (ASP), Advera Senso, ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Jeshi hilo,
kuhusu nadai hayo, alisema mfumo wa upandishwaji vyeo katika jeshi hilo,
ni wakawaida ambapo kigezo kuu ni sifa.
“Hakuna askari
wakike wala wakiume bali wote ni askari na wako sawa kigezo kikubwa
kinachoangaliwa katika upandishwaji vyeo hivyo ni sifa”alisema Senso
Alisema mfumo wa jeshi hilo,
unawachukulia kuwa askari wote kuwa wako sawa, pale inapotokea askari
wakiwemo wanawake kama waana sifa zinazostahili kupandishwa cheo
inafanyika hivyo na si vinginevyo.
No comments:
Post a Comment